Nimemuacha baada ya kutaka kumuua paka mwenye mimba!

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Kuna wamanzi ni wakatili sana

Kuna demu nilikua naishi naye sasa ni siku kadhaa mwanzo alikuwa anakuja na kuondoka

Ila majuzi akalowea mazima kakaa kama siku nne hapa na nikajiset kichwan kwamba nitulie na huyu na ikifaa nije kumuoa siku za usoni maana tayari nishamlabel kama future wife

Sasa hapa jirani kuna paka ana mimba tena kubwa sana ni paka mstaarabu sana hana sifa ya udokozi wala nini ila sasa mwenye paka alihamia mkoani sasa alishindwa kuhama na Paka basi yule paka akawa kaachwa tu anashinda mazingila ya hapa hapa.

Alikua anateseka sana unakuta analia njaa tu maana hajazoea maisha ya maporini nikawa nikija nikila basi nitamwita na kumpa mabaki ya chakula

Siku zikaenda akanizoea sana mwisho akawa ni kama paka wangu tu akahamia kwangu akawa anashinda hapa.

Nikawa nampa chakula kila msosi lazima nimtengee kidogo hata kama hayupo nitamuwekea tu kwenye kisosi najaza vizuri sasa ana mimba kubwa sana mimi napenda sana paka wala hajaharibu chochote nilitoka nimerudi nakuta paka hayupo namuuliza mwenzangu hanipi majibu.

Kuambiwa kumbe nikitoka huwa anamfukuza yule paka na kumpiga sasa kaona haitoshi kaenda kununua sumu ya panya kachanganya kwenye kipolo cha mchuzi wa nyama kwenye kisosi anachoriaga paka narud nakuta ndo anakiweka kisos huko ndani ashachanganya ili paka akija ale kumbana ndiyo akasema alikua anamuwekea paka akasema hapendi paka kwahiyo bora amuue tu kwa sumu.

Nikamuuliza huyo paka kafanya nini mbona sio mdokozi jibu lake ni hapendi paka tu nimekasirika sana sikuwa na budi zaidi ya kumuambia achukuwe nguo zake aondoke.

Kama mwanamke anaweza kumuua paka kiumbe cha Mungu tena mwenye mimba kubwa huo si ukatili?Paka mwenyewe ukimuona utaona huruma mimba yake imekua kubwa analala sana muda mwingi na kachoka sana muda wowote anazaa

Sikutegemea kwakweli, nimemuambia afungashe akuongea akachukua vitu vyake akatoka sahizi anatuma msg za matusi tu hapa.

Kuna watu wana roho mbaya sana napenda paka sana kwenye maisha yangu huwa nakumbuka utotoni nilishuhudia paka wetu akipewa sumu halafu alikua na vitoto vichanga hadi leo naumiaga huwa nakumbuka najiskia hasira na uchungu sana
 
ki ukweli naona sio sahihi kuna mtu hana mapenzi na paka kama mimi napendelea mbwa kuliko paka zaidi....

Paka anakuga na kero zake kama kulialia usiku na ata kila ukitaka kula anakua anasonga njee na kujiliza njaa na kama ashakuambia hapendelei paka muondoe unamng'ang'ani kama paka wa dawa.
 
Umefanya poa mkuu sasa kilichobaki chukua uyo paka ingiza ndani atabeba majukumu ya uyo aliye ondoka.
K ni K haiwezi kuwa M.
Jamaa nampongeza sana kumfukuza huyo mwanamke.
Huwezi kujikaribisha kabla haujakaribishwa halafu bado anamtukana jamaa.
Angekuwa mwanamke mzuri angeomba msamaha. Wanawake wapo wengi wengine mpk wanajiuza huko hawana wa kuwaoa😁😁😁😁😁
 
Jinga kwani unakula paka
Huyo paka anaishi kwenye nyumba ya huyo mwanamke?
Kama anaweza kumuua paka ambaye chakula hampi yeye si ipo siku moja atamuua jamaa?
Kama angekuwa mwanamke mwema angeongea na jamaa kuwa yeye hapendi paka halafu jamaa angejua namna ya kumfanya ili asimkwaze mwanamke.
Mwanamke wa kujibebelea na kuhamia kwako kimya kimya huyo hafai
 
Back
Top Bottom