Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Niseme tuu miaka michache niliyodumu hapa imekuwa ya furaha sana
Nilivutiwa kujiunga hapa na Mzee Mwanakijiji kwa hoja zake kuntu (kabla hajakengeuka)
Pia nampa heko Le Mutue kwa kudumu miaka yote licha ya mashabulizi makali anayo yapata

le mutuz alikuwa wembe mkali bwana ...nadhani pia alikua na alias name
 
Mimi nilikuwa sina bahati nayo jamii forum nilikuwa nikiifatilia muda mrefu ila kila nikijiregister nasahau password, nikireset mara password inagoma nikaachana nayo, nikawa na peruzi tu kama mgeni, baadae nikaamu sasa wacha niifatilie niwe na password niweze kuchangia mawazo, ila mie darhotwire ndo nilikoanzia 2003 na baadae ndo nikhamia hapa nadhani itakuwa nina miaka 6 ya kujiunga japo muda mwingi niliperuzi kama mgeni.
 
...Jokakuu, Karibu sana!

...Nikiri kuwa, wewe ni moja ya watu ambao hunifanya nirudi humu kuchangia mada. Uko sober most of the time.

...Nikiona id yako lazima nisimame nisome bango lako. Michango yako ni ya muhimu sana humu.

...Lazima darasa ziendelee kutolewa humu. Vijana wanahitaji kujenga hoja si matusi. Vichwa ndio vitajenga nchi, si misuli pekee.

Assalamu alaikum.
Ahsante kwa hekima zako, tunawahitaji katika ulezi wa kizazi hiki

Kuhusu JokaKuu umenigusa kidogo. Huyu ndugu yangu anakumbu kumbu za muda mrefu na ni mwepesi sana wa kuunganisha kumbu kumbu hizo na wakati uliopo, ni kati ya wakubwa tunaowatumaini sana katika ujenzi wa kutumia vichwa na ulezi wa kizazi hiki kilichosahau debate
 
Mkuu Nyani Ngabu, Mimi nipo japo siku hizi napita hapa Mara chache sana.
Uchaguzi wa 2005 ndio ulichochea sana kuanzishwa kwa JF maana ile mijadala ya kule business times ilikuwa moto na iliwasaidia wengi.

Mzee ES ni katika watu waliochangia kukua kwa JF kwasababu alikuwa na inside information kuhusu viongozi wetu. Akiwa mtoto wa waziri mkuu mmojawapo alikuwa amekulia kwenye gossips za vigogo na hivyo ku share hizo info kulichangamsha jamvi.

Nawatakia wote ushiriki mzuri JF.
 
Asante mleta uzi kwa flash back uliyotupa, ila napendekeza upigwe ban for name calling, umemuexpose Le Mutuz kwa ID aliyokuwa anaitumia kumtukana matusi ya nguoni Kikwete. :)

Pili nitambuwe mchango wa Mwanakijiji kwa uhai wa JF lakini cha kushangaza ndio amegeuka kuwa kituko cha karne na hastahili tena heshima tuliyompa hapo kabla, huyu kwa sasa ni miongoni mwa watu mazezeta kuwahi kutokea Tanzania, ni bor hta Mkandara aliyeamuwa kukaa kimya atleast mjinga akinyama huficha mengi.

Tatu heshima kwako na kwa mkuu Kiranga hizi ni dikshenari zetu hapa JF, heshima pia kwa dada yetu AshaDii she is great woman, pia bila kumsahau mzee wa Bonafie genuine Pasco huyu ni mdau muhimu sana hapa jukwaani.
 
Mpui Lyazumbi sidhani kama tulikuwa msumbufu, tulikuwa tunatofautiana tu kimtizamo na kutetea kile tulochokuwa tukikiamini. Siku hizi nimekuwa msomaji zaidi. Na haiwezi kupita siku bila kupitia hapa. Kwa kifupi jamiiforums inasaidia mengi. Inaleta mawazo ya watu pamoja. HHongera JF
Mkuu, kumbe UPO!?
 
Asante mleta uzi kwa flash back uliyotupa, ila napendekeza upigwe ban for name calling, umemuexpose Le Mutuz kwa ID aliyokuwa anaitumia kumtukana matusi ya nguoni Kikwete. :)

Pili nitambuwe mchango wa Mwanakijiji kwa uhai wa JF lakini cha kushangaza ndio amegeuka kuwa kituko cha karne na hastahili tena heshima tuliyompa hapo kabla, huyu kwa sasa ni miongoni mwa watu mazezeta kuwahi kutokea Tanzania, ni bor hta Mkandara aliyeamuwa kukaa kimya atleast mjinga akinyama huficha mengi.

Tatu heshima kwako na kwa mkuu Kiranga hizi ni dikshenari zetu hapa JF, heshima pia kwa dada yetu AshaDii she is great woman, pia bila kumsahau mzee wa Bonafie genuine Pasco huyu ni mdau muhimu sana hapa jukwaani.
Haha hah hah KIRANGA mzee wa thibitisha kama MUNGU yupo heshima kwake sana.
 
Safi sana Bossman.

Nakumbuka DarHotwire kulikuwa na mizaha mizaha mingi.

Na hata huku JF watu tulikuwa tunaambiana hivyo hivyo, kwamba kama unataka udaku nenda DarHotwire.

Lakini kusema ukweli kipindi hicho..2006 - 2008 sikuweza kabisa kudhani kuwa JF ingetimiza miaka 10.
Asante kwa kumbukumbu nzuri ndugu Nyani Ngabu (McCain). Hilo la Darhotwire ni kweli, tulikuwa tunaambiwa kama ni siasa basi tuende JF ndiko kunahusika. Kule kulikuwa na mambo ya MMU mengi.
Ni kumbukumbu murua sana hii.
 
Mimi nilikuwa sina bahati nayo jamii forum nilikuwa nikiifatilia muda mrefu ila kila nikijiregister nasahau password, nikireset mara password inagoma nikaachana nayo, nikawa na peruzi tu kama mgeni, baadae nikaamu sasa wacha niifatilie niwe na password niweze kuchangia mawazo, ila mie darhotwire ndo nilikoanzia 2003 na baadae ndo nikhamia hapa nadhani itakuwa nina miaka 6 ya kujiunga japo muda mwingi niliperuzi kama mgeni.
Aisaee Asmaa una matatizo ya memory !! Full kusahau....
 
Nilijiunga JF kwa ajili ya kupambana na mpuuzi mmoja alikuwa anajiita Rev Masanilo mie nikiwa na ID yangu kapuni baada ya kupigwa life ban mwaka mpya nikaibuka na Ritz.

Pongezi kwa JF nilikuwa namsubua sana Invisible kwenye PM kuhusu kunipa ban kila wiki.

Nakumbuka nilinyimwa access ya kuingia jukwaa la siasa.

Teh teh teh.
Duuh! Mkuu we ndo Malaria Sugu?
 
Back
Top Bottom