'Miafrika' ilipigwa lini/wapi teki na 'Mizungu'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Miafrika' ilipigwa lini/wapi teki na 'Mizungu'?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Sep 6, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Assimilado Zakumi, Evolue Ngabu, Civilado Mkandara na wadau wengine wa historia ya 'Miafrika ndivyo Tulivyo' karibuni kwenye mjadala mpana wa historia ndefu ('long duree') ya siasa uchumi ya Mwafrika. Historia hii inaanza na mwanadamu wa kwanza. Dhahania kuu (ambayo mnaweza kuipinga) ni kwamba hapo mwanzo wanadamu wote waliumbwa sawa na walikuwa katika kiwango kimoja cha maendeleo. Sasa ni lini/wapi 'miafrika' ilipigwa teki/bao, yaani ikazidiwa, na 'mizungu? Kwa nini?

  Ufuatao ni mstari wa muda wa kihistoria (historical time line) ambao utatumia kalenda ya Kiafrika, Kiislamu na Kikristo. Tuunganishe hivyo vidoti hapo chini. Humo ndipo kuna siri ya kupigwa bao. Pia kuna ufunguo wa kuwanusuru Waafrika tulioporomoka (regress/mutate) kutoka kuwa 'Wana wa Adamu' na kuwa 'Wana wa Nyani', yaani, kutoka kuwa 'watu' na kuwa 'wanyama' na kutoka kuwa 'Waafrika' na kuwa 'Miafrika'!

  6000BC: Adamu (Mwafrika?)

  ...

  2000+ BC: Nimrod the Mighty

  ...

  2900+BC: Farao Menes wa Misri

  ....

  1000+ BC: Makeda, Queen of Sheba

  ....

  0-AD: Simoni Mkirene

  ...

  1000+ AD: Mansa Mussa

  ...

  1500+AD: Queen Nzinga

  ...

  1800+AD: Shaka the Great

  ...

  2000+AD: Nyani Ngabu (Jiafrika?)

  ...
   
 2. S

  Shamu JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Historia haizungumzii sana Waafrika, zaidi ya Utumwa. Kwa hiyo usiamini sana Historia, ni uongo mtupu.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Sep 6, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Companero, it would serve us well if we, Miafrika, cut all this nonsense of talking the talk and start walking the talk. We, Miafrika, talk more than we do.

  I believe that, yes, probably at some point all humanity was at the same level of development. But when Europe came into contact with Africa, at that point I don't think we were on the same level. They were already ahead of us.

  You all can talk all you want. Theorize all day, everyday. But the bottomline is this: Miafrika Ndivyo Tulivyo and we will never catch up! Prove me wrong.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Sep 6, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Historia haizungumzii Miafrika zaidi ya utumwa? Si vya kuzungumzwa vipo...au? I guess kama vya kuzungumzwa vipo sioni kwa nini visizungumzwe. Labda unambie hakuna vya kuzungumzwa zaidi ya utumwa!
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu ni toka siku tuliyoamini kuwa Wayahudi ni Taifa teule la Mungu..Siku tuliyokubali kuwaweka watu wengine mbele yetu ktk Upendo wa Mungu, ndio siku tulipokubali kiroho kuwa sisi ni duni na inferior..Na ndio siku tuliyokubali kuwa Miafrika - NDIVYO TULIVYO.
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Historia sio msahafu. Inaandikwa. Inahojiwa. Na inaandikwa upya. Hapa tunajaribu kuiandika upya historia ya mwafrika ili tujue imekuwaje akawa hivyo alivyo na jinsi ya kumfanya awe ambavyo yeye anataka kuwa.
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo panacea (dawa ya matatizo yote) ni kutokubali kuwa duni?

  Unakumbuka maneno hayo hapo chini ya Steve (Bantu) Biko?

  The first step therefore is to make the black man come to himself; to pump back life into his empty shell; to infuse him with pride and dignity, to remind him of his complicity in the crime of allowing himself to be misused and therefore letting evil reign supreme in the country of his birth." - We Blacks, I Write What I Like, 1978
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Sep 6, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hizi ngonjera za hawa militants zipo nyingi tu tokea enzi na enzi! Zimefanya nini kubadili jinsi mambo yalivyo?
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  This is not about proving you wrong. It is not a question of 'that is how we are'. Rather, it is a question of why we are who we are even though we don't like being who are? As Chinua Achebe asks, 'when did the rain start beating us'? Why did it start beating us? How did it start beating us?

  More significantly, how can we stop this rain of 'miafrika ndivyo ilivyo' from beating us? How can we reclaim our glorious past of ancient Kemet, Kush, Nubia and Zimbabwe when were who we wanted to be? How can we become what we ought to be? How can we be what we want to be?

  P.S. All great civilizations were founded on the basis of 'talks'/'theorizations' of great sages/philosophers!
   
 10. Companero

  Companero Platinum Member

  #10
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Unapimaje mabadiliko/matokeo?

