Mhariri Mtendaji wa Gazeti la MwanaHALISI, Saed Kubenea avamiwa na kumwagiwa tindikali akiwa ofisini kwake

NGD ZANGU WANA JF NAANZA NA SALAAM KWA NA KUTOA POLE KWA WANA HABARI KWA TUKIO HILI NA PIA FAMILIA YA SAIDI KUBENEA HASA NILIPOMUONA JANA MAMA YAKE NILIPATWA NA HURUMA SANA.

PILI,naomba nitoe pole kwa niaba ya wana CCM kwa familia na wanahabari wote na kusema tukio hili ni baya sana na kusikitisha.

Tatu,ningependa kutoa ushauri kwa baadhi ya wana JF ambao tayari wanatoa hukumu kua KUBENEA kafanyiwa kitendo hicho na MVI,or mafisadi or ccm etc inaonyesha ni jinsi gani watu wenye mawazo hayo ni wavivu wa kufikiri na kupenda majibu ya haraka haraka kwa kutumia zaidi hisia bila kua na FACTS.

Ifike wakati tusihukumu bila kua na facts.

KWA NIABA YA CCM NATOA POLE KWA FAMILIA YA KUBENEA NA WANAHABARI WOTE NA TUNAFATILIA KWA KARIBU TUKIO HILI.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Nimesoma asubuhi hii,
Poor guy nusura wamtoe macho
Hii hari sasa inatisha,huko nyuma jamaa wana mtandao si waliwafatafata wale wa Magazeti ya KULIKONI sasa huyu,lkn hii kali kuliko.
 
Pole kwa wote waliojeruhiwa na maharamia hawa. Mungu awajalie kupona haraka.

Tunaomba wote waliohusika na uhaliu huo wasakwe popote walipo ili sheria ichukue mkondo wake.

Inasikitisha sana jamani!!!!!!!!
 
nilianza kuamini uandishi wa habari umevamiwa. lakini sasa napata mashaka kuhusu credibility ya huyu ndugu. Je kama kuna ukweli wa hilo Ndimara na yeye alikuwa anavuta hela? kwa nini na yeye kabamizwa sasa. habari inatisha hii kwa kweli. Mzee mkjj usijaribu kuvuta kidogodogo ndugu yangu, watakumwagia acid, ohhooo!

Kwa hiyo na wewe umeshakubali this simple conspiracy theory bila hata kuipa thought kidogo, pole sana, ndio maana wapiga kura wetu ni rahisi kubadilishwa hata kwa kanga, I can understand!
 
Walianza kumpelea Maofisa wa TRA ambao walivamia ofisi yake kutafuta sababu ya kulifungua gazeti kwa kutolipa kodi nadhani wamekosa pa kumshiklia sasa Wanaitaka Roho yake! HAwa mafisadi watatumaliza maana wanataka Kuifanya Tzanzania kuwa Jamhuri ya MAfisadi.
 
Mkuu GT,heshima mbele,
nimesoma post yako unadai kuwa ndugu Kubenea alikuwa "anavuta hela" kutoka kwa hao mafisadi ili asiwaumbue,na kuwa kumwagiwa kwake acid ni mafarakano baina yake na hao jamaa,sasa kuna FMES alikuwa anadai ushahidi kutoka kwa baadhi yetu waliousisha tukio la kumwagiwa acid kwa Kubenea na CCM an mafisadi,na akawataka watoe ushaidi,sasa mi pia nakuuliza swali moja,hilo swala la Kubenea kuwamo katika payroll ya mafisadi unao ushahidi wake?Ikiwa hoja yako itakuwa sahihi kuwa alifarakana na mafisadi ambao humlipa (kama unavyodai wewe kulingana na ushahidi utakaoutoa hapa) basi wewe na kina ES na wenginea mtakuwa mnakubaliana nasi kuwa tukio hili la Kubenea lina mkono wa mafisadi,na kwa kuwa mafisadi ni wana CCM basi ni CCM ndo wahusika wakubwa,simple logoc will tell you that.Unless you can bring someting else out of all this.
 
Hii habari ni crucial, dont take it simple na kutaka kuifanya ni mzaha. Mafisadi yalianza kwa kununua vyombo vya habari na baadhi ya vyombo yameshindwa kuingia sasa kilichobaki ni kuwaondoa wahariri na wamiliki ili yaweze kutanua nchini kama yapendavyo.
 
Kwa hiyo na wewe umeshakubali this simple conspiracy theory bila hata kuipa thought kidogo, pole sana, ndio maana wapiga kura wetu ni rahisi kubadilishwa hata kwa kanga, I can understand!

as usual WRONG again!! acha politics na sera za "kufuata mdundiko"...........i hope umenielewa. Its complicated as it can get, think hard bro!! majority hapa hawapendi mafisadi, lakini ni independent thinkers na wanapenda ku-digest news na udaku kama unavyokuja.......for a long time, wewe upo kwenye wrong side of the tracks......goodluck!!.
 
