Tanzania tuna miaka 63 ya Uhuru lakini kimaendeleo, kisiasa na kidemokrasia tuko juu kuliko Haiti iliyopata uhuru miaka 220 iliyopita. Hongera CCM

Shotocan

JF-Expert Member
Nov 21, 2023
2,216
4,624
Tanzania tuna miaka 63 ya toka tupate uhuru lakini kimaendeleo na kisiasa na kidemokrasia tuko juu, kuliko Haiti iliyopata uhuru miaka 220 iliyopita.

Hongera CCM kwa kuipeleka nchi spidi kali kimaendeleo, kisiasa na kidemokrasia kiasi cha kuiacha nchi ya Haiti mbali huko pamoja nankuwa walipata uhuru kiaka 220 iliyopita.
 
Tusijifananishe na HAITI na kuanza kujisifu .Hiyo nchi imekuwa ikikumbwa na natural Disasters kwa karne nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu,ndio maana wazungu waliamua kuikimbia na kuwaacha watumwa huko waishi maana ilionekana si sehemu salama ya kuishi binadamu.
Haiwezi kupita miaka 5 bila tetemeko kubwa la ardhi au Vimbunga vikubwa kupiga huko na kuharibu miundo mbinu yote .Tetemeko la 2010 lilivunja kila kitu wakaanza upya.Vimbunga vya Huriccanes sijui katrina ndo eneo lake hilo la kujidai.Na ukizingatia watu wenyewe wanaoishi huko ndio sie wamatumbi tusiojiweza kwa chochote basi imekuwa
ni kizingiti kikubwa kwa nchi kusogea maana wakati wote wanawaza kukabiliana na natural disaster.
Yale matetemeko na vimbunga yanayowakumba yangetokea hapa Tanzania usingeongea hayo
Timeline of Haiti’s natural disasters

Timeline: Haiti’s history and current crisis, explained
 
Tanzania tuna miaka 63 ya toka tupate uhuru lakini kimaendeleo na kisiasa na kidemokrasia tuko juu, kuliko Haiti iliyopata uhuru miaka 220 iliyopita.

Hongera CCM kwa kuipeleka nchi spidi kali kimaendeleo, kisiasa na kidemokrasia kiasi cha kuiacha nchi ya Haiti mbali huko pamoja nankuwa walipata uhuru kiaka 220 iliyopita.

Kweli ujinga ni sifa kama ilivyo ufupi au urefu.

Fikiroa mtu analinganisha nchi ambayo eneo lake ni kama ukubwa wa mkoa mmoja wa Tanzania na nchi nzima ya Tanzania.

Tanzania 945,087 sq. Km
Haiti 27,560 sq. Km

Tanzania population 65m
Haiti population 11.45m

Tz GDP per capita $1,080
Haiti GDPper capita $ 1,829

Kwa nini usilinganishe Tanzania na nchi inazofanana au kukaribiana katika mambo mengi kama vile rasilimali asilia, ukubwa wa nchi, idadi ya watu, n.k? Linganisha Tanzania na nchi kama Angola, Ghana, Malaysia, Thailand, Kenya au South Africa?

Hiyo Haiti kwanza ipo kwenye eneo hatari kwa sababu ni ukanda wa tetemeko la ardhi. Mwaka 2010 pekee, karibia watu laki 3 walikufa kwa tetemeko la ardhi.

Throughout its history, Haiti has suffered cyclones, hurricanes, tropical storms, torrential rains, floods, famine, diseases and earthquakes.
 
Tanzania tuna miaka 63 ya toka tupate uhuru lakini kimaendeleo na kisiasa na kidemokrasia tuko juu, kuliko Haiti iliyopata uhuru miaka 220 iliyopita.

Hongera CCM kwa kuipeleka nchi spidi kali kimaendeleo, kisiasa na kidemokrasia kiasi cha kuiacha nchi ya Haiti mbali huko pamoja nankuwa walipata uhuru kiaka 220 iliyopita.
Huu ni ujinga kiwango cha ccm. Ni mawazo ya kujisifu kwa kupiga hatua kurudi nyuma badala ya kwenda mbele. Unawaza na kujisifu kuwa mbele ya Haiti, wenzio Kenya, Botswana, S. Africa, Rwanda etc wanawaza kufikia viwango vya Korea, Singapore, Brazil, hatimaye wawe kama Japan, Ulaya au America.
 
Back
Top Bottom