Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Yote ya yote tabia ya hii forum ni kua na multiple IDs kila mtu anayo walau mbili...
 
Napenda kutoa pongezi kwa uongozi na wanachama.binafsi nilijiunga rasmi kama mwanachama Mwezi November 2010 nimejua mengi kupitia majukwaa tofauti. Natoa pongezi sana kwa uongozi wa Jamii forum.
Thank you Jf Team
 
Hivi kimbweka yuko wapi? na Zumbe Mkuu nilikuwa nawafuatilia kama guest hapa Jf.
 
ni sehemu mojawapo ambayo kabla sijapost kitu lazima nifikirie...outcome ya hicho nitakachoandika n nn?..hongera jf
 
niwapongeze wanajf wote humu mods wote ,waanzilishi wa jamii forum leo tuna jamii iliyohabarika vyema ,jamii forum imekuwa ni kioo cha jamii chanzo cha habari za uhakika ,mahali pa watu wenye fikra kubwa ,pia niwape pole wale waliokiuka maadili ya jamii forum na kufungiwa naamini wamejifunza kitu,na pia wale ambao hajakutana na adhabu hizo wasibweteke ,watii sheria ,tuitumikie jamii ,pia niwapongeze wale members wenzetu waliopata bahati ya kuteuliwa nyadhifa mbalimbali wanatuwakilisha serikalini naanmini tuko wengi humu tukipewa nafasi tuna weza kutumikia jamii bila shida yeyote ,hongereni sana jf.
 
Nyani Ngabu

This is a WONDERFUL thread. Wonderful indeed.

Mie naomba nitoe pongezi kwako NN, hongera sana kwa kuwa a consistent member on JF period! Regardless nini… Hili linafanya uwe na experience na kumbukumbu ya kutosha ya wapi JF imetoka, wapi ilipo na wapi inaweza kuwa inaenda. Kwa maelezo yako katika post ya kwanza pamoja na post zingine, umetukumbusha mbali.. Na kwa wengi ambao ni wakongwe ninaamini imewagusa.

Nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa dhati Maxence Melo na Mike Mushi kwa kuanzisha JamiiForums na kuiwezesha ikafika hapa ilipo. Miaka 10 si mchezo, na zaidi, si mchezo kwa misingi kwamba JF ilivyoanza na ilipo inaendelea kukua kila kukicha - tokana na watumiaji wake, kila kinachopatikana, watu wanaofikiwa na nafasi yake kwa jamii kwa ujumla. Wala si ajabu kwamba imefika wakati inakumbwa na vikwazo vya kisheria. Inshaallah Mwenyezi Mungu ataweka wepesi na shauri hilo litaenda sawa.

Natoa pongezi kwa team yote ya Jamii Media (Wafanyakazi wa FikraPevu & JamiiForums), jinsi kwa njia moja ama nyingine wanachangia JamiiForums kuendelea kuwa JamiiForums yenye mafanikio chini ya uongozi wa Mkurugenzi Maxence Melo na Management kwa jumla. Hongereni sana.

Natoa pongezi kwa members wooote! Tuna members wengi sana JamiiForums, kila mmoja akiwa na nafasi yake, kila mmoja akiwa huru kuchukua au kufuata angle yake, kila mmoja akiruhusiwa kufuata itikadi ama imani yake (kwa uhuru kabisa) ili mradi havunji sheria za Jf. Members wa JamiiForums ndiyo JF yenyewe, uwepo wao ndiyo uwepo wa JamiiForums. Kwa misingi hiyo kila mmoja anapongezwa kwa kuwa a part of JF.

I have had some of my great moments in my life hapa hapa JamiiForums na kupitia JamiiForums. Nimejifunza mengi, nimeongeza ujuzi, nimepata maarifa na nimeelimika kwa kupitia hapa. Hadi leo hii nina marafiki wa dhati na wa karibu ambao nimewapatia hapa… They are a great part of my life; and they will forever be.

Wengi humu mmeongea meeengi, na naunga mkono karibu yote yale yaliyogusiwa. Kwa upande wangu yamenikumbusha mbali, yamenichekesha na kufurahisha. La msingi ambalo ningependa kugusia ni kwamba kunaweza kukawa kuna idadi kubwa ya wanaojiunga kushindwea kusimamia mijadala, ila suala la kuanzisha mada ukawa na uhakika wa kupata wachangiaji wa kubadilishana mawazo, ni suala ambalo halibadiliki na limekuwa consistent, kwa maana nyingine; hilo ndiyo msingi mzima wa kuwa na thread na ukapata mrejesho wa kile ambacho kimewasilishwa. I wish members wa zamani wote warudi, ila bahati mbaya 'Wishes are not horses'...

