Miaka 5 kazini mshahara haujawahi kutana

Miaka 5 kazini mshahara haujawahi kutana

Jamaa atakuwa na akili zaidi yangi mara 100. Yani mimi 10 million nimeishia kununua kiwanja tu lakini yeye kajenga nyumba na kuhamia kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
M8 ni kujenga tuu. Kiwanja tayar nlkua nacho tayari
 
sasa kama ulianza na 400k ikawa aitoshi,ikapanda mpaka 1,2m aitoshi tu hata ukipata 10m aitotosha.

unadai hujui pesa yako inaenda wapi,unadai huwa unafanya bata mara moja moja na huwa hutumii si zaidi ya 30k.
hapo shida tu ni matumizi ya pesa,maana mshaara wako upo sawa hata ukitaka kujiendeleza ila nidhamu tu ya matumizi ndo imekukosa.

fanya zoezi hili ili ujue hela yako inaenda wapi,nunua notebook ya 1,500tsh hii ni ile dizaini ya kuweka mfukoni,huitaji kununua kalamu maana huwa zinakuja na kalamu yake ndogo na inatosha kwa matumizi.

anza kuandika kila kitu unachotolea pesa mfukoni mwako,pesa yoyote unayoitoa mfukoni kwa matumizi yoyote.
andika kila kitu,hapa usijiambie kuwa:haaa na mia nayo ya pipi niandike!!! rafiki yangu andika kila kitu,hata hile mia tano utakayo mpatia omba omba pale kamanga ferry wewe andika.hela ya sadaka kanisani andika.mpaka hile ya michango ya kijamii yote andika.

nachokuambia ni kuandika kila pesa inayotoka mfukoni mwako.

fanya zoezi hili kwa mwezi mmoja,alafu rejelea matumuzi yako,angalia matumizi yapi yaliyochukua hela yako,kisha ujue kama ni ya lazima au si ya lazima.

hapo utafanya kuwa na bajeti,itakuepusha kutumia hela hovyo kwa kuwa tu unayo,kama ni hela ya pipi utapangilia kabla ya kuitoa
 
Acha upuuzi wako ww
Nyumba ya mwenzio utaitaje utopolo mpuuzi wewe
Na kwa taarifa yako kwa hiyo 80m na bado hujamaliza hapo umepigwa
Nyumba milioni 8, wakati mi nishautumia milioni 80 na nyumba haijaisha. Hiyo nyumba au utopolo
 
Me wife nlkua namrushia ktk account yake 300k kila mwezi... afu nkamwambia afiche atm card asinipe... mwezi wa kwanza nilizivuta hela kwa nmb mobile mdogo mdogo had zikaisha..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapo tatizo ni attitudes towards money i will explain yaani kuna watu hua wanaona kila sent ni ya kutumia hata kifungo cha shati kikitoka anapeleka kwa fundi,sinki la kunawia uso likivuja fundi halaf kila mtoko sio lazima utumie hela having fun haimanishi kutumiatumia tu hela. Kwa hio mzee wangu naona unatatizo la attitude zaidi...vile vile. Attitude inanzaga na self talk (feelings) na hua inaishia na kitendo (action) kwahiyo hizo feelings zinaweza kua NEGATIVE au POSITIVE kama zikiwa negative zichange kua positive mfano uliposema huwezi kukaa bila hela hio ni negative fellings (attitude) means hapo tayari umejiandalia a sababu za kutumbua hizo hela it is better to say im in control of my habit pia kuliko useme mshahara wangu haukutani (kweny self talk ni sawa na unasema i`m worrying about my salary)vitu ambayo ni negative feelings ni bora useme nipo confident na optimistic na mshahara wangu. Jitahidi sana kutengeneza semantical self talk kwa kifupi Attitude is the past reaches into the present and programs the future, by your recollections and your internal rhetoric what you perceived to have happened in your life.
 
Nshajaribu mara 2. Tatizo la wife ninammudu mno. Naenda kuchukua. Maana sipendi kukaa bila hela. Nikiishiwa tuu nataka hela zangu... ananipa
Nenda machame au meru kaoe Mwanamke mwingine ukishamkabidhi pesa kutoka mpaka damu imwagike...jokes Pole mkuu ilo siyo tatizo lako peke yako Ni almost wafanyakazi wote...Ufumbuzi wa Kwanza tayari umeshaupata kitendo Cha kujiuliza hivyo tayari upo karibu kupata Ufumbuzi...all the best mkuu.
 
Mkuu hupaswi kuachana na forex,kitu kinacchokusumbua ni ujuzi kama una nia nambie nikuelekeze cha kufanya....
Nshajarbu mwaka jana.. nlianza na bonus account nkachoma. Maana forex niliona siielewi. Ofcoz najua sababu cjapataga mkufunzi akae anieleze. Nmeijulia tuu humu jf, na youtube kiasi nkafungua fx broker akanipa bonus usd 100 nkaichoma.. nkaachana na forex.
 
nilikuwa kama wewe mkuu..nilichofanya nikabadili mtindo wangu wa maisha, marafiki wasiokuwa na maana nikawapotezea, mshahara ukitoka natoa laki 5 tu..laki 3.5 nampa wife kwa ajili ya matumizi ya home,me nabaki na 150k tu mfukoni..the rest naiacha bank..ATM nampa wife akae nayo..saiv nimepiga hatua sana, walau naweza kusema na mie nasave..
 
Shetani na mawakala wake wanakamata uchumi wa watu, jaribu kutafakari namna Mungu anavyoweza kukusaidia kukulinda kwenye maeneo mbalimbali ya maisha, ikiwemo na eneo la uchumi. Ukisoma kitabu cha Ayubu utagundua mafanikio yake yalikuwa yanalindwa na miale ya moto, yaani roho wa Mungu...ule ulinzi ulipoondolewa ndo ibilisi akapata upenyo wa kumshambulia na kila aina ya mabalaa na mikosi...
Mawazo ya kilokole wakati walokole wenyewe ni makapuku wa kutupa.china hawamjui huyo ayubu wako wala nani na ndio nchi ya pili kwa uchumi duniani
 
Mawazo ya kilokole wakati walokole wenyewe ni makapuku wa kutupa.china hawamjui huyo ayubu wako wala nani na ndio nchi ya pili kwa uchumi duniani
Kama wewe na wachina hamumjui Ayubu ni matatizo yenu, huo uchumi mkubwa haujawakinga na kifo cha magonjwa kama korona, na wewe mlolongo ni ule ule, kufa kifo cha mtu anayekufa.....lakini nafasi ya kutubu huwa inakuwepo hadi siku ya kukaribia kukata roho.....Mungu ana rehema sana...
 
Nshajaribu mara 2. Tatizo la wife ninammudu mno. Naenda kuchukua. Maana sipendi kukaa bila hela. Nikiishiwa tuu nataka hela zangu... ananipa
Hii tabia ya bro wangu. Anaweza akakupa laki 2 umtunzie kwa kuwa hana nidhamu ya hela. Siku akiunga behewa bar na washkaji atakurudia hata mara 3!
Dogo hebu nipe 50k hapo. Anaenda zungusha, zikiisha tena anakurudia upya!
 
Ďah kuna staff mwenzetu mme wake ni mtu wa gambe sana .sasa akipata mkwanja kabla hajaenda kulewa anampatia mkewe amuhifadhie pesa.Ila akishatupia mbili tatu anarud maskani akiwa mbogo anataka apewe mkwanja wake yaan anatishia hadi kichapo kwa mkewe.

Mzunguko unaenda ni hvo kila hela inaishia kwenye tungi yaani.
Huyo ni bro wangu kabisa tabia yake hii. Gari ya gambe ikiwaka tu atarufia hela kwa mafungu hadi ziishe!
 
You are FINANCIALLY SLAVE.....fanya mpango uhakikishe unakua na FINANCIAL FREEDOM.
 
Clinker belite,

Angalia matumizi yako kwa mwezi wapi hela kubwa zinatumika.Ukianzia hapo utajua pesa inakopotolea na kuziba hiyo loop hole.

Pesa huwa inatabia moja yaani 'get more consume more' then unajikuta pesa inaisha fasta sana.
Cycle inajirudia hivyo hivyo na usipobadilika unakuta kwa mwaka umepitisha hata m20 lakin hujafanya cha maana
Hii pia inantokeaga sana. Nikiwa na hela nyingi mfukoni huwa siogopi kuitumia ila ile paap imebaki laki ndio naanza kuitumia kibahili. Af hapo ndio matatizo yanakujaga kwa kasi!
 
Kijana wangu Eyce akipita hapa kwa thread hii atanitukana kimoyomoyo
 
Back
Top Bottom