Miaka 28 sina nyumba wala gari, roho inaniuma

Miaka 28 sina nyumba wala gari, roho inaniuma

Nahuzunika kwa hili
Unapoangalia sana watu wa chini yako (masikini zaidi yako) hua ni rahisi sana kunyanyua mikono na kumshukuru Mungu kwa neema na baraka alizokupatia.
Unapokua ni mtu wa kuangalia sana watu wa juu yako (matajiri) basi ni rahisi kwa shetani kukuchezea akili mpaka utafikia kukufuru maana hautaona jema lolote ambalo Mungu amekutendea.
Kuna kipindi na mimi nilikua nnapitia hali kama unayoipitia wewe, kuna jamaa yetu alikua anaumwa kansa amelazwa Ocean road, baada ya kwenda kumtembelea na kuona hali za wagonjwa wengine waliokua wamelazwa hapo hospitali, hakika nilijiona mimi ni miongoni mwa watu waliobarikiwa kuliko watu wengi hapa ulimwenguni.
Sisemi haya kwa kukukatisha tamaa ya kupambana ili utimize malengo yako, bali nataka uone neema na baraka kubwa ya uzima na afya uliyopewa na Mola wako.
Kuna watu wanateseka jamani na maradhi hapa duniani.
 
Focus on what you have.

Uhai, afya njema...family, friends.

Hata ukidinda fresh Ni Jambo la kushkuru pia.

Mengine tia bidii, focus on your realistic goals Mungu atayaleta tu.
Kwa presha hii ya kuangalia maisha ya majirani hiyo 'kudinda' atasikilizia kwa mabaharia tu.
 
Kosa kubwa sana kwenye maisha kushindana au kujilinganisha na yyte, run your own race...kila mtu hubarikiwa kwa wakati..nilipata pesa za kutosha at your age, hamna la maana nlifanya, lakin nlipofoka 39 na kupata ndio nimepiga hatua. Subiri muda wako, na usishindane na mtu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa kubwa sana kwenye maisha kushindana au kujilinganisha na yyte, run your own race...kila mtu hubarikiwa kwa wakati..nilipata pesa za kutosha at your age, hamna la maana nlifanya, lakin nlipofoka 39 na kupata ndio nimepiga hatua. Subiri muda wako, na usishindane na mtu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
K,ila wivu wakimaendeleo unafaa mkuu
 
badala usikitike huna akili unasikitika ujinga huo.

kuna watu wameuza gari/nyumba ili tu wapate afya njema (kama yako)
Kila mtu na huzuni yake mzee, akili zipi sina?
 
Usipopata ushauri unaonekana unaweza kujinyonga baadae kwakuwa unatamani kupata na sio kusubiri au kukosa, tambua unaweza pambana miaka mingi kutafuta mwaka mmoja wa furaha. Ktk maisha ya kupata na kukosa wewe bado kinda kbs kwa umri huo, kikubwa subira na usianze kujilaumu kwa kuwasaidia ndugu zako maana huijui kesho yako, Mungu ana mipango juu yako na ndugu zako huwezi kuijua.
 
Back
Top Bottom