Mianaume ndo tulivyo......hovyoooo!

Mianaume ndo tulivyo......hovyoooo!

Sorry sana ndugu yangu Bishanga, utanisamehe kwa comment yangu. Yaani ni muda mrefu sana huwa nakuhisi kuwa wewe ni mmoja wa wanaJF wanao fake gender... sijui kwa nini, lakini niwie radhi.
huna haja ya kuomba radhi,its all about perception,kwa hiyo kwa uzi huu ume conclude kuwa Bishanga ni mwanamke?
 
Hebu fikiria:

1.Uko ndani ya ndoa,mwaka wa kumi sasa na hamjapata mtoto, mkeo hospitali zote kamaliza na anaambiwa hana tatizo,kila akikwambia na wewe ukapimwe hutaki unajidai huna tatizo,ndo nini sasa hiyo? Kwa nini usipimwe mkajaribu IVF?

2.Ukienda Rose Garden we ndo Reginald Mengi kazi kuzungusha raundi huku ukijidai kusema...'uza nyumba utunze heshima bar'....asubuhi mwanao akikwambia 'baba shati la shule limechanika'..unakuwa mkaaaaaali,hovyooooo!

3.Umetoka zako kwenye mipombe,ni saa saba za usiku ,mama siku nzima mihangaiko kachoka we ukifika kitandani na ny....zako unamrukia tu bila hata maandalizi....ku ku...ku .....aaaaaaaagh....halafu huyo unakoroma,yaani mpaka mkeo anaona ka alikuwa anaota hivi,jamani hiyo sio baiskeli ya gym huyo ni binadamu ati.

4. Mnawaita beki tatu ma haus geli hao,juu ya nini unajipoza kwa mtumishi wa ndani? huoni unamdhalilisha mwenzio? Hivi ukibambwa utasema nini?

5.Ulipompenda ulimkuta ana kakazi kake,we na miwivu yako hutaki afanye kazi unamwachisha,hivi una uwezo wa kumpatia mahitaji yake yote yakiwemo matunzo ya wazazi na ndugu zake? Halafu kwa nini utake mwenzio kazi yake iwe kusafisha makochi na kuangalia plasma wakati wewe uko bize unachangamsha mwili na akili? Kufanya kazi au biashara is more than kuingiza kipato ,na ku interract na watu pia is healthy.

6.Mkeo akikusoea unaanza kumtangaza kwa watu...'mkeo wangu sijui yukoje....mara hivi mara vile.....huoni unajiaibisha mwenyewe?

7.Na hizo nyumba ndogo hizo,ukienda huko kazi kumsimanga mkeo,matokeo yake siku mkeo akigombana na hawara yako anashangaa matusi anayovurumishiwa...we nae mwanamke wewe...si kikojozi wewe....du toba yarabi!

8.Ukiumwa kidogo tu full madeko yaani unajitia hata kidole huwezi kukisogeza,mwenzio serious tumbo linamsumbua,hata kusema ngoja nikae ndani nimuuguze mwenzangu ndo kwaaaanza unawahi kaunta Jackies,sana sana unampigia simu dada yako akamwangalie wifi,inahuu kwani yeye ndo kamwoa,akilalamika mkeo unamsimanga eti anadeka.

9.Nje utembee sasa ndo hata kuzaa uzae kabisa huko? maduka zinakouzwa condoms huyajui? au utasingizia ilikupasukia,na wa pili nayo ilipasuka? acheni hizo!

10.Huko kwenye mabaa na huo upuuzi unaoongelewa huko ....eh chapati shurti ikaangwe pande zote...sijui nini sijui nini...unarudi nyumbani na mipombe yako unataka ujaribu upuuzi wako kwa mkeo,peleka huko ujinga wako.

11.Umelala nje asubuhi unajitia kurudi nyumbani umefungwa pingu ili mke aone ulilala kituoni,mambo ya 1947 hayo,kinamama hawadanyiki na hizo siku hizi!

12.Mpira ..mpira...mpira....hamchoki? wikiendi nzima uko bar unaangalia mpira ,jumamosi man siti vs man yu,jumapili aseno vs chelz, weekdays kazi,hivi lini unakaa na kukagua kazi za watoto za shule? lini unakaa na mke na wanao na ku chat nao? mpira ndo utakaokuzika?

13. Ubinafsi wako huo,ukikaa sebuleni remote control haiko mbali na wewe unabadilisha tu chanel,si umuulize mkeo au wanao kama nao kuna kitu wanataka kuangalia? kuna mtu aliwahi kusema eti wanaume huona remote control kama ni extension ya mb....zao.

14.Sijui ndo umepiga wapi kabomu kako cha kwanza unamnunulia hawara yako ka vitz wakati mkeo anapanda daladala,kha!

15.Mke akilalamika mitabia yako mibovu unaanza..'kwani unataka nini..gari nimekupa..zaabu nakununulia...frigi imejaa chakula...kelele za nini? kwani kwao hakuacha chakula? yeye alikufuata wewe ati na sio plasma yako.

.......itaendelea....leo wababa wa humu ndani nakula nao sahani moja!

Mkuu naomba mwongozo wako hapo kwenye Blue, ulisema mwanzo kabisa kuwa hao ndugu zako hawana watoto so.........

 
Tatizo kubwa hapa ni maudhui ya hii thread ya Bishanga kuwa kila mwanaume ni mlevi, kila mwanaume ni mshabiki wa mpira wa miguu hasa ligi ya uingereza, kila mwanaume ni fuska na ana nyumba ndogo au anatembea na house girl, kila mwanaume hana muda na familia yake na amewatelekeza watoto. Hii siyo sahihi hata kidogo na mtu responsible hawezi akaiacha mada kama hii ipite bila kurekebishwa. Nimefuatilia thread za akina mama inaonekana wengi wanakubaliana na huo mtazamo wa Bishanga na wengine wanahamu ujumbe uwafikie waume zao. Wasichotaka kukiri ni kuwa wapo wanaume wengi ambao hawaingii kwenye hii "stereotying" ya Bishanga kuhusu wanaume. Hii thread haiwatendei haki wanaume ambao:
  • siyo walevi kwa hiyo hawakai bar muda huo anaosema Bishanga,
  • siyo washabiki wa mpira wa miguu kiasi cha kukesha wanaangalia mpira,
  • wanahudumia familia zao kwa hali na mali,
  • wake zao wanafanya kazi na bado wanawapa huduma zote kama wanawake ndani ya nyumba,
  • hawadeki wanapougua kama anavyotaka kutuaminisha,
  • hawana muda wa kunyang'anyana remote na watoto - Mfano kwangu watoto hawaruhusiwi kuangalia TV muda wote na vipindi wanavyoangalia vinadhibitiwa: siyo kila kipindi watoto wanaruhusiwa kuangalia; Huo ni utaratibu wa taasisi ya familia yetu ya Tata & family.
  • hawaongei habari za wake zao nje - hili hata mila na desturi zetu wengine haziruhusu na sijawahi kukaa chini na rafiki au hata ndugu zangu kujadili matatizo ya familia yangu. Siamini kama hii ni njia sahihi ya kutatua matatizo kama yapo.
  • Hawatembei nje na vimada/malaya
Hoja yangu ya msingi ni kuwa siyo sahihi kuchukua tabia mbovu za wanaume wachache ukadhani ndio tabia za kila mwanaume. Sipingi kimsingi kuwa kuna baadhi ya wanaume wana hizo tabia kama ambavyo tumeshapata ushuhuda wa baadhi ya wachangiaji wanawake humu ndani - Japo siamini kuwa wote waliochangia wanakutana na matatizo hayo. Ni muhimu kuwaeleza hata hao kina mama wenye wanaume wasiowajibika "irresponsible" kama hawa wa Bishanga kuwa siyo kila mwanamke aliyeolewa anakutana na matatizo kama hayo.

Baelezee mkuu, alafu napata shida kidogo, hivi huyu Bishanga ni MWANAMUME AU MWANAMKE?
 
Bishanga bana,Aspirin hajaukubali uzi wako pia!Kasema hauna point za msingi!
 
Mkuu naomba mwongozo wako hapo kwenye Blue, ulisema mwanzo kabisa kuwa hao ndugu zako hawana watoto so.........

Mkuu umenielewa hapo? Kila point 1 to 15 iko independent of each other.
 
Baelezee mkuu, alafu napata shida kidogo, hivi huyu Bishanga ni MWANAMUME AU MWANAMKE?
bona baana bona baana bona bana lutambukage mbaluga omumalembo,
nolya noyenda nolya noyenda,
nolya noyenda.......hahahahahaha bishanga male or female? Wewe ni wa pili kuniuliza hili swali leo.
 
Kama gender yake unknown! Basi amekua Samenya (yule mwanariadha wa S. Africa) au ?

Mh yan amekuwa dumejike kisa leo yuko against u guyz .... loh! bishanga atakuwa "He" Tu apo ameamua tu kufunguka! achen izooo.
 
Namba nane MmmH!!!, imekupunguzia heshima,,, mwanaume kusema "inahuu" ni dalili ya ukameruni, sijawahi ona hii tokea nizaliwe.
 
Namba nane MmmH!!!, imekupunguzia heshima,,, mwanaume kusema "inahuu" ni dalili ya ukameruni, sijawahi ona hii tokea nizaliwe.
si ndo mana mjadala unaendelea kama bishanga ni He au She?
 
Eiyer hii ndio thread ulikua ukitaka ya B'?
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada angepaswa kusema "Baadhi ya mianaume...."

Si sawa na si uungwana kujumuisha wanaume wote na hayo mapungufu!
 
......hahahhahaaaaaaaaaaa...... kama yupo mwanaume atayechenga yote hayo.........Mungu tusaidie na tuepushe na hizi mishemishe.....
 
Back
Top Bottom