Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

brother Nyani Ngabu ungetutoa pia nafasi ya pongezi waliowengi ambao walipata nafasi ya kuifahamu jf kabla kushawishi members wapya hadi wakajiunga na hatimae familia ikawa kubwa kama ilivyo sasa.... binafsi nilipata ushawishi kwa rafiki zangu Wawili Gurta na daffy mwanzoni mwa 2011 na ilipofika July 11 nikajitumbukiza rasmi....
tuamini kuwa jf haitakufa kwani naamini kuna wanamember humu bila jf Siku haiendi....
 
kumbe ni wengi tumepata life partners humu. hongera sana.
 
Linalonisikitisha ni kwamba kwa mambo yanavyokwenda sidhani kama kuna cha kusherehekea kwani JF ni wazi imepoteza hadhi, msimano na mwelekeo. Nilianza kusoma Jambo Forums tangu kuanzishwa kwake ila ilinichukua karibu miaka miwili kujiridhisha kwamba ni chombo huru na makini kabla sijajiunga nacho mwezi Mei, 2008.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 mabadiliko yalianza kujitokeza ndani ya Jamii Forums kiasi kwamba wengine tuliwaomba viongozi wa JF wajaribu kurudisha hadhi ya jamvi hili. Lakini maombi yetu hayakushughulikiwa na jamvi letu pendwa likageuka kutoka forum na kuwa uwanja wa vijembe, mipasho na upuuzi mwingi tu wa kisiasa.

Taratibu wengine tunaanza hata kusita kuchangia JF na nina hakika siko peke yangu...what happened to our beloved forum?
 
Tuhengehenge historia, tuache kusambamai kwenye siasa ya sasa yenye usaliti mwingi, Siasa ni mchezo mchafu!! We unaumia wao wala!!
 
Hata mimi nilikuwa dar hotwire n akina mzee mwanakijiji,zeze,supergal,jeansal,papa k,mume wangu n.k kulivyosuasua tukasikia hii kitu tukahamia kiukweli kijiwe kilikuwa murua sana. Dar hotwire kama ilikufa kizembe ilikuwa na majukwaa mazuri sana sijui ilikuwaje.
 

Ulikuwa unatumia jina gani kule?
 
Pamoja na haya yote,hivi masai dada yupo wapi?mwenye taarifa please
 
Hii siwezi isahau imenipa mume mwaka wa 12 now ,tulianzia kutaniana DHB mpk kuonana na mpk kuoana ahahahaaaaa
 
japo so mchangiaji kivile lakini hakika Nina Maradhi ya jf ukitafuta watu walio wahi kukesha humu nimo mpaka nikadhani nawehuka hongereni wanajamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…