Mhe. Godbless Lema alichana Jeshi la Polisi

Pasco naheshimu sana mawazo yako na mijadala unayotoa hapa jamvini.
Bila shaka unashindwa kusema ukweli kwa kuhofia kukosa "tender" za maonyesho mbali mbali wanazokupa.
Pasco ni pen name ya mwana JF, kumfananisha na Pasco mwingine yoyote unayemfahamu wewe na kuposti humu mfanano huo,
hiyo ina amount to 'name calling' na adhabu yake ni 'ban', kwa vile naamini umefanya kosa hili bila kujua, Pasco wa JF, amekusamehe, sitakuripoti kwa mode, naomba tuchangie mada na sio mtoa mada!
 
Naibu spika is the worst leader in our parliament, second to makinda.
Sio siri, mimi ni miongoni mwa waliokuwa wakimshutuma Mama Makinda, jana na leo, nimemkumbuka, She is much much better!.
Naibu Spika ana "complex" fulani!.
 
Je atazuia ngoma kuwa kwenye hansard pia ? Sababu zipi za kuwatoa nje ? Yaanii hawa jamaa wanaijenga Chadema bila ya kujua hakika .Uonevu huu unawapa nguvu Chadema sana sana .
 
Lema sio tuu ni jembe, anaweza kuwa ni zaidi ya jembe, bali ni shoka kabisa au sime ya makali kuwili, asipodhibitiwa ndani ya chama chake, anaweza kuhamashisha maandamano ya wananchi wote, kuelekea Ikulu, kumng'oa rais halali, hivyo anaweza kutenda jinai ya uhaini kwa jina la siasa.
Sio siri, Lema ni hatari, hamungunyi maneno!.

hapo kwenye red, ni hatari kwa mafisadi na majangili, ila ni mkombozi na tumaini kwa walalahoi, sisi tunasubiri aongoze mapambano ya kuwang'oa mafisadi ikulu, nakumbuka yale maandamano ya arusha yeye ndo wa kwanza kutokeza bara barani na kusema piipooooosss....ndo wengine wakafuata.
 
nazani ccm wameamua kuja kwa mtindo huu mpya-wa kutoa watu nje-
Hivi wanataka kila mtu asifie serikali hata pale pasipo sifika?jeshi lapolisi ni chafu sana-wawaache watu wazungumze-
 
Pasco ni pen name ya mwana JF, kumfananisha na Pasco mwingine yoyote unayemfahamu wewe na kuposti humu mfanano huo,
hiyo ina amount to 'name calling' na adhabu yake ni 'ban', kwa vile naamini umefanya kosa hili bila kujua, Pasco wa JF, amekusamehe, sitakuripoti kwa mode, naomba tuchangie mada na sio mtoa mada!

Mkuu usiogope kivuli chako, wapi nimefanya name calling??

Hata kama siye (ingawa ninashaka na utetezi wako) lakini kwa jinsi unavyojaribu kum"brand" Lema kwamba ni mhaini huku ukikiri kwamba hamung'unyi maneno, sihitaji kwenda shule ya kata kujua kwamba una maslahi binafsi na serikali inayoambiwa ukweli bungeni.

Tuendelee kukata issues hayo mengine tuyaache, ila ukitaka ushahidi njoo chemba.
 
si vibaya serikali kupokea ushauri toka upinzani hata kama unamiza maana twaambiwa ukweli utawaweka huru.
 
Pasco ni pen name ya mwana JF, kumfananisha na Pasco mwingine yoyote unayemfahamu wewe na kuposti humu mfanano huo,
hiyo ina amount to 'name calling' na adhabu yake ni 'ban', kwa vile naamini umefanya kosa hili bila kujua, Pasco wa JF, amekusamehe, sitakuripoti kwa mode, naomba tuchangie mada na sio mtoa mada!
Pasco usitishe watu nani asiyekujua mara nyingi unapotuletea habari unajivisha ngozi ya kondoo kama vipi hakuna mtu aliyekulazimisha wewe leta habari ilivyo sio kuongeza ambayo hayapo mambo ya uhaini wa Lema yanatoka wapi nyamb................f.
 
hapo kwenye red, ni hatari kwa mafisadi na majangili, ila ni mkombozi na tumaini kwa walalahoi, sisi tunasubiri aongoze mapambano ya kuwang'oa mafisadi ikulu, nakumbuka yale maandamano ya arusha yeye ndo wa kwanza kutokeza bara barani na kusema piipooooosss....ndo wengine wakafuata.

Swadakta mkuu, labda pasco atufahamishe kama kuna maana nyengine ya hatari tofauti na tunayoifahamu.

Polisi hawa walioshindwa kuthibiti wizi, ujambazi, ajali za barabarani na kuishia kuua raia wasio na hatia wakiambiwa ukweli ndo umwite aliyewaambia ukweli ni hatari!!??
 
Mkuu usiogope kivuli chako, wapi nimefanya name calling??

Hata kama siye (ingawa ninashaka na utetezi wako) lakini kwa jinsi unavyojaribu kum"brand" Lema kwamba ni mhaini huku ukikiri kwamba hamung'unyi maneno, sihitaji kwenda shule ya kata kujua kwamba una maslahi binafsi na serikali inayoambiwa ukweli bungeni.

Tuendelee kukata issues hayo mengine tuyaache, ila ukitaka ushahidi njoo chemba.

ulikuwa hujamuelewa pasco mkuu, haina haja ya kugombana, tunajenga nyumba moja. kama alikuwa anampondea LEMA kachemka, najua anaogopa yatakayomkuta soon tukiingia mtaani. piipooooos......
 
Mkuu usiogope kivuli chako, wapi nimefanya name calling??

Hata kama siye (ingawa ninashaka na utetezi wako) lakini kwa jinsi unavyojaribu kum"brand" Lema kwamba ni mhaini huku ukikiri kwamba hamung'unyi maneno, sihitaji kwenda shule ya kata kujua kwamba una maslahi binafsi na serikali inayoambiwa ukweli bungeni.

Tuendelee kukata issues hayo mengine tuyaache, ila ukitaka ushahidi njoo chemba.
Achana naye huyo Pasco tunaojua kazi yake hatusumbui.
 
Kuhusu Utaratibu: Waziri Lukuvi,
Ameomba muongozo kuhusu kanuni ya 64 ikivunjwa na hotuba nzima ya kambi ya upinzani. Amesema wabunge wamekuwa wavumilivu, lakini hajui kama masikio ya Watanzania yatakuwa mavumilivu.

Mwenye kuijua kanuni ya 64 aiweke.

Mhe. Lukuvi anaweke nukuu baadhi ya maneno yaliyokiuka kifungu hicho cha 64.

64. (1) Bila kuathiri mashart ya ibara ya 100 ya katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika bunge, mbunge:
(a) hatatoa ndani ya bunge taarifa ambazo hazina ukweli
(b) hatazungumza jambo ambalo haliko kwenye mjadala
(c) hatazungumza jambo lolote ambalo linasubiri uamuzi wa mahakama au jambo ambalo lilijadiliwa na kutolewa uamuzi kwenye mkutano uliopo au uliotangulia.
(d) hatatumia jina la rais kwa dhihaka katika mjadala au kwa madhumuni ya kutaka kulishawishi bunge kuamua jambo lolote kwa namna fulani
(e) hatazungumzia mwenendo wa raia, spika, jaji, mbunge hakimu au mtu mwingine yyoyote anayeshughulikia utoaji wa haki, isipokuwa tu kama kumetolewa hoja mahsusi kuhusu jambo husika
(f) hatamsema vibaya ama kutoa lugha ya matusi kwa mbunge au mtu mwingine yoyote
(g) hatatumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watu wengine

(2) Mbunge yoyote anayeamini kuwa mbunge mwingine amevunja au amekiuka masharti ya fasili ya (1) ya kanuni hii atasimama na kusema 'kuhusu utaratibu' na atakaporuhusiwa na spika kusema atalazimika kutaja masharti ya ya kanuni hii yaliyokiukwa na kuvunjwa na mbunge huyo mwingine huku mbunge huyo mwingine akilazimika kukaa na kusubiri mwongozo wa spika kuhusu jambo hilo.
 
Back
Top Bottom