Tanzania inafikisha miaka 46 ya Uhuru tarehe 9 Disemba 2007.
Ningependa kuwakaribisha wadau kujadili mafanikio makubwa na ya msingi ambayo tumeyapata na vile vile kujadili changamoto tulizonazo na jinsi ya kuzitatua.
==============
1yr later:
Ningependa kuwakaribisha wadau kujadili mafanikio makubwa na ya msingi ambayo tumeyapata na vile vile kujadili changamoto tulizonazo na jinsi ya kuzitatua.
==============
1yr later:
UMEBAKI mwezi mmoja vile Tanzania iadhimishe miaka yake 47 toka iwe huru. Mwanamme wa miaka 47 bila shaka ana mke na angalau watoto wawili. Mwanamke wa miaka 47 nadra tena kupata mwana.
Kwa Tanzania hii yetu sifa yake kubwa katika kutimiza miaka 47 ni nini?
Ninavyoona mimi:
- Kuua taratibu amani na umoja tuliolea kwa shida na taabu;
- Watu kutafutana uadui usio na sababu,
- wabunge kujiwakilisha wenyewe badala ya wananchi,
- mawaziri kuwa matarishi badala ya mameneja.
- watu wa nje kupewa mali asili yetu bure wafaidi wao na sisi tunakosa,
- ubepari umekubalika waziwazi na awamu ya nne bila kuwa na mawazo wala akili ya kupambana na makali yake,
- tumewagawa watoto kati ya watoto wa wale walichonacho na watoto wa wale wasichonacho,
- tukichaji kihalali makampuni au migodi ya dhahabu tunaweza kutoa bure huduma za afya na kugharamia elimu ya wenetu hadi Chuo Kikuu lakini tumeamua kutofanya hivyo kwa sababu wanasiasa na mangimeza wa serikali wanazozijua,
- Serikali imekuwa kubwa mno na inakula ashemu kubwa ya kodi ya wananchi bila sababu ya msingi, ila tu, kwamba sera ya wanasiasa waliopo madarakani ni kutozalisha ila kula sana,
- Pamoja na kutumia fedha nyingi vyombo vya serikali havifanyi vizuri kama vyombo binafsi iwe ni vyombo vya habari, usalama, uchukuzi kama vile vya watu binafsi vinavyotumia fedha kidogo,
- Tumekosa msimamamo wa kuchagua marafiki wa kweli na badala yake tunayumba yumba na kurudi kule kule kwa wale ambao misaada yao na elimu yao na mawazo yao ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo,
Nisimalize yote basi, labda wenzangu na nyie mna maono na uono wenu hebu tubadilishane tujue hali halisi ya Mtanzania miaka 47 baada ya Uhuru.
Kumbuka Botswana, Namibia, Rwanda, Gabon na kadhalika walipata uhuru nyuma yetu lakini wana GDP per capita mara 3 au nne kama sio zaidi ya ile ya kwetu.
Tumepoteza fursa nyingi kama ile ya kwenda kuweka amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na tunaviachia vinchi kama Rwanda kujifanya vijogoo visivyo hata na kilemba achilia mbali mkia!
Tungeliweza kuigeuza nchi yetu SOKO KUBWAAA -soko linalonunua BIDHAA MBALIMBALI toka Mashariki ya Kati na Mashariki ya Mbali na kuuza kwenye maeneo mbalimbali Afrika Mashariki, Kati na Kusini lakini tumeachia fursa hiyo tena ambayo ingelitukomboa kwa kutuwezesha kuwa na mitaji ya kuwekeza kwenye KILIMO na VIWANDA kwa urahisi.
Kama unabisha sio biashara au soko ndiyoinayotajirisha watu nitajie WAKULIMA waliotajirika Tanzania au WASOMI waliotajirika Tanzania au WAFUGAJI waliotajirika Tanzania au WAVUVI waliotajirika Tanzania bila kuuza kitu!
Akili,
Dodoma