Ujue ukizoea kukaa karibu na choo kinachonuka, unaweza kuzoea ile harufu ya choo kunuka mpaka akaja mtu aliyetoka kwenye hewa safi akakawambia hapo ulipo pananuka, ukambishia hapanuki, ukasema anakutukana bure tu.mbona sijaona tusi hapo.
hebua ainisha hayo unayosema ni matusi.
@Mleta mada usithubutu kurudi huku nyumbani kuna mateso hasa kama unapenda haki na amani yako.
mkuu asante kwa somo.Ujue ukizoea kukaa karibu na choo kinachonuka, unaweza kuzoea ile harufu ya choo kunuka mpaka akaja mtu aliyetoka kwenye hewa safi akakawambia hapo ulipo pananuka, ukambishia hapanuki, ukasema anakutukana bure tu.
Ndicho unachofanya hapa.
Nilipofika New York City mara ya kwanza, kuna OG mmoja aliniambia hapa kuna machizi kibao wanataka kujionesha wao watoto wa mjini, wana vituko sana, lakini hawa wengi wakuja hapa. Ndio wanaoupa mji sifa mbaya. Akaniambia, sisi wenyewe tuliozaliwa hapa mjini wengi tuko poa sana.
Sasa ninavyoona watu wa "Johnny come lately" waliotoka nyumbani miaka saba iliyopita wanavyokuwa na machepele ya kutukana kwao, nimemkumbuka OG wangu wa New York.
Wakuja juzi huwa wana matatizo mara nyingi sana.
Ma OG waliozaliwa viwanja Brooklyn huko Wanyamwezi wenyewe kina marehemu Ruge Mutahaba huwezi kuwasikia wanatukana kwao. Ma veteran waliokaa viwanja miaka 20 na zaidi ni nadra sana kuwasikia wanasema maneno mbovumbovu.
Ni kulimbuka tu.
Sasa kama mtu ni wa kwanza kijijini kwao kwenda South Africa kwa nini asilimbuke?
Amenikumbusha rafiki yangu mmoja alirudi kutoka masomoni Uingereza miaka ya 90s kati, akawa anasema sasa amekuja kulikita bongo, hatoki tena nje. Na huyo ni mtu mwenye kila access ya kusafiri nje, tulikuwa tukisafiri naye nje tukifika immigrations za watu, anaulizwa "wewe baba yako ndiye fulani Tanzania?".
Sasa kwetu ambao hatujatoka mitini, tuna familia zenye heshima, hata Tanzania ikipigika vipi kwa mambo ya mpito ya uongozi mbovu, kuitukana kwamba ni shithole country ni jambo la huzuni sana.
Na walio na machungu na uongozi wetu kiasi cha kukubali matusi haya ya bei rahisi ya jumla, naelewa kwa nini wanaghafilika hivyo. Na nawaachia nafasi yao ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.
Hata kama sikubaliani na matusi yao.
Mleta mada nimempa nafasi yake kubwa sana kwamba ana haki ya kujisikia hivyo na kujieleza na naelewa kiasi ni kwa nini anajisikia hivyo. Kuna watu wengi sana wanajiona hawana hisa katika nchi yao wenyewe. Mfano, Bongo kuna msoto na ujinga mwingi, ukisoma tabu, usiposoma moto. Na kukataa hilo si haki, lakini kwangu msoto huo si sababu ya kutukana nchi.mkuu asante kwa somo.
kwa upande wangu nakubali maelezo yako pia nakubali maelezo la mleta mada kwa 100% pia.
Hahaha hata wewe umepanic?! Huwa sielewi kitu kuhusu tusi, lina impact gani kwamtu?! Nchi ikitukanwa inaumia au inabadirika chochote au maisha yetu yanabadirika? Mi huwa naona sawa tu atukane asitukane sioni tofauti, hizo ni hisia zake ambazo hazina impact yoyote kwa yeyote. Muacheni atukane ajisikie vizuri, stress mbaya sana.Nina huzuni sana kuona mtu akiandika matusi ya hivi kuhusu nchi yake ya kuzaliwa.
Ama ikiwa yeye anafanya makosa kufikiri hivyo, au ikiwa wengine wamemkosea mpaka kumfanya aseme hivyo, au hata ikiwa ni mchanganyiko wa mawili hayo, bado ni jambo la huzuni sana.
Nimekaa nje ya nchi niliyozaliwa ya Tanzania, hususan Marekani, miaka takriban 20 sasa, na kwa kweli nitakuwa muongo nikisema sijawahi kufikwa na hisia za kuhoji uzalendo wangu kutokana na mwenendo wa uongozi nyumbani, na baadhi ya tabia za kijamii, na pengine kuhoji huko ndio uzalendo wenyewe.
Lakini kamwe sijajisikia kufika kuitukana nchi yangu ya kuzaliwa kwa jinsi hii.
Licha ya hivyo, naelewa baadhi ya sababu za matusi haya na watu kuyachukulia kirahisi.
Hahaha hata wewe umepanic?! Huwa sielewi kitu kuhusu tusi, lina impact gani kwamtu?! Nchi ikitukanwa inaumia au inabadirika chochote au maisha yetu yanabadirika? Mi huwa naona sawa tu atukane asitukane sioni tofauti, hizo ni hisia zake ambazo hazina impact yoyote kwa yeyote. Muacheni atukane ajisikie vizuri, stress mbaya sana.