  How do you measure change/impact?
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 6, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Siyo lazima uwe na limashine lakupimia. Angalia tu jinsi mambo yalivyo. Siyo rocket science kugundua kwamba hakuna lolote la maana lililobadilika. Watu bado wanaishi kwa mlo mmoka kwa siku kwa wastani. Miundombinu mibofu mibofu. Mivumbi kila kona. Vijumba vya udongo. Mahospitalini wagonjwa wanalala kwenye sakafu! Mashuleni watoto wakaa chini. Shule nyingi za msingi na sekondari hata umeme hazina. Hata hapo Dar kuna shule ambazo hazina umeme hadi leo hii. Sasa nambie hizo ngonjera za hao militants wako zimetufikisha wapi?
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  For the hundredth time you got it right Nyani. We are very good at talking, talking nonsense actually, and actaully doing nothing. Ukimuuliza leo mwanasiasa wa Tanzania kwanini Tanzania masikini anaweza akakueleza uongo mwingi kwa siku nzima, lakini ukimuuliza mnafanya nini kuondoa umaskini hapo atapiga blaaaa blaaa.

  Ukuangalia wenzetu huko majuu they really work hard mpaka unawaonea huruma, lakini hapa Bongo we hardly work, ni politiki zisizo na maana tu.

  Siamini kama tulilaaniwa na Mungu kwa sababu tumewekwa kwenye nchi ambazo zimebarikiwa, kama tungekuwa tumelaania labda tungewekwa Indonesia au Asia kwenye matetemeko na mafuriko kila siku, au tungewekwa Siberia kwenye baridi kali.

  I believe kama Tanzania ikipata watu 100 tu determined, wenye vision, wenye mapenzi na Tanzania, it is very possible to prove Nyani wrong. Lakini kwa sasa naona tunaendelea kuprove kuwa Nyani is right, na tutaendelea hivyo kwa miaka mingi, unless otherwise...
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  In addition to that hakuna haja ya kutafuta formula ya kuprove the obvious. Toka Mkoloni ameondoka Tanzania hatuna airport hata moja tuliyojenga, hakuna hata ndege tuliyonunua, airport vyooni wanatumia maji ya ndoo zenye kutu utadhani misikiti ya vijijini, tumeharibu Dar es salaam na kuifanya iwe ya kiswahiliswahili na kuanza kufanana na big village badala ya city. Ikulu inakuwa sehemu ya futari badala ya sehemu ya kazi za kiserikali.
  How do you want to measure negative change my brother, it is very visible hakuna ugumu. Uliza mtu yoyote aliyeishi wakati wa ukoloni ayakwambia kama Kariakoo kulikuwa kunanuka, au kama magomeni koto nyuma zilikuwa zinavuja.
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Sep 6, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kihistoria nadhani labda unaweza kusema kuwa waafrika "Tulionewa na Mungu Baada ya Kutupendelea na Kutupa Mazingira Mazuri Ambayo Hayakutuhitaji Kutumia Bongo Zetu ili Kukabiliana Nayo."" Matokeo yake tukalemaa na kuwa vilaza wa kutupwa. Tulikuwa na chakula tele na tungeweza kulala popote bila wasiwasi,. Kitu pekee tulichotakiwa kupambanoa nacho ni wanyama wa porini, na kama unakumbuka basi unajua kuwa tuligundua silaha za kuopambana nao.

  Kinachotusumbua leo, ni hicho kilema tulichorithi kutoka kwa mababu zetu.
   
 15. Companero

  Companero Platinum Member

  #15
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  NN & BL: Kwa hiyo hakuna hata badiliko dogo 1 zuri/chanya Afrika?

  P.S. I thought change can be evolutionary and/or re-volutionary!
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ina maana kati ya Watanzania 40,000,000 hatuna hata hao 100 (0.00025% ) achilia mbali 1 ya 10 (10%)?

  Ina maana heri mkoloni - tusaini mikataba nao warudi kututawala/kutuongoza kwa ridhaa yetu wenyewe?
   
 17. Buricheka

  Buricheka Member

  #17
  Sep 6, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais anakaa Ikulu, anakula Ikulu, hebu nisaidie, wewe ungetoa pendekezo Rais Muislam aende kufuturu wapi?
   
 18. T

  Tom JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halafu Mji mkuu wa nchi kuwa DAR pia inachangia kutukwamisha, watu wengi toka bara huhamia DAR wakakaa nyumba za vyumba sita nk na kuiga uswahili wa wenyeji wao kama maisha ya kula mlo mmoja, kusema sana, nk wakidhani ndio uborn town kumbe ni uvivu. Ona wanasiasa wetu wanavyokua maarufu wa bla bla baada ya kuhamia DAR. Mji mkuu ungekua Arusha, Njombe ama Moshi mambo yangekua mazuri kwani wenyeji huko ni wachapa kazi.
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  "I am ready to concede that on the plane of factual being the past existence of an Aztec civilization does not change anything very much in the diet of the Mexican peasant today. I admit that all proofs of a wonderful Songhai civilization will not change the fact that today the Songhais are under-fed and illiterate, thrown between sky and water with empty heads and empty eyes...But...The claim to a national culture in the past does not only rehabilitate that nation and serve as a justification for the hope of a future national culture. In the sphere of psycho-affective equilibrium it is responsible for an important change [kutoka 'miafrika ndivyo ilivyo' kwenda 'waafrika watakuwa vile'] in the native" - Frantz Fanon on 'The Wretched of the Earth
   
 20. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Tena tushukuru hata huo utumwa na ukoloni wa wazungu , kwa hiyo utaona leo sijui 50 cents, 2boys wanajinafasi huko bila hivyo leo wangekuwa wanakula OSOKONOI .

  Unajuwa maana ya osokonoi? kaome kitabu kinaitwa Is it Possible.
   
Loading...