Huu sio ujambazi wa kawaida, inavyoonyesha wametumwa.

Pole mhariri, kila la heri kwa safari yako ya India kwa ajili ya matibabu zaidi. Get well soon!!!!!!!!
 
Mkuu Mlalahoi,

Heshima mbele mkuu, unajua siku zote ninazipa heshima sana posts zako humu, isipokuwa sijawahi kuona ukitumia mabavu kupitisha hoja, Yaaaani matusi mazito kama kuwaita wananchi wazembe, wachovu wa weekend, na wanaotaka kuongeza idadi za posts hapa,
kwa sababu tu ya kuuliza kistaarabu iwapo kuna ukweli kwamba serikali n CCM inahusika na huuu uvamizi?

Maandishi yaliyo ukutani mnayoyaona some of you ambayo sis wengine hatuyaoni yako wapi hayo mkuu? Ndimara ninamfahamu sana amekuwa mbunge wa upinzani kwamuda hakumwagiwa acid, Slaa mwenyewe hajamwagiwa acid, Zitto hajamwagiwa acid, sasa iweje leo imwagiwe kwa waandishi tu?

Mimi kama ni fisadi, ninammwagia acid Zitto/Slaa wenye evidence, au waandishi wa habari ambao wanasubiri habari toka kwa Zitto na Slaa? I mean kama ni acid unaimwaga kwa chanzo cha evidence na sio messengers kina Ndimara, hii ishu ni nzito sana mkuu ni lazima tuichukulie serious sana kabla ya kuhukumu bila ushahidi maana in the end mambo kama haya yanaweza kuwa na influence kubwa sana kwa maamuzi ya kesi hiyo ya mafisadi, maana tukumbuke kuwa bado kuna muda mkubwa na wa kutosha kulingana na sheria zetu kwa mafisadi kwenda mahakamani, sasa maneno yasikyokuwa na uhakika kama haya yanaweza kuwapa nguvu hawa, maana kama ni acid unaimwaga kwa chanzo cha evidence na sio kwa muandishi tu wa habari, maana pia tujue kuwa kuna hili gazeti kuharibu biashara za magazeti mengine kwa kutoa habari nzito sana na hivyo kuuza kwa wingi kuliko magazeti ya establishment, kama kuna fats zaidi ziwekwe hapa jamani sio mabavu!

Mlalahoi, you are too big for this mkuu!

Field Marshal ES,

Kwanza napenda kumpa pole Ndugu Kubenea kwa masaibu yalompata, na namwombea kwa Mwenyezi Mungu apate nafuu haraka, aweze kurejea katika shughuli za kulijenga taifa letu na kutunza familia yake. Mie pia sijui aliyemuumiza ndugu Kubenea wala sina yeyote ninayemhisi, lakini sikubaliani na maandishi yako niliyonakili hapo juu, hasa hayo niliyoyawekea bold. Ni kwamba mtu anapopambana na anayemdhania ni adui yake huwa anaangalia pia gharama zinazohusika na mahali pa kumuumiza kwa urahisi. Kiswahili tunasema "kamba hukatikia pembamba". Hata simba anapowinda, huwa anamfuatilia yule ambaye ni rahisi kumkamata, na si lazima awe yule mnono! Hata kule Afrika kusini wakati akina Mandela wanapambana na ubaguzi, jeshi la Mandela la Umkhonto we Sizwe lilikuwa linafanya hujuma kwenye miundombinu kama reli, maofisi ya serikali nk, na ndio maana makaburu wakasema ANC kilikuwa kikundi cha kigaidi. ANC wangekuwa na fikra za kusema wapambane na chanzo (ati jeshi lenyewe la makaburu) kamwe wasingefanikiwa au ingechukua miaka mingi zaidi!. Hujuma ni mbinu pia katika mapambano. Kama ni kweli kuna watu walikuwa wanaogopa taarifa zao zisifike mahala na mfikishaji alikuwa Kubenea, sishangai wakimshughulikia yeye badala ya kukishughulikia chanzo, kwani inaweza kuwa kazi rahisi zaidi kumpata yeye kuliko hizo sources, labda yeye ni dhaifu kuliko hao sources (kamba hukatikia pembamba), au athari za kuipiga hiyo source (mfano retaliation) ni kubwa zaidi kuliko kumzima huyo, na pia hiyo inaweza kuwatisha messengers wengine wasipokee na kueneza taarifa kutoka kwa huyo source unayemsema, mwishowe na source mwenyewe atakosa chombo cha kupelekea taarifa zake.