Huwa naona unatumia logic kwenye mijadala ya kutokuwepo Mungu, hili halina maana kabisa, huyu anajifurahisha tu.
bongo hata uwe Bill Gates itabaki kuwa shithole tuNchi yetu sio shithole hata kidogo, hata kama kuna mapungufu lakini hatuwezi kukubaliana na wewe eti this is shithole hapana aisee, Wapo watu wanapambana humu humu na wametoboa tena inawezekana mara 100 zaidi yako wewe, kushindwa kwako mikikimikiki ya Bongo hakuwezi kutuaminisha nchi yetu ni shithole..
Binadamu kuhama kutoka sehemu moja na nyingine kutafuta maisha ni kawaida tu mkuu, Watu wametoka USA wako hapa wamekuja kupambana, watu wametoka UK wako hapa, wahindi wametoka India wako hapa, Chinese ziko hapa za kumwaga tu, watu wametoka SA wako hapa tunapambana, Sio ajabu pia kwako kutoka na kwenda huko kupambana ni haki yako mkuu.
Mwache aeleze hisia zake katiba inamruhusu!Nina huzuni sana kuona mtu akiandika matusi ya hivi kuhusu nchi yake ya kuzaliwa.
Ama ikiwa yeye anafanya makosa kufikiri hivyo, au ikiwa wengine wamemkosea mpaka kumfanya aseme hivyo, au hata ikiwa ni mchanganyiko wa mawili hayo, bado ni jambo la huzuni sana.
Nimekaa nje ya nchi niliyozaliwa ya Tanzania, hususan Marekani, miaka takriban 20 sasa, na kwa kweli nitakuwa muongo nikisema sijawahi kufikwa na hisia za kuhoji uzalendo wangu kutokana na mwenendo wa uongozi nyumbani, na baadhi ya tabia za kijamii, na pengine kuhoji huko ndio uzalendo wenyewe.
Lakini kamwe sijajisikia kufika kuitukana nchi yangu ya kuzaliwa kwa jinsi hii.
Licha ya hivyo, naelewa baadhi ya sababu za matusi haya na watu kuyachukulia kirahisi.
Mimi ndiye niliyeanzisha kusema aachwe aseme atumie haki zake za kikatiba na kibinadamu.Mwache aeleze hisia zake katiba inamruhusu!
Sawa tumejua na wewe umeishi Marekani takribani miaka 20.
Nimeona mwandiko wako kama unamlaumu kwa namna fulani,any way ujumbe uwafikie wale wanaoona jamaa kakosea kusema hisia na mawazo yake!Mimi ndiye niliyeanzisha kusema aachwe aseme atumie haki zake za kikatiba na kibinadamu.
Halafu wewe tena unakuja kuniambia mimi nimuache aeleze hisia zake katiba inamruhusu?
Mwandiko wangu kuusoma na kuuelewa mara nyingine unataka kukaa kitako.Nimeona mwandiko wako kama unamlaumu kwa namna fulani,any way ujumbe uwafikie wale wanaoona jamaa kakosea kusema hisia na mawazo yake!
Tawire mtanganyika uliyeishi Marekani zaidi ya miaka 20.Mwandiko wangu kuusoma na kuuelewa mara nyingine unataka kukaa kitako.
I dissect paradoxes out of boxes, remove contradictions with my diction.
I am compassion, even as I express with a passion.
Kiranga the singularity, vulgarity with no parity.
Stop defining me by that. That does not even begin to define me.Tawire mtanganyika uliyeishi Marekani zaidi ya miaka 20.
Mkuu,Nchi yetundio unayoiita shithole country kweli?kwahio utafia huko na kuzikwa hukohuko,hustahili kupongezwa aisee
Wewe ni chootu tena chakikeMaana ya kwanza ni kumshukur Mungu kwa kunifikisha hapa nilipo leo na pia ni happy birthday day yng kwa kuzaliwa siku kama ya leo, kuvuka boda siku kama ya leo kwa mara ya kwanza na pia ilikuwa ni siku ya kutengana na Afrika kuingia huku ukubwan ndio maana nikasema siku hii huwa ni muhimu kwng.
Huku kwetu ni makaburi akifa lazima aje azikwe huku.Mkuu,Nchi yetundio unayoiita shithole country kweli?kwahio utafia huko na kuzikwa hukohuko,hustahili kupongezwa aisee
Nimeandika nimefuta zaidi ya mara kumi....ngoja nipite hivi.Kwanza nianze kuwasalim wote mliopo humu na wale ambao hawakubahatika kuingia humu leo, najua siku wakiingia watazipata salamu zao.
Dhumuni la kuandika uzi huu kwanza kbs ni kumshukuru mola muumba kwa kunifikisha hapa nilipo leo maana bila baraka zake pengine mpaka leo ningekuwa bado nipo ndani ya shithole country.
Pengine nishakufa kwa kutekwa na wasiojulikana, au kwa stress zinazosabishwa na ugumu wa maisha wa nchi hiyo.
Naadhimisha siku hii au tareh hii ya leo ambayo ndio ilinitenganisha mimi na Afrika, pia ndio tareh ambayo pia nilivuka boda kwa mara ya kwanza kusogea bonden bila kujua kwamba kule ndio kungetokea neema ya kuwa hapa nilipo leo.
Kwahiyo naweza kusema kuwa kila mwaka tareh 25/06 huwa na kumbuka kumbu nayo kwa mambo haya na mengin mengi ya kimaisha.
Baada ya uzi huu najipongeza pia mwenyew kwa juhudi zang i can tell myself "Happy Birthday to me" kwa kufikisha miaka 7 nje ya Afrika, pia nawatakia siku njema na maisha mema.
Muda wangu wa mapumziko unakwisha ngoja niwahi niingia ndan kushughulika na majukumu ya kimaisha
Tunajua unajua kusema na kuandika kiingereza mzee baba!Stop defining me by that. That does not even begin to define me.