I could say thousands… But all in all it narrows it down to kuipongeza JamiiForums kutimiza miaka 10. Max kuna mahala aligusia kutakuwa na sherehe ya kutimiza miaka 10 ya JamiiForums, tusubiri hilo kwa hamu.

Mkuu Nguruvi3, idawa, Rapherl, Matola, Consigliere & double R, nawasalimu with Love. Asante kwa salamu, ninazipokea kwa furaha; mimi pia namiss kuwepo hapa consistently. Ninaamini tutazidi kuonana hapa.

Long Live JamiiForums. Long Live the Founders.

Pamoja Saana!

AshaDii.
 
nakumbumbuka mara ya kwanza natumia jamii forum ilikuwa usiku niliangaika sana kufungua account hahahaha
 
Wapi @Companero ...nakumbuka thread moja ya kinyamwezi kule jukwaa la Celebrities kuhusu DJ Premier vs DJ Funk Master flex (kama sikosei) ..... Kiranga , @Companero walitia chachu nzuri sana ya mjadala.
Mimi nilianza kufatilia JF kuanzia vuguvugu la uchaguzi wa 2010 nikiwa bado mtumishi wa umma...nikajiunga mapema 2011...wengi sana wamenivuta kwa michango yao makini enzi hizo ....heshima kwenu wakongwe wote ....bado najifunza ...
 
Wapi @Companero ...nakumbuka thread moja ya kinyamwezi kule jukwaa la Celebrities kuhusu DJ Premier vs DJ Funk Master flex (kama sikosei) ..... Kiranga , @Companero walitia chachu nzuri sana ya mjadala.
Mimi nilianza kufatilia JF kuanzia vuguvugu la uchaguzi wa 2010 nikiwa bado mtumishi wa umma...nikajiunga mapema 2011...wengi sana wamenivuta kwa michango yao makini enzi hizo ....heshima kwenu wakongwe wote ....bado najifunza ...
mkuu unaweza ukanipa link ya huo uzi
 
Nguruvi3 mie nipo ila nimekua mzee sana kaka
Tunahitaji busara za uzeeni, mkikimbia jamvi vijana wanacheza cha ndimu na nage

Jamvi lenyewe moja, vijana wakiharibu itauwaje? kwani hujasoma daladala zenye maandishi, mbuzi kala mkeka wapambe watakaa wapi kwi kwi kwi
 
Hongera JF... Hongera Maxence na viongozi wote humu. Mi nilijiunga 2009 nikiwa Ughaibuni yani ilikua nikiingia JF rahaa nakua kama nipo Tanzania vile na home sickness yote inaisha. Hadi sasa najifunza mengi.
 
Kuna watu kama mimi nimejoin karibuni mwaka jana ila nilikuwa nafatilia nyuzi sababu ukiwa nje ndo ilikuwa the only way ya kupata breaking news. Nilikuwa nasita kujoin sijui kwanini mpaka mwaka jana nikaona liwalo na liwe ngoja nijoin. Sijaona polisi mlangoni kunikamata. Nawashukuru wale waliowezesha JF kufikia hapa na wachangiaji wa nyuzi mahiri ambazo zimetuliwaza, sikitisha, elimisha na kutuchekesha saana. Nafurahishwa sana na Avatar za watu kuliko chochote.

Melo na Mods wote komaa kuhusu hii issue ya Polisi. Mimi kama Member niko tayari kuchangia gharama za lawyer kama mtahitaji mradi mtujulishe kivipi ili tusije tukaingia mkenge na hao NSHEMBA maana huwa wanakuja kwa kila aina.

Nimeweza kupata marafiki humu na vile vile nimepata maadui ambao wamenitumia mess ambazo nilishindwa hata kujibu nikaona ukishayavulia nguo lazima uyaoge. Nyani Ngabu thanks a lot for this thread, you made all of who care for this Place called JF happy. Be blessed. xxxxxxx
 
Back
Top Bottom