Narudia, sijui aliyemuumiza Kubenea, lakini sipingi uwezekano wa kwamba kafanyiwa hujuma. Yeye kuwa messenger tu wa habari haitoshi kumkinga, mbele ya hao "maadui" zake anahesabika kama accomplice tu, kwa hiyo pia ni target. Waandishi wa habari wengi tu duniani wamedhurika na hata kuuawa katika mazingira kama hayo, na tukiamua kuitisha orodha tutaipata ndefu tu.
 
Alipohojiwa Kubenea Kutoka Kitandani Muhimbili Alisema Anaamini Moja Kwa Moja Tukio Hilo Linahusiana Na Hatua Ya Gazeti La Mwanahalisi Kuandika Kuhusiana Na Ufisadi
 
Kithuku kwa kuongezea,
ndo maana pia walipotaja nia ya kwenda mahakamani, gazeti la mwanahalisi lilikuwa mojawapo! Sasa haiwezekani kwamba hawana shida nalo wakati walisha tamka wazi wanalipeleka mahakamani!
 
Quote:-

"kina ES na wenginea mtakuwa mnakubaliana nasi kuwa tukio hili la Kubenea lina mkono wa mafisadi,na kwa kuwa mafisadi ni wana CCM basi ni CCM ndo wahusika wakubwa,simple logoc will tell you that.Unless you can bring someting else out of all this."

Mkuu sio mfisadi wote ni wana-CCM, na CCM has nothing to do na mafisadi, halafu ninaomba nikuambie wazi kuwa so far toka hii topic ianze GT ndiye peke yake ametoa hard evidence ya anachokisema, ninaweza kumpa some support kwa sababu wengine wote mmeshindwa kutoa angalau a hint kuhusiana na madai yenu kuwa serikali ya CCM au mafisadi ndio wanaohusika na huu uharamia,

Ninarudia tena so far ni GT peke yake ndiye anaye make a sense kwa kutoa angalau "Evidence" ku-back up theory yake, hebu na nyinyi toeni japo dataz kidogo, badala ya kuanza analysis over analysis, bila dataz, siamini 100% anayosema GT, lakini kama mjadala ukifungwa sasa theory yake inasimama tena kwa nguvu sana, kwamba Mwandishi alikuwa aki-play double stadard against the rules za uandishi, Mkuu Kithuku, lete facts tuacheni na analysis bila facts!

Please tunahitaji facts na sio itikadi na hisia, pia tunawaombea walioathirika kupona haraka warudi kutuamusha wananchi. Lakini ukisoma hapa chini GT makes a lot of sense na pia ana back-up theory yake na some "Evidence" ingawa siamini lakini angalau mnyonge mnyongeni lakini ninaichukulia hii chini as a fact unless mwingine aje naz tofauti, please enough of analysis tunahitaji facts!!
 
SAIDI KEBENEA tatizo lake siyo ku expose UBADHIRIFU bali tatizo lake ni njaa

Alienda kwa hao ambao kila kukicha anawaandika kwenye magazeti wakampa pesa za kumpooza mbona hakutoa kwenye gazeti kuwa alipewa RUSHWA?

Huyu mtu all of a sudden watu wanamwonea huruma lakini cha ajabu hakuna anyesema kuwa naye yuko kwenye payroll sema tatizo lake ni pale alipoambiwa apunguze eyey akaamua kuwa ataongeza kwa kisingizio hapati matangazo

walimtumia MSG kupitia gari lake hivyo yeye alishajua kuwa hana muda mrefu na zaidi angweka wazi kuwa hao wanaopinga CHANGES wanajaribu kumnyamazisha...akakaa kimya huku akiendelea kuvuta pesa sasa juzi kafarakana nao tena ndio yamemkuta haya na kusema ukweli jamaa hawataki kumwondoa kwani its not in anyone's interest kufanya hivyo

Nilimfananisha na Bhutto ambaye alijua nani wabaya wake lakini still akaamua kujiachia mpaka wakamwondoa kwa kesi ya SAIDI ni kuwa hawajataka kumwondoa lakini still ni nuisance kwa jamaa
 
Mwana Halisi washambuliwa




Saed Kubenea akiwa Muhimbili




na Happiness Katabazi



KATIKA tukio linaloweza kutafsiriwa kuwa jitihada za kutisha mhimili wa nne wa utawala, watumishi wawili wa gazeti la Mwana halisi, juzi walivamiwa na watu wasiojulikana, kutishwa, kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya.
Katika tukio hilo la aina yake, watu hao watatu, walizivamia ofisi za gazeti hilo, na kuwