Miaka takribani 50 ya Uhuru Tanzania: Ni yapi ya kujivunia?

Azimio jipya,
Ndugu yangu sgukran sana kwa kipande ulichotupa link. Huyu mwandishi Robert Mndeme bomba sana na hsa nukuu hii hapa imenifungua:-
Kutoka kitabu 'Maadili ya Taifa na Hatima ya Tanzania', somo la 'Mtazamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu ukombozi', Ibrahim Mohamed Kaduma anaandika: "Wakati wa uhai wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julios Nyerere, alitamka kwamba...Ukombozi wa Mtanzania hautakamilika mpaka kupitia hatua kuu tatu: Uhuru wa bendera, Uhuru wa fikra na Uhuru wa kiuchumi.

Tatizo kubwa la Azimio la Zanzibar lilikuwa kuruka kipnde cha uhuru wa Fikra kuingia Uhuru wa kiuchumi. Pengine yawezekana tulichukua muda mrefu sana wakati wa Nyerere tukijazwa Ujinga kwani hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kujikomboa kifikra hasa baada ya kuondoka ktk Ujamaa na kuingia Ubepari. Tulikuwa tumeandliwa kutazama upande mmoja tu na kuwa Ubepari ulikuwa shetani na dhambi kubwa kwa hiyo hatukuweza kujiandaa kifikra jinsi ya kukabiliana na shetani huyo...bado leo hii wananchi tumejaa watumwa wa fikra za mkoloni na viongozi wetu wamechukua nafasi ya mkoloni kuendeleza tawala zote mbili FIKRA na UCHUMI.

Inabidi nikitafute hicho kitabu cha Ibrahim Mohammed Kaduma.....

Ni kweli lazima kukaa na kutafakari kwa kina Ni nini maana ya kweli ya utumwa wa fikra..Tutaupataje..maana lazima kufanya mchakato wa kina ...hivi tunakosea wapi? tunapigwa je magoli na hawa wawekezaje..etc? Tunafikiria kinyumenyume nini? Wanawezaje kuingia fikra za viongozi wetu na kuwamudu kirahisi...Kuna mchezo wa kifikra wanatuchezea nini? Lazima kuwa na Fikra Timamu tunapoingia kwenye vita nzito ... ya kukamilisha uchumi kwa taifa Tz!!!! Kushinda? Tutashinda lakini Tujipangeni!!!! Tena kikamilifu sio masuala ya kukurupuka tu..na kutumia mbinu za kizamani..maadui wako vizuri sana! Inabidi tufanye kazi kwelikweli.. Vinginevyo Tutakuwa watumwa milele!!TUKOMBOENI FIKRA WANA JF!!!!!!!!
 
Mimi ninajua iko siku nitauwa mtu tena mzungu nitampiga risasi kama ataniletea jeuri nitamwonyesha nini waafrika jinsi tusivyotaka upuuzi na kudharauliwa katika continent letu la Africa,washenzi wanatudharau na kutuchukia sana sis waafrica na watu weusi wote duniani.
peace
zee la Ujiji
Karengas
 
Kuvamia nchi za watu under pretext ya ku spread democracy

yaani siku hizi tuna spread democracy kwa mtutu wa BUNDUKI
 
UMEBAKI mwezi mmoja vile Tanzania iadhimishe miaka yake 47 toka iwe huru. Mwanamme wa miaka 47 bila shaka ana mke na angalau watoto wawili. Mwanamke wa miaka 47 nadra tena kupata mwana.

Kwa Tanzania hii yetu sifa yake kubwa katika kutimiza miaka 47 ni nini?

Ninavyoona mimi:
- Kuua taratibu amani na umoja tuliolea kwa shida na taabu;
- Watu kutafutana uadui usio na sababu,
- wabunge kujiwakilisha wenyewe badala ya wananchi,
- mawaziri kuwa matarishi badala ya mameneja.
- watu wa nje kupewa mali asili yetu bure wafaidi wao na sisi tunakosa,
- ubepari umekubalika waziwazi na awamu ya nne bila kuwa na mawazo wala akili ya kupambana na makali yake,
- tumewagawa watoto kati ya watoto wa wale walichonacho na watoto wa wale wasichonacho,
- tukichaji kihalali makampuni au migodi ya dhahabu tunaweza kutoa bure huduma za afya na kugharamia elimu ya wenetu hadi Chuo Kikuu lakini tumeamua kutofanya hivyo kwa sababu wanasiasa na mangimeza wa serikali wanazozijua,
- Serikali imekuwa kubwa mno na inakula ashemu kubwa ya kodi ya wananchi bila sababu ya msingi, ila tu, kwamba sera ya wanasiasa waliopo madarakani ni kutozalisha ila kula sana,
- Pamoja na kutumia fedha nyingi vyombo vya serikali havifanyi vizuri kama vyombo binafsi iwe ni vyombo vya habari, usalama, uchukuzi kama vile vya watu binafsi vinavyotumia fedha kidogo,
- Tumekosa msimamamo wa kuchagua marafiki wa kweli na badala yake tunayumba yumba na kurudi kule kule kwa wale ambao misaada yao na elimu yao na mawazo yao ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo,

Nisimalize yote basi, labda wenzangu na nyie mna maono na uono wenu hebu tubadilishane tujue hali halisi ya Mtanzania miaka 47 baada ya Uhuru.

Kumbuka Botswana, Namibia, Rwanda, Gabon na kadhalika walipata uhuru nyuma yetu lakini wana GDP per capita mara 3 au nne kama sio zaidi ya ile ya kwetu.

Tumepoteza fursa nyingi kama ile ya kwenda kuweka amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na tunaviachia vinchi kama Rwanda kujifanya vijogoo visivyo hata na kilemba achilia mbali mkia!

Tungeliweza kuigeuza nchi yetu SOKO KUBWAAA -soko linalonunua BIDHAA MBALIMBALI toka Mashariki ya Kati na Mashariki ya Mbali na kuuza kwenye maeneo mbalimbali Afrika Mashariki, Kati na Kusini lakini tumeachia fursa hiyo tena ambayo ingelitukomboa kwa kutuwezesha kuwa na mitaji ya kuwekeza kwenye KILIMO na VIWANDA kwa urahisi.

Kama unabisha sio biashara au soko ndiyoinayotajirisha watu nitajie WAKULIMA waliotajirika Tanzania au WASOMI waliotajirika Tanzania au WAFUGAJI waliotajirika Tanzania au WAVUVI waliotajirika Tanzania bila kuuza kitu!



Akili,
Dodoma
 
Na sasa mambo ndio magumu zaidi tusitegemee misaada kama tulivyozoea maana huko majuu wenyewe wako hoi bin taaban.
Tukumbuke maneno ya Mwalimu Nyerere alipotuambia WaTanzania Uchumi tunao lakini tunaukalia.
Naona umefika wakati wa kuamka na kuanza kuutumia uchumi ili tuondokane na bajeti tegemezi.Ndipo tunaweza kupima maendeleo kwani haya tuyaonayo ni maendeleo hayamsaidii Mtanzania wa kawaida bali ni maendeleo ya wachache ambayo huwanufaisha wachache hao na familia zao,si mnaona makodi yanavyoongezeka wakati faida ya kodi hizo hazionekaniki wanazirundika mabenki na kuzichukua kwa mlango wa uwani.
 
Tanzania ina umri sawa na Obama: Yeye kapiga maendeleo, Tanzania imepinga maendeleo
 
Sahihisho -Tanganyika ndio inayoadhimisha Uhuru ilioupata 1961 na sio Tanzania, jamani TANZANIA haikuwepo wakati huo au ilikuwa haijazaliwa.Sijui kwa nini tunaonaga tabu kusema Uhuru wa Tanganyika ?
 
Sahihisho -Tanganyika ndio inayoadhimisha Uhuru ilioupata 1961 na sio Tanzania, jamani TANZANIA haikuwepo wakati huo au ilikuwa haijazaliwa.Sijui kwa nini tunaonaga tabu kusema Uhuru wa Tanganyika ?

You are right
 
Cha kufedhehekea ni kwamba nchi inaongozwa na genge la wahuni waliokosa mbele wala nyuma na wala hatuna cha kujivunia!
 
Kwako ndugu Akili:

Mada kama hizi zitaanza kuleta emotions hapa. Kuna watakaosema Nyerere alisema hivi. Mwinyi alifanya vile. Mkapa kavuta uchache na JK anachemsha.

Kwa maoni yangu naona tuacha kupima maendeleo yetu kwa kutumia migodi ya dhahabu na mbuga za wanyama. Na tuweke vipimo vipya ambavyo vitaangalia maisha ya watanzania wengi kwa kila siku.

Kwa mfano tuweke wastani wa matumizi ya chakula kwa mtanzania wa kawaida kwa kila siku. Mtanzania wa kawaida anatakiwa ale kifungua kinywa chenye vitumbua viwili na kikombe kimoja cha chai au kahawa. Chakula cha mchana awe anapata ugali na maharage au nyama. Chakula cha usiku ugali, mtori au wali na kuku.

Na kwenye malazi, ziwepo index zake. Na kwenye elimu ziwepo index zake. Na juhudi za serikali ziwe kuwafanya wananchi wengi kufikia index hizo kwa kupewa misaada na serikali au kwa kutumia uwezo wao binafsi.
 
Maendeleo ya nchi sio kitu cha overnight despite matatizo ya hapa na pale tunakwenda mbele japo in snailing pace
 
Wakati wa utawala wa Wakoloni walilenga kuimarisha kundi dogo la kuwalinda ili waendelee kuwa madarakani. Hata katika utawala uliopo, wako watu wachache sana ambao ndo wanafaidi matunda ya nchi hii na walalahoi ndo wengi. Tunaweza kutofautisha utawala huu kwa yapi?

nawasilisha
 
Wakati wa utawala wa Wakoloni walilenga kuimarisha kundi dogo la kuwalinda ili waendelee kuwa madarakani. Hata katika utawala uliopo, wako watu wachache sana ambao ndo wanafaidi matunda ya nchi hii na walalahoi ndo wengi. Tunaweza kutofautisha utawala huu kwa yapi?

nawasilisha

There is no difference, agenda ndiyo ile ile. Only that wakoloni walitumia too much physical power, hawa more of soft power.Matokeo ni yale yale.
 
tofauti ni kuwa mkoloni aliondoka na hakurudi.

No my dear,mkoloni yupo hapa,tena ukoloni huu ubaya wake ni kwamba tunajipeleka wenyewe kwa hiari kwa hiyo sio rahisi kutoka. Ukoloni huu is by remote control.
 
Nimefurahi sana, ila mpwa tofauti ipo kubwa sana, moja; wao walitumia fullkobe, hawa wa sasa wanatumia V8, Pili, wale walitumia viwanda vidogo vidogo(processing ind) hawa wameviuza kabisaa( akili au matope) wale hawakuiba pesa hawa wanaiba pesa, rasilimali, utu na afya zetu, wale walituua publicly ( mauaji yakawa machache) hawa wanatuua kimyakimya na hivyo tutakufa wengi kwa muda mrefu( northmara) haya nawaachia wengine waendelee...
 
Bora ukolio ondoka kuliko makamuzi ya ccm, chumvi na khanga unachgua kiongozi???? Huu utawala wa ccm ni hatari na kandamizi zaid ya mara 100 wa wazungu mwalim aliowatimua akidhani kuna mbegu nzuri ipo akaachia madarka manyangau. Hii nommmmmmma mbaya
 
Wakati wa utawala wa Wakoloni walilenga kuimarisha kundi dogo la kuwalinda ili waendelee kuwa madarakani. Hata katika utawala uliopo, wako watu wachache sana ambao ndo wanafaidi matunda ya nchi hii na walalahoi ndo wengi. Tunaweza kutofautisha utawala huu kwa yapi?

nawasilisha

Oh! lovely, baada ya kuondoka wakoloni waingereza walikuja wakoloni wanaoitwa CCM, ambao mpaka leo wanaitawala Tanzania.

Tukipata katiba mpya yenye kuaccomodate vyama vyote then that will be real freedom!!! n
 
Back
Top Bottom