'Miafrika' ilipigwa lini/wapi teki na 'Mizungu'?

Toward Unsilencing 'Silences in African History'

“Of all the crimes of colonialism there is none worse than the attempt to make us believe we had no indigenous culture of our own; or that what we did have was worthless – something of which we should be ashamed, instead of a source of pride”
Julius Nyerere

"History will one day have its say. It will not be the history taught in the United Nations, Washington, Paris, or Brussels, however, but the history taught in the countries that have rid themselves of colonialism and its puppets. Africa will write its own history, and both north and south of the Sahara it will be a history full of glory and dignity"
Patrice Lumumba
 
the damage was done ions ago,our grand grand fathers,were wanderers for too long,for some reasons they could not domesticate and tame wild animals.NB-all domesticated animals in africa are imports we couldnt even tame the elephant-indians did.Not being able to domesticate animals etc, we could not settle down and in the process Division of Labour passed us by,with this setback,ORGANISATION crept into our societies long after others had a headstart-to this day we are still playing catchup
 
Nimelipenda sana jibu hili kutoka kwenye thread ya JF kuhusu Mwakikagile:

I remember asking him [Mwakikagile], I don't know if he remembers this but he probably does since he had excellent memory, but I remember asking him about 30 years ago if he thought that Africa would ever develop like Europe did. He responded quickly and said, no, not in our life time; it is too short a time. Even Europe did not develop that fast. It took hundreds of years for Europe to develop, he said. I agreed with him on that. But he also brought up the Soviet Union and said it was able to industrialize (in heavy industry) within 40 years since the Russian Revolution because of central planning, although he emphasized that the foundation of modern Russia was laid before then by Peter the Great, an achievement that helped facilitate progress at a faster pace years later, especially in education and heavy industry, after the Bolsheviks seized power and started implementing their strategy of central planning.
 
Ina maana kati ya Watanzania 40,000,000 hatuna hata hao 100 (0.00025% ) achilia mbali 1 ya 10 (10%)?

Ndio maana yake wangekuwa hata 20 mambo yasingekuwa shaghalabagala kama sasa. Waliopo kuna wachache wana qualities nzuri lakini hawako determined au kwa sababu za kisiasa wanazuiwa au wanashindwa kutumia akili zao. ajabu hao hao wakiwa nje wanafanya kazi kuliko hata wazungu.

Ina maana heri mkoloni - tusaini mikataba nao warudi kututawala/kutuongoza kwa ridhaa yetu wenyewe?

Ndio maana yangu, tuwape serikali watawale sisi tuangalie tu kama wanatuibia au kama wanaleta ujinga, wao si waharibifu na hawapigi porojo wanafanya kazi vizuri sana. Evidence za utendaji wao zipo mpaka leo. Japokuwa walikuwa wezi, lakini walijaribu kujenga barabara, shule, madaraja, hata miji iliyopangika. La kuwasimamia hilo naona tunaweza kufanya kuliko kutawala wenyewe, miaka 40 ya uhuru tume-prove failure.
 
Rais anakaa Ikulu, anakula Ikulu, hebu nisaidie, wewe ungetoa pendekezo Rais Muislam aende kufuturu wapi?

Unauliza kitu gani? Hujui kuwa Uislamu na Waislamu ndiyo vipimo vya mediocrity (ufinyu) na general inferiority (uduni) uliyoenea kwenye kila sekta ya jamii Tanzania na in fact ndiyo sababu muhimu inayochangia Taifa na nchi kuwa nyuma na kudumaa siku zote.
 
