Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,131
Azimio jipya,
Ndugu yangu sgukran sana kwa kipande ulichotupa link. Huyu mwandishi Robert Mndeme bomba sana na hsa nukuu hii hapa imenifungua:-
Kutoka kitabu 'Maadili ya Taifa na Hatima ya Tanzania', somo la 'Mtazamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu ukombozi', Ibrahim Mohamed Kaduma anaandika: "Wakati wa uhai wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julios Nyerere, alitamka kwamba...Ukombozi wa Mtanzania hautakamilika mpaka kupitia hatua kuu tatu: Uhuru wa bendera, Uhuru wa fikra na Uhuru wa kiuchumi.
Tatizo kubwa la Azimio la Zanzibar lilikuwa kuruka kipnde cha uhuru wa Fikra kuingia Uhuru wa kiuchumi. Pengine yawezekana tulichukua muda mrefu sana wakati wa Nyerere tukijazwa Ujinga kwani hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kujikomboa kifikra hasa baada ya kuondoka ktk Ujamaa na kuingia Ubepari. Tulikuwa tumeandliwa kutazama upande mmoja tu na kuwa Ubepari ulikuwa shetani na dhambi kubwa kwa hiyo hatukuweza kujiandaa kifikra jinsi ya kukabiliana na shetani huyo...bado leo hii wananchi tumejaa watumwa wa fikra za mkoloni na viongozi wetu wamechukua nafasi ya mkoloni kuendeleza tawala zote mbili FIKRA na UCHUMI.
Inabidi nikitafute hicho kitabu cha Ibrahim Mohammed Kaduma.....
Ni kweli lazima kukaa na kutafakari kwa kina Ni nini maana ya kweli ya utumwa wa fikra..Tutaupataje..maana lazima kufanya mchakato wa kina ...hivi tunakosea wapi? tunapigwa je magoli na hawa wawekezaje..etc? Tunafikiria kinyumenyume nini? Wanawezaje kuingia fikra za viongozi wetu na kuwamudu kirahisi...Kuna mchezo wa kifikra wanatuchezea nini? Lazima kuwa na Fikra Timamu tunapoingia kwenye vita nzito ... ya kukamilisha uchumi kwa taifa Tz!!!! Kushinda? Tutashinda lakini Tujipangeni!!!! Tena kikamilifu sio masuala ya kukurupuka tu..na kutumia mbinu za kizamani..maadui wako vizuri sana! Inabidi tufanye kazi kwelikweli.. Vinginevyo Tutakuwa watumwa milele!!TUKOMBOENI FIKRA WANA JF!!!!!!!!