Mhe. Godbless Lema alichana Jeshi la Polisi

Mhe. Godbless Lema alichana Jeshi la Polisi

Mbunge wa Arusha, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Mhe. Godbless Lema analichana Jeshi la Polisi!.

Mhe. Lema, anatoa shutuma mbalimbali kwa jeshi hilo, wakati akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kwenye bajeti ya Mambo ya Ndani.

Amelishutumu Jeshi la Polisi kuhusu serikali kutumia mabavu. Naibu Spika amezuia paragraph fulani isisomwe, Lema akalazimisha kutaka kuisoma kwa kutetea kuwa yeye kama Waziri Kivuli wa Upinzani, asitegemee yuko hapo kuitetea serikali.

Huku akinukuu wapiginia haki maarufu duniani akiwemo Martin Luther King Jnr kuwa 'Amani sio kuweko kwa utulivu, bali kutendwa kwa haki", hivyo Tanzania sio nchi ya amani kwa vile haina haki!

Amelaani mauji yanayofanywa na polisi kama ukwiukwaji mkuu wa haki za binaadamu.

Uchanaji huo wa jeshi la polisi unaofanywa na Mhe. Lema, unafanywa huku Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspecta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na makamanda wake wakuu wakiwa wote wako bungeni.

Uptate kwa hisani ya Edson.
Hiyo paragraph huenda ilikuwa ni mwiba mchungu kwa watawala ndio maana ikatakiwa kufutwa
 
Back
Top Bottom