Toward Unsilencing 'Silences in African History'

"Of all the crimes of colonialism there is none worse than the attempt to make us believe we had no indigenous culture of our own; or that what we did have was worthless – something of which we should be ashamed, instead of a source of pride"
Julius Nyerere

"History will one day have its say. It will not be the history taught in the United Nations, Washington, Paris, or Brussels, however, but the history taught in the countries that have rid themselves of colonialism and its puppets. Africa will write its own history, and both north and south of the Sahara it will be a history full of glory and dignity"

Mkuu nadhani hapa ndipo utamwelewa Nyani Ngabu vizuri anachosema yeye..
Yaani toka Lumumba, Nyerere na majuzi Prez. Obama huko Ghana wote wameimba wimbo huo huo tuu hakuna tulichofanya.. yaani toka enzi hizo tunajua sababu kwa nini tuko hapa, ni zaidi ya miaka 40 lakini ndio kwanza tunazidi kujichimbia zaidi ndani ya chimo la maji taka..
 
Kwa hiyo tufanyeje?Tubwage manyanga? Hakuna njia ya kutokea?
 
In addition to that hakuna haja ya kutafuta formula ya kuprove the obvious. Toka Mkoloni ameondoka Tanzania hatuna airport hata moja tuliyojenga, hakuna hata ndege tuliyonunua, airport vyooni wanatumia maji ya ndoo zenye kutu utadhani misikiti ya vijijini, tumeharibu Dar es salaam na kuifanya iwe ya kiswahiliswahili na kuanza kufanana na big village badala ya city. Ikulu inakuwa sehemu ya futari badala ya sehemu ya kazi za kiserikali.
How do you want to measure negative change my brother, it is very visible hakuna ugumu. Uliza mtu yoyote aliyeishi wakati wa ukoloni ayakwambia kama Kariakoo kulikuwa kunanuka, au kama magomeni koto nyuma zilikuwa zinavuja.

Bongolander,

Mimi nikiwa ni Mwislamu ninavyokusoma kwa nini nisiishie kusema Wakristo ndivyo walivyo, kutwa kucha kudharau Waislamu?
 
Kwa hiyo tufanyeje?Tubwage manyanga? Hakuna njia ya kutokea?
Hakuna saababu wala haja ya kubwaga manyanga.. Isipokuwa ni kutekeleza Ujumbe tunazopewa toka enzi za Nuhu, kina Mkwawa, Mirambo, Mangi sina U name it.. zilifanyiwa kazi hadi tukaupata Uhuru wetu.. lakini baada ya hapo tumevaa misuri yetu tunacheza bao na kunywa kahawa jioni tunakutana kwenye kitumoto..kisha ukiuliza unaambiwa kahawa ni ya Waislaam sijui kitumoto ya WQakristu kumbe ni kundi hilo hilo la Mijuha inazunguka kote kutangaza uvivu wao wa kufikiri..

Mkuu wangu toka kina Lumumba, Kwame Nkurumah, Nyerere, Bob Marley, Martin Luther King, Malcom X na wengine wote wazungumze au waandike vitabu vya kuhamasisha waafirka au watu weusi utakuta kwamba hakuna nguvu hizo zikifanyika Afrika. hakuna vikundi vya vijana au wananchi wanaoenzi fikra hizo kwa vitendo zaidi ya kuunda Foundation under their name kuomba fedha kwa wazungu..Zile fikra za Mwalimu hata ktk hiyo foundation yake hazipo zaidi ya nukuu ya vitabu na hotuba zake..sana sana tunawacheka wale wanaosema zidumu fikra za mwalimu kwa sababu hizi ni fikra tupu ambazo haziwezi kufanya kazi bila kuziweka ktk matendo hata kama zili fail wakati wa Cold war!
Hakuna vikundi vinavyofanya hata moja alozungumza Bob Marley au Martin Luther zaidi ya wenzetu weusi marekani ambao kwa kufuata mafundisho ya kina Martin Luther King, Malcom X na wengine wameweza kujijikomboa kwa kiasi kikubwa hasa hata kufikia leo wana rais mweusi.

