Miaka 28 sina nyumba wala gari, roho inaniuma

Miaka 28 sina nyumba wala gari, roho inaniuma

dimaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
4,305
Reaction score
5,837
Husika na kichwa cha habari tajwa.

Mimi ni kijana, mwenye umri wa miaka 28 , roho inaniuma kuona similiki nyumba wala gari, kila nikiingia JF nahuzunika kuona majamaa yalivotusua in life.

Mara nina nyumba 3, huyu 5, mara nina gari 4, huku mimi nikijiona mnyonge kweli kweli.

Nimwajiriwa wa serikali, kilichonigharimu nimewahi kupokea ndugu sana kabla sijajipanga vizuri. Kila nilkijiitahidi kumeki lakini wapi.

Nipeni maujanja ili nami nitusue kimaisha. Mamake wenzangu tuloanza nao katika ukuaji ama kuajiriwa, wako mbali mno kimaisha.
 
Mkuu. Mi nagonga 70 Julai na sina kitu wewe 28 ndiyo unapaniki. Tulia maisha ndo yanaanza !!!

Pia epuka sana dhambi ya kujilinganisha na wengine kwa sababu hata ufanyeje kuna watu ambao watakuzidi tu. Keep your pace, muombe Mungu na makinikia sana malengo yako uliyojiwekea huku ukirekebisha mapato na matumizi yako na kuchakarika huku na huko.

Na pia kumbuka kwamba kati ya wenzio hao unaowarejelea naamini kuna wengine tayari wameshatangulia mbele ya haki. Ile kuwa hai bado ni mibaraka tosha
 
Unajishughulisha na kitu gani?

Kipato chako kwa mwezi kinafikia kiasi gani?

Matumizi yako yakoje? Unahisi kwamba unatumia vibaya ndio maana umeshindwa kumiliki hivyo vitu au ni kwamba kipato chako ndio hakikuruhusu kumiliki hivyo vitu?
 
Mkuu. Mi nagonga 70 Julai na sina kitu wewe 28 ndiyo unapaniki. Tulia maisha ndo yanaanza !!!

Pia epuka sana dhambi ya kujilinganisha na wengine kwa sababu hata ufanyeje kuna watu ambao watakuzidi tu. Keep your pace, muombe Mungu na makinikia sana malengo yako uliyojiwekea huku ukirekebisha mapato na matumizi yako na kuchakarika huku na huko.

Na pia kumbuka kwamba kati ya wenzio hao unaowarejelea naamini kuna wengine tayari wameshatangulia mbele ya haki. Ile kuwa hai bado ni mibaraka tosha

Anko shikamoo[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom