Miaka 5 kazini mshahara haujawahi kutana

Miaka 5 kazini mshahara haujawahi kutana

Ukipata ela nunua assets mm naamini katika msemo wa hela haikai, kila mtu anamapungufu yake ikifikia ishu ya Ela, unaweza ukawa hunywi pombe lakini unapenda vitu vingine.
 
Ukweli mchungu. Ukiwa na pesa zinakuwa kama zinakuwasha hivi. Zinakutaka uzitumie tu. Usipokuwa na nidhamu ya matumizi utachanganyikiwa.
Mi naona njia nzuri ni kuweka limit ya matumizi kwa mwezi. Binafsi hio hela naona ni nyingi mno kwa mtu ambaye hana familia kubwa.
Mf. Budget ya chakula:
Sukari
Mchele
Unga
Mafuta
Tambi
Chumvi
Nyama
Samaki
Kuku

Miscellaneous:
Dawa za mswaki
Pampers
Vifurushi vya Tv na simu
Luku
Bill ya maji
Toilet papers
Napkins
Wipes
Nauli
Petrol/Diesel (kama ana gari)
Gas ya kupikia
Vehicle maintance (kama ana gari)
Gambe weekends

Aanze na kuangalia hivyo vyote na kulimit matumizi na ili ku save anunue jumla kwa suppliers. Kununua hayo mahitaji kwa rejareja inaumiza sana ila hatujui tu.

Kwa mfano mwezi kwa average family hata vikabaki sio kesi.
Sukari 5kgz, kwa jumla 15k

Unga Fika mashineni nunua mahindi kwa sado au debe saga mwenyewe. Haitazidi 12k ila utapata unga wa kutosha!

Mchele fanya kama unga tu, fika mashineni nunua. 25kg itakuwa kati ya 50k-55k

Chumvi nunua carton kabisa ile yenye vifuko vingi utasahau. Haitazidi 15k

Mafuta dumu la litre 5 almost ni 20-22k kulingana na ulipo.

Tambi, sio lazima ila kama utapenda nunua hata nusu dozen kwa bei yake jumla sidhani kama zitazidi 10k

Nyama, nenda machinjioni kule weekend moja damka ukanunue kilo za jumla kule. Kwa 10kg cost hazitazidi 70k .

Samaki, hawa sina uzoefu nao sana maana naonunua wanatoka nyumba ya Mungu, huku niliko nikiwa na 30k nawajaza frijini 🤣🤣🤣🤣🤣 nakula mpaka nachoka. Naweza nikawala mwezi mzima size tofauti tofauti bila kubadili mboga. Ila wale sato, sangara, kibua naona wapo expensive. Kukadiria labda anunue wa 30k tu kwa aina anayopenda.

Kuku, jumla ni buku 5500 kwa order kubwa ila roughly kwa 6k hawezi kuku wake hata 7 wanatosha kwa mwezi. Hii ni optional akitaka punguza anaweza pia ila 7 ni around 42k inatosha.

Hizi ni estimates tu ila anaweza limit budget akapunguza mpaka around 200k kwa matumizi ya kula kwa mwezi akawa anaongezea vinavyopungua tu akifika mwishoni.

Miscellaneous:
Nako akilimit kwa 250k inatosha na hii itafika kama akiwa na gari! Bila gari anaweza save 100k au zaidi.

NB: Gari aweke full tank inasadia zaidi kuliko mafuta ya kujaza kwa kibaba. Yanakula hela nyingi zaidi.

Akiweza tumia mfumo huu kadri siku zinavyoenda gharama itakuwa inapungua na ataweza ku save mpaka laki 5 kwa mwezi.

Mke ampe laki na nusu tu. Hela zote hizo za nini? Hana kazi
 
Hii pia inantokeaga sana. Nikiwa na hela nyingi mfukoni huwa siogopi kuitumia ila ile paap imebaki laki ndio naanza kuitumia kibahili. Af hapo ndio matatizo yanakujaga kwa kasi!
Yaani mtego wa pèsa ndio uko hapo.ikishakuwa nyingi inaleta utumiaji mkubwa.Ukiweza kutumia kwenye normal range wakati kipato ni kikubwa basi ndio hapo siri ya kufanikiwa kuwa na mamlaka juu ya pesa yako inaanzia.Otherwise unakuta pesa ndio inatu drive
 
Yaani mtego wa pèsa ndio uko hapo.ikishakuwa nyingi inaleta utumiaji mkubwa.Ukiweza kutumia kwenye normal range wakati kipato ni kikubwa basi ndio hapo siri ya kufanikiwa kuwa na mamlaka juu ya pesa yako inaanzia.Otherwise unakuta pesa ndio inatu drive
Yani mkuu najikutaga najiachia sana. Unamaliza 50k hamna kitu cha msingi labda nimenunua earphones tu 20k nimekula 15k. Dogo kanililia njaa nimempa 10k yani dah! Unajikuta ghafla una 5k mara nimejiunga kifurushi cha simu kuongezea MB tu wakati bado ninazo. Hapo siku imeisha umeua 50k kisoro tu!

Kimsingi hela inawashaga sana, matumizi yanajitokezaga tu hela ikiwa nyingi mkononi. Shughuli ni pale reserve imebakiwa na laki tu!🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wakuu, hii ni nini?

Nilipomaliza chuo, 2014 nikapata shule fulani ya kujishikiza huku nikisubiri ajira ya fani yangu. Mshahara ulikua 400k kwa mwezi. Nilikuwa naishi fresh, natuma kwa maza home, namlipia dogo tution mapambako akija likizo na pesa ikawa inakutana na mshahara ujao. Nilifundisha kwa mwaka mmoja na sijawahi ishiwa.

Mwaka 2015 nikapata ajira yangu sasa. Mshahara take home ikawa ni around 900k. Lakini pesa haijawahi kutana. Sinywi pombe, naendaga club na matamasha ya muziki mara moja moja lkn sijawahi tumia zaidi ya 30. Na kwa mwezi labda ktk bata naenza enda mara 2 au 3.

Mwaka 2018 nikapata kazi ingine, take home ikawa zaid ya 1.2m. Nilkuwa nishaoa. Wife nikawa nampa 300k matumizi, inabaki 900k. Wazazi na nini labda inabaki 700k. Lkn haijawahi wekeka bank ikutane na mshahara ujao na sioni nimefanyia nini.

Nikaona siwezi weka pesa nikaamua kuchukua mkopo 8m nikajenga nyumba nimehamia home. Makato 410k. So nikikatwa mkopo nabaki na hela lakini same story, hazikutani a mshahara ujao.

Kuna mtu anapitia situation kama hii isiyo na majibu? Tukutane hapa.

Uzi tayari
Duh nyumba ya 8m ni ya udongo , nyasi au mabati matupu?
 
Ndo nmefanya hivo hivo...
Watu wanafanya maisha kuwa magumu bure! Sasa hapo mkuu si utaanza kujipanga taratibu kujenga ile ya mbele hata ikichukua 10 years! Kikubwa sasa hivi hudaiwi na baba mwenye nyumba, asubuhi na mapema kanakuja kamejifunga taulo kukudai utafikri wewe ni kijana wake!!
 
mimi tatizo langu nikisha weka ela ya matumizi kwa mwezi
hiyo pesa nahakikisha inaisha kweli ndani ya huo mwezi hata kwa lazima hahahahaaaa aiseee mashetani kweli yapo
 
A
Umemalizaa Mkuu...!!


Japo ni risk lakini kama una mwanamke anaejielewaa mpe akushikiee baki na kiasi kidogo cha matumizi na mkeo awe mbinde sanaa yani kila ukitaka hela sio anakupa tuu bora akupe ya kutumia siku hiyo tu maana umeshindwa kujiendeshaa mkuu japo haya mambo acha tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Pesa ya mshaara ina mapepo sijui
Ahahah
 
Back
Top Bottom