Tunachofanya sisi waafrika ni sawa na kubeba Biblia au msahafu lakini hatusali, hatuombi wala kufanya ibada ya aina yoyote ile. Kuta zetu na makabati yetu yamejhaa vitabu vya kila aina na pengine tumevisoma vyote iwe eleimu ya dini au Dunia.. Ukweli unabakia it's only few pages ya vitabu hivyo tumepractice ktk maisha yetu.. Kwa hiyo tulichokuwa nacho ni imani tu ya kuwezekana.. ile ya ONE DAY YES! wakati tunacheza kamari na maisha yetu wenyewe...
 
Bongolander,

Mimi nikiwa ni Mwislamu ninavyokusoma kwa nini nisiishie kusema Wakristo ndivyo walivyo, kutwa kucha kudharau Waislamu?

Mkuu umenielewa vibaya, siko kwenye kudharau dini ya mtu wala siko kwenye kutukuza dini ya mtu. Mimi ni mwislamu ndio maana najua hata misikiti ya vijijini, kwa hiyo natoa mifano kwa kuonesha hali duni ninayoiona kwenye jamii yetu.

Hili la umaskini na uduni linatuweka pamoja, ukienda kwenye mji au kijiji chochote wakristo,waislamu au hata watu design ya kingunge utaona ni yaleyale tu, hata kudharau watu wa dini nyingine ni sehemu ile ile tu ya "ndivyo tulivyo". We still have a long way to prove Nyani Ngabu otherwise.
 
Companero, it would serve us well if we, Miafrika, cut all this nonsense of talking the talk and start walking the talk. We, Miafrika, talk more than we do.

I believe that, yes, probably at some point all humanity was at the same level of development. But when Europe came into contact with Africa, at that point I don't think we were on the same level. They were already ahead of us.

You all can talk all you want. Theorize all day, everyday. But the bottomline is this: Miafrika Ndivyo Tulivyo and we will never catch up! Prove me wrong.

NN:

You are doing a fabolous job here. Hapa ninapoishi nilikuwa naalikwa kwenye mikutano ya Pan Africanism. Kwenye mkutano mmoja akatokea mama kutoka Haiti anaomba misaada ya kwenda kufungua radio na shule za kimapinduzi Haiti ambazo zitafundisha kwa kutumia Creole.

Nikamuuliza kwani kuna tofauti gani kati ya kufundisha kwenye Creole na kufundisha kwenye proper French. Akasema Creole ni lugha yetu wenyewe na French is a Bourgeoisie Language.

Nikamwambia kuwa Tanzania ilijaribu kutumia lugha yake lakini hakuna mafanikio makubwa yaliopatikana. Au kwa lugha nyingine, mfumo wa elimu wa Tanzania unaboronga. Basi nikazua kizaazaa kwamba ninamtukana Nyerere na Pan Africanism nzima.

Mama aliyetoa mada akatoa mfano wa wayahudi kufufua na kutumia lugha yao. Na vilevile mwiEthiopia fulani kuandika kitabu cha theory of relativity katika lugha ya kwao ya Oromo.

Nikamwambia kwa bahati nzuri niliishi Ulaya. Na wayahudi wengi wametokea nchi za Ujerumani, Poland, Czech na nchi zingine za Ulaya Mashariki. Na katika nchi hizi walikuwa na vyuo vyao vikuu na ndio waliokuwa wanasayansi mahiri. Pamoja na yote hayo walikuwa na lugha yao ya Yiddish. Hivyo wao kutafuta terminologies ya masomo mbalimbali, ilikuwa sio kitu cha kutoa jasho sana. Pamoja na hayo yote kulikuwa na resources za kutosha kutoka kwa Uncle Sam.

Kwa upande mwingine kutumia Creole au Swahili ni kitu kizuri. Lakini lugha zenyewe hazina wataalamu wa kutosha kutoa mchango wa maana kwenye lugha yenyewe na kwenye taaluma mbalimbali. Na cha muhimu zaidi hakuna resources za kutosha.

Katika mijadala hii kuna vitu viwili muhimu. Kwanza, kuna majadiliano ya kutunza pride. Haya tumeshayafanya sana. Lakini wakati umefika kuonyesha kuwa yale tunayoyasema yanaambatana na vitu vinavyoweza kuonekana.

Pili ni lazima tuwe realistic. Kuna miradi tunairudia sana au tunaitamani kuifanya lakini haina matokeo yoyote yale ya kubadilisha jamii. Tulikuwa na miradi ya elimu ya kufundisha kwa lugha zetu, tumeboronga. Kama kuna uwezekano wa ku-swallow pride angalau kwa muda fulani hili tujifunze vitu kwa ajili ya manufaa ya vizazi vinavyokuja, basi ni muhimu kufanya hivyo. Kuliko kuwa na majaribio yenye matarajio ya kushindwa.
 
Kihistoria nadhani labda unaweza kusema kuwa waafrika "Tulionewa na Mungu Baada ya Kutupendelea na Kutupa Mazingira Mazuri Ambayo Hayakutuhitaji Kutumia Bongo Zetu ili Kukabiliana Nayo."" Matokeo yake tukalemaa na kuwa vilaza wa kutupwa. Tulikuwa na chakula tele na tungeweza kulala popote bila wasiwasi,. Kitu pekee tulichotakiwa kupambanoa nacho ni wanyama wa porini, na kama unakumbuka basi unajua kuwa tuligundua silaha za kuopambana nao.

Kinachotusumbua leo, ni hicho kilema tulichorithi kutoka kwa mababu zetu.

Inawezekana Mkuu. Jamaa yangu mmoja wakati zinaanzishwa shule za msingi kwa wote, alipangiwa kufundisha jamii za wasandawe. Anasema kuwa wanafunzi walikuwa wakiona ndege, basi wataacha masomo na kuanza kumfukuza ndege mpaka wa mpate. Na kwa usalama wao shule ikajengwa na madirisha makubwa, hili kuwapa nafasi wanafunzi kupitia sehemu yoyote wanayotaka.
 
Zakumi kumbe unaudanganya mpaka umma wa African Diaspora? Nani kasema Tanzania ilijaribu kutumia lugha yake? Tulichofanya ni kuchanganya lugha - Kiingereza Sekondari, Kiswahili Msingi! Na hili ndilo kosa kubwa kuliko yote alilolifanya Mwalimu.!

Alafu Ndugu naona una nyepesi nyepesi nyingi zilizojaa kasumba kuhusu jamii za wafugaji na wawindaji. Hizi dharau ndizo zinarudisha nyuma maendeleo ya ndani. Hao ndio modeli ya maendeleo asilia endelevu (sustainable autochthonous development)!

P.S. Hivyo viatu ulivyovaa hapo ndio mfano halisi wa ubunifu wa kutohoa maarifa ya kigeni na kuyachanganya na maarifa ya asili ili kuleta maendeleo ya ndani ya jamii (local development)!
 
Companero.....,
The people who forget their struggle and their history are a people who have no awareness of their destiny," Evo Morales. ...Bolvia Peoples president...2009.
 
Companero.....,
The people who forget their struggle and their history are a people who have no awareness of their destiny," Evo Morales. ...Bolvia Peoples president...2009.

Perhaps that works in Bolivia and in other Bolivarian states. For sure we know our history, but also for sure we have forgotten the core principle of our struggle (well being of Mtanzania), if not then we have intentionally messed it up. in 40's and 50's we organised ourselves to get rid of a white thief from London, and because of our ignorance we celebrated the coming of the other, the native one who is worse than the former(ndivyo tulivyo). We fought for our well being, and ended up in a sutuation worse than when the white thief was in the house. Even worse we are still accusing him for our ills most of which are post 1961 and most of which are locally made
 
P.S. Hivyo viatu ulivyovaa hapo ndio mfano halisi wa ubunifu wa kutohoa maarifa ya kigeni na kuyachanganya na maarifa ya asili ili kuleta maendeleo ya ndani ya jamii (local development)!

