Miaka 28 sina nyumba wala gari, roho inaniuma

Miaka 28 sina nyumba wala gari, roho inaniuma

weka mipango uanze kutafuta kimoja kimoja weka nia na mipango dhabiti usitake kupata vyote kwa wakati mmoja utaishia kukosa vyote kabsa. mtaka yote kwa pupa.... umri ni namba tu usikutishe mkuu..
Okay
 
Watu wana 40yrs na bado hawana lamani yeyote ile, Sembuse wewe mtumishi wa serikali unakopesheka na bado umri wako ni mdogo sana
Tatizo dini yangu imekataza riba, napenda kweli pesa nyingi ili nifanyie jambo fulani
 
Unajishughulisha na kitu gani?

Kipato chako kwa mwezi kinafikia kiasi gani?

Matumizi yako yakoje? Unahisi kwamba unatumia vibaya ndio maana umeshindwa kumiliki hivyo vitu au ni kwamba kipato chako ndio hakikuruhusu kumiliki hivyo vitu?
Niko idara ya elimu, salarry ni below 1m, bajeti ni zaidi ya 350k kwa mwezi
 
Mke ninaye, naishi kota
Unganisheni nguvu mpambane yote unayotamani mtayapata mkiwa wamoja. Vile vile jengeni urafiki na familia zenye mafanikio zaidi yenu ili muige maendeleo yao badala ya kuchangamana na mlio sawa au mliowazidi kiuchumi kwani mtakuwa mnajazana ujinga tuu mara mwenye ghorofa lile ni FREEMASON mara mwenye ile gari kaiba nk
 
Shukuru Mungu kwa hiki ulichonacho, tena una kazi serikalini, angalau una jua mwisho wa mwezi una kitu unaingiza. Bado una nafasi ya kusimama tena nakuanza upya, ukafanikiwa. Jipange upya na ongeza nguvu ya mafanikio. Mana kuna wenzio wana miaka 30 mpk ss hawana ajira na wala hawaingizi kitu mwisho wa mwezi. Shukuru Mungu una uwezo wa kuanza tena mkuu. Mungu atakupigania.
The Most Winner
 
Unajishughulisha na kitu gani?

Kipato chako kwa mwezi kinafikia kiasi gani?

Matumizi yako yakoje? Unahisi kwamba unatumia vibaya ndio maana umeshindwa kumiliki hivyo vitu au ni kwamba kipato chako ndio hakikuruhusu kumiliki hivyo vitu?
Nahisi matumizi yangu ni mabaya sana, afu wapo wadogo zangu wananitegemea, kwahiyo unajikuta salarry inaishia hewani tu.
 
Mkuu. Mi nagonga 70 Julai na sina kitu wewe 28 ndiyo unapaniki. Tulia maisha ndo yanaanza !!!

Pia epuka sana dhambi ya kujilinganisha na wengine kwa sababu hata ufanyeje kuna watu ambao watakuzidi tu. Keep your pace, muombe Mungu na makinikia sana malengo yako uliyojiwekea huku ukirekebisha mapato na matumizi yako na kuchakarika huku na huko.

Na pia kumbuka kwamba kati ya wenzio hao unaowarejelea naamini kuna wengine tayari wameshatangulia mbele ya haki. Ile kuwa hai bado ni mibaraka tosha
Ujue kufanya comparison inakusaidia na wewe kufight zaidi, wote wako hai
 
Niko idara ya elimu, salarry ni below 1m, bajeti ni zaidi ya 350k kwa mwezi
Kama uko elimu na una shahada Ina maana salary yako ni kuanzia 700k+ unaweza fanya makubwa boss hofu yako tu ishinde.

Usiishi kwa hofu kwa kuangalia maisha ya watu hata Mimi hiyo hali ilinipelekesha sana.

Hiyo "fear oc failure" uliyo nayo ni mbaya na itakuangamiza zaidi kuliko maisha unayoishi
 
Usiwe na wasi. Nina miaka 50 lakini sina chochote. Umeona watu wengi tu wakizikwa mwaka huu. Je, yupo alizikwa na pesa na nyumba? Haya mambo ya duniani ni ubatili tu (vanity).
Mungu katuambia tutafute sana kama tutaishi milele, na tufanye ibada zaidi kama tunakufa kesho
 
Hapo ukitaka kujichimbia kaburi, OA sasa na uwe na familia yani unajizika mzima mzima huo, ila JF pia isikuogopesha humu kuna Ma bazazi kibao kwenye nyuzi wakijitamba tamba ili kunasa mbebezi
Nina mke na mtoto 1
 
Nahisi matumizi yangu ni mabaya sana, afu wapo wadogo zangu wananitegemea, kwahiyo unajikuta salarry inaishia hewani tu.

Cha kwanza na cha msingi wema usizidi uwezo.

Jaribu kubana matumizi kwa kufanya yale matumizi ya msingi, Halafu kwa kipato hicho inahitaji kujidunduliza kwa muda ili uweze kufikia hayo malengo. Cha kufanya anza kuweka akiba kidogo kidogo na ukifika kiwango fulani unaweza kuongezea kwa kuchukua mkopo na kufanya hayo malengo. Naamini unakopesheka kwa kuwa ni mtumishi.

Pia unaweza kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo kulingana na mazingira uliyopo na uhitaji wa mzunguko wa biashara husika. Kipato hicho cha ziada kitakusaidia kwa hayo majukumu ya kuwasaidia ndugu zako.
 
Wala tu usijali haujachelewa tena upo pazuri endelea kupambana na kuongeza juhudi. Kuna wenzako umri huo hata uhakika wa kipato hawana. Be grateful of what you have na jitume zaidi
Thanks
 
Umri bado shukuru una ajira mwenzio iyo ajira naitafuta kwa tochi na namba zishasoma zaid ya iyo 28 nkikaa na kufikilia kuwa nmepoteza najiona bado nafasi zipo na nkimuangalia mtoto wangu anafurah anaenda choon najiona nami ni miongon mwa waliofanikiwa japo kwa nyanja tofauti ila nn maisha bila changamoto kama izo ni kama supu bila ndimu na pilipili ainogi
 
Pole! Yaani huo muda wa kuwaza umiliki wa nyumba ilihali huna hata kiwanja. Huo ujasiri wa kuwaza nyumba unautoa wapi mpendwa
 
Back
Top Bottom