Miaka 27 huna mtoto? Jichunguze

Miaka 27 huna mtoto? Jichunguze

Ndio maana mnazaa watoto wanaishia kuzagaa mitaani na mkiwapeleka shule basi zile za kidumu mkononi,1st born wangu nilikua na 30 years nilikua na uhakika wa kumlea katika njia sahihi ingawa wadogo zangu walinitangulia ila niliweka malengo mtoto aje anikute nimefanya ABC's sio nisake mtoto kisa umri.
Pata mtoto ukiwa na miaka 18 na mimi 30 ila muhimu wapate malezi bora sioni sababu ya kukimbizana kama wataishia mtaani tu,kwa wale ambao wanahisi wamechelewa fanyeni vitu kwa mipango siku hizi hakuna zile za mtoto kulelewa na babu na bibi au ba'mdogo lazima tujipange hakuna haja ya kuwasikiliza haw wanaowaaminisha eti lazima mtoto aje ukiwa umri fulani.
Vipi km Maisha yakakushinda... hutozaa. Maana si Wote wanaosema wanajipanga wanafanikiwa...
 
Waoga wa Maisha siku zote wanaogopa Watoto, wanakuambia wanajipanga.

Cha ajabu Umri unazidi kwenda, na bado hali yao kimaisha si Simba wala Yanga.

Sasa sijui wanajipanga nini!

Watoto wana raha yake, msiwe waoga.

Kama wewe unakula Tembele, na Mtoto atakula Tembele, hivyohivyo mpaka Mtoto anakua.

Jiulize, wewe unaeogopa Mtoto.

Wewe ulikuzwaje?

Lini Wazazi wako/wenu walilala nje eti kwasababu ya wewe Mtoto, nyie Watoto!
Mi sijaona Tatizo la Mleta mada ingawa watu wanamshambulia sanaa... Kuna watu wakifikisha 25 wameshafanikiwa kuliko anayesema 30 ...

Sisi wengine mbn tumesoma shule za Kupeleka mbolea na majembe ... Ila Wazazi baadae ndo maisha yamekuwa mazuri tunasoma Vyuo vya Private.. na Mdogo wangu ambaye nimemzidi miaka 10 ndo Anafaidi Kuliko hata Sie Wawili ...

Ila Kuna Msemo Mmoja Alishaniambia Mtoto wa Ba Mkubwa.. Ukiwa na Familia Baraka Mungu Ndo Anazinwaga... Ingawa Si wote Tutaweza Pata Watoto ila Kwa Uweza Wake Mungu
 
Una uhakika wa kufika hiyo miaka 40
Hata Mi Nashangaa Mtu ana Uwezo Wote Hapo anasema Anataka kuendesha Gari aina Zote Halafu Anakuambia Mwishoni Ada Ni Million sasa Kama Anauwezo wa kuendesha Gari la Mil 20 anashindwaj kusomesha... Tena Elimu siku Hizi Bure.. Mtoto unampeleka Shule Ila Unamtafutia na Tution za kutosha

Huyo anataka miaka 40 ndo awe na Mtoto

Mtoto mpk Aanze Shule Yeye Ana Miaka -47
Mtoto Akimaliza La Saba Yeye ana Miaka 54
Mtoto Akimaliza Secondary yeye ana 58
Mtoto akimaliza A level yeye ana 60
Akifika chuo Kwa Kozi za Miaka 3-5 yeye ana 63-65

Life Span ya watanzania Haifiki Huko...

Hapo Mtoto Hajarudia Shule wala Kufeli Au Kuresiti
 
Kutokana na hii post yako nimegundua yafuatayo:
(1) Wewe utakuwa bado mtoto (ndio kwanza umebalehe/umevunja ungo) au;
(2) Huna uzoefu na kitu kiitwacho MAISHA au;
(3) Umekariri maana ya maisha na hivyo huelewi maana yake halisi!
NB:
Jitahidi usome au kuchunguza maisha ya watu walio karne 2 mbele yetu, utagundua kuwa kuoa/kuolewa, kuzaa ni almost NEGLIGIBLE, ndio maana kwa sasa hasa nchi za kimagharibi zina program za ku-import wafanyakazi toka oversees, eg Green Card (USA). Watu wanaojua maana ya maisha wana tabia ya kutanguliza furaha binafsi mbele na sio cjui mtoto, mume/mke, ndugu, nk!
Aiseee nimekupenda, u r the great thinker, i real like that. Blessed
 
Umeamua kunisema mi nina kazi lakini nina kipato cha kati but mke wa kuoa nimekosa nitazaa na Nani?
 
Mbona mi Nina miaka36 mwanangu ana mwaka Na miezi saba
 
Jamani nahisi ndiyo maana sisi huwaga maskini sana,wazungu wenzetu utakuta Mzee Ila mtoto wake wdoogo
 
Kama unachosema ni sahihi basi wengi tupo pabaya kwa kweli.

Nchi za wenzetu walioendelea hua wanasema "Bila tafiti hakuna ruhusa ya kuzungumza"

Sina shaka kama hujafanya tafiti ya ulichozungumza. Shaka yangu ni moja tuu, Je, umefanya tafiti ya hicho ulichosema ????
Na je wale waliopata watoto wao wakiwa na zaidi ya miaka 27 inakuaje ??
Mh.Reginald Mengi amepata watoto mapacha akiwa na 50 yrs plus,
Ndugu zetu wa mitaani waliochelewa kupata watoto baada ya ndoa nao vipi ??
Waliooana mapema ktk ujana wao angali na miaka 24-25 tu lakini hawakupata watoto ndani ya ndoa kwa zaidi ya miaka mitatu mpaka mitano Je ??
Wasomi wengi huchelewa kuoa, wengi wao huoa na umri wa miaka 30, lakini hakuna tafiti inayooanisha mojakwamoja kati ya wasomi na ukosefu wa watoto. Je ??

Tunahitaji tafiti madhubuti kabla ya kuamini falsafa yako hii, vinginevyo tunaomba mtizamo wa kitaalamu wa wataalam wa Afya ktk hili.
Ukumbuke Pia,Mzee Huyo alipata watoto wawili wakubwa kabisa na mkewe was ndoa.Mmoja marehemu.binti ana umri zaidi ya miaka 30
 
Mkuu suala la mtoto halihitaji kujipanga,we una ubinafsi unahisi ukiwa na mtt atapunguza pesa zako,si ajabu huna chochote
Nyie mnaozaa bila ya kujipanga mnafanya watoto wa mitaani kuzidi na omba omba wengi sana sana kwa ndugu, na ndio maana watoto wanakua mashoga baadae koz hamuwez kuwahudumia
 
Back
Top Bottom