Miaka inaenda sioni Future yangu. Nimekata tamaa!

MIAKA IMEENDA SIONI FUTURE YANGU; NIMEKATA TAMAA!

Kwa Mkono wa Robert Heriel.

"Nina miaka 33, sina mke, sina mtoto, sina kiwanja, Kodi inanishinda, wala sio Kodi nyingi haifiki hata elfu 50 Kwa mwezi lakini inanitoa jasho kuilipa, chakula nakula Kwa mbinde Kama mvuta upinde. Mavazi yangu ni duni, sikutegemea mambo yawe hivi, tangu nikiwa Chuo nilifikiri ningefanikiwa mapema mara tuu nitakapomaliza shule. Lakini mambo yamekuwa mbali mno na matarajio yangu. Nikikuambia naendelea na mapambano ninakudanganya, nimekata matumaini.

Ona Mimi sio WA kukosa hata hela ya kununulia Dawa ya Meno, ona! Mimi sio WA kukosa sabuni ya kuogea na kufulia hata marapurapu ninayoyavaa! Ona! Mimi sio huyu! Labda Mimi wamenibadilishia. Mimi wakula mlo mmoja kweli!

Hapa sina pakwenda! Kodi nadaiwa miezi mitatu sasa. Mwenye nyumba kanipa notisi kesho kutwa nafurumushwa hapa. Loooh!!

Labda ungefikiri nilimuasi Mungu Kwa kutokwenda kwenye nyumba zake za ibada, lakini sivyo. Nilikuwa Muumini mwaminifu hapo awali kabla sijageuka muasi, uasi uliosababishwa na mambo yangu mengi kwenda mrama huku watumishi wakinitoza kila nifikapo kwenye nyumba za Ibada. Nikaasi nikasema kumbe kuabudu Napo ni mpaka ulipie. Nikaacha kwenda huu mwaka wa Saba sasa.

Nataka kuoa lakini Nani akubali Hali yangu dhalili na fukara. Wanawake wote wa mjini hutaka maisha ya magari, urembo na majumba ya kifahari. Nitawawezea wapi.

Usifikiri kuwa nilizembea kwenda huko vijijini, nilifika mpaka Makanya huko, nikateremkia Saidong mpaka Hanang huko ndani ndani, nikapandisha mpaka vijiji vya Singida mpaka nilipojikuta Kibati huko Turiani Morogoro, kote huko kutafuta mwanamke wa kijijini, lakini niliambulia patupu.

Si ungenilaumu Kama sikufika kule kwenu Handeni, nilifika kote huko mpaka Lushoto nikapandisha milima ya shambalai kote huko licha ya kuwa na wasichana wazuri lakini kote walikatalia. Ati walihitaji mwanaume kwenye wadhifa na Mali walau Mbuzi wawili tuu. Nikawaza Mimi haya kuku mmoja sina sembuse Mbuzi. Loooh! Nikamkumbuka Paka wangu mzuri wa madoa doa niliyemfuga anikamatie panya na mende waliokuwa wakinisumbua humu ndani lakini Paka Yule Kwa hila akanikimbia akaenda Kwa jirani yangu huyo hapo nje mwenye Geti la rangi ya kijivu.

Paka Yule huenda alichoka Kula Mlo mmoja, kila siku Panya tuu na hata akikosa panya angekula Mende. Nani angekubali mlo mmoja miaka nenda Kula Milo mmoja. Hata Mimi huenda nisingekubali Kama kuna nafasi ya Kula minofu.

Siku hizi Paka wangu namuona juu ya kuta za jumba la jirani yangu. Hunitazama Kwa jicho la Dharau na mara huachia mlio wa dhihaka. Basi hasira hunipandaga sana, naokotaga jiwe ili nimpige lakini Paka Yule hata hashtuki kunikimbia. Aaargrrrrrrrhii! Sitaki Kueleza haya.

Ningetaka niwe mganga wa jadi, nipige Ramli chonganishi nijipatie kipato. Wazo hilo likanipeleka mpaka Pangani huko nikajifunze elimu ya uganga na uganguzi. Niliishia kutapeliwa na hata nilipohitaji Utajiri wakaishia kuugeuza mwili wangu uwanja wa viwembe, ninachale Mimi mpaka sehemu nyeti.
Nafikiri hata siku Mungu akinijalia mara paap nikatusua maisha na kuoa, huyo mwanamke ataniona Mimi ni mlozi niliyebobea haswa. Tena angeniona Mali zangu niza ndagu.

Haya tuachane na hayo!

Embu niambie Rafiki yangu utanisaidia nini maana mambo yangu yameniendea mrama. Macho haya ni mapambo tuu hayaoni mbele.
"

Akasema akinitazama!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Makanya, Kilimanjaro
Wewe unakaa Makanya Kijiji kilichojaa wachawi, Kijiji kilichojaa Malaya, Kijiji chenye ukame wa kupitiliza unategemea kutoboa?
Halafu huwaheshimu mama zetu mpaka unasema hawastahili huruma huoni kwamba unajiwashia Moto?
Hapo Makanya utaendelea kuona magari ya wachagga wakienda kwao kula Bata.
Nyie watu wa Makanya mnasubiri ajali zitokee muwaibie majeruhi unadhani baraka mtazipata wapi?
Kingine watu wa Makanya mna roho mbaya sana za kishirikina, kweli baraka zitakuja Makanya?
Endelezeni uchawi muone Kama mtafika popote.
 
"Siku hizi Paka wangu namuona juu ya kuta za jumba la jirani yangu. Hunitazama Kwa jicho la Dharau na mara huachia mlio wa dhihaka."

Dah
 
Ukikutana na alokusimulia muulize hv... "Nauli ya Hizo route alizokuwa anapiga ktk kutafuta mwanamke wa kijijini alizitolea wapi?"

Saidong to Hanang = 7000
Hanang to Ngamu( singida) = 5000
Ngamu to Singida mjini =4000
Singida to Morogoro =25000.
Morogoro to Mbingu = 15000 to and fro = 30000
..........

Nisaidieni afike Tanga na vijiji vyake af aje aseme anakosaje kodi na uhakika wa kula.
 
Ukikutana na alokusimulia muulize hv... "Nauli ya Hizo route alizokuwa anapiga ktk kutafuta mwanamke wa kijijini alizitolea wapi?"

Saidong to Hanang = 7000
Hanang to Ngamu( singida) = 5000
Ngamu to Singida mjini =4000
Singida to Morogoro =25000.
Morogoro to Mbingu = 15000 to and fro = 30000
..........

Nisaidieni afike Tanga na vijiji vyake af aje aseme anakosaje kodi na uhakika wa kula.


Ngoja napandisha Uzi wa safari zangu za malori na mafuso
 
Ngoja napandisha Uzi wa safari zangu za malori na mafuso
kwa uandishi nakupa 100% mkuu. Nikipata muda nitakuuliza swali hili... "Hio sanaa unaoinaje kwa jicho la tatu?"..... Ni ya kuishia JF au uko na mkakati mwingine mbali na hapa....?
 
Kama upo makanya shuka tu hapo combo muungano au turiani nunua samaki za laki moja njoo nazo Hadi lami uza utanishukuru
 
Uandishi ndio kitu kikubwa kucheza na maneno na fasihi sio kitu kidogo mkuu


Moja ya kazi zangu humu jamvini na kitabu kipo sokoni mwezi January
👇👇
 
Back
Top Bottom