Umeona miguu yake ilivyopauka lakini? Hayo makatambuga hayahitaji kiwango chochote kikubwa cha ubunifu. Kwanza hayakutengenezwa (from the looks of them) tokea mwanzo kama makatambuga. More than likely yalikuwa matairi ya lori na watu kwa dhiki yao wakaona ni heri na bora wajitengenezee footwear.

Halafu Zakumi usikute kayaokota sehemu...kwa sababu yako oversized! Lol
 
Zakumi kumbe unaudanganya mpaka umma wa African Diaspora? Nani kasema Tanzania ilijaribu kutumia lugha yake? Tulichofanya ni kuchanganya lugha - Kiingereza Sekondari, Kiswahili Msingi! Na hili ndilo kosa kubwa kuliko yote alilolifanya Mwalimu.!

Alafu Ndugu naona una nyepesi nyepesi nyingi zilizojaa kasumba kuhusu jamii za wafugaji na wawindaji. Hizi dharau ndizo zinarudisha nyuma maendeleo ya ndani. Hao ndio modeli ya maendeleo asilia endelevu (sustainable autochthonous development)!

P.S. Hivyo viatu ulivyovaa hapo ndio mfano halisi wa ubunifu wa kutohoa maarifa ya kigeni na kuyachanganya na maarifa ya asili ili kuleta maendeleo ya ndani ya jamii (local development)!

Companero:

Sina kasumba zozote zile lakini nimechoka na mambo yako ya kutuimbisha kuhusu wafugaji na wawindaji.

Na mifano mingi sana niliyotoa kuashilia kuwa jamii karibu zote zilianza kwenye ufugaji, uwindaji na ukusanyaji wa matunda au mboga mwitu. Lakini uzio wa Vasco Da Gama uliongeza idadi ya vyakula na settlements.

Hivyo miaka 300 iliyopita kulikuwa hakuna tofauti kubwa sana kati ya Mchagga na Mmasaai. Hivyo wewe kutuimbisha kuwa watu wa jamii zingine kukopi wamasaai ni kutothamini maendeleo ya jamii zingine na kutaka kuwarudisha kule walikotoka.
 
Umeona miguu yake ilivyopauka lakini? Hayo makatambuga hayahitaji kiwango chochote kikubwa cha ubunifu. Kwanza hayakutengenezwa (from the looks of them) tokea mwanzo kama makatambuga. More than likely yalikuwa matairi ya lori na watu kwa dhiki yao wakaona ni heri na bora wajitengenezee footwear.

Halafu Zakumi usikute kayaokota sehemu...kwa sababu yako oversized! Lol

Kwikwikwi. Hivi viatu ni chupa za plasti za cocacola na vinatumika na vijana wa Zimbabwe kwenye mashimbo ya dhahabu.

Na kwa bahati nzuri kiongozi wa nchi hiyo ni mtu mwenye digrii saba, I mean one of the talented tenth.
 
Mugabe ana shahada 7? Are you serious? Kazitoa wapi zote hizo wakati muda mwingi katika maisha yake katumia akiwa msituni au madarakani. Huo muda wa kusoma alipata wapi? Kama ni kweli basi jamaa atakuwa "kichwa" kama Tuntemeke Sanga...Lol
 
Wikipedia:

Originally graduating with a Bachelor of Arts degree from the University of Fort Hare in 1951, Mugabe subsequently earned six further degrees through distance learning including a Bachelor of Administration and Bachelor of Education from the University of South Africa and a Bachelor of Science, Bachelor of Laws, Master of Science, and Master of Laws, all from the University of London External Programme. The two Law degrees were earned while he was in prison, the Master of Science degree earned during his premiership of Zimbabwe.
 
Back
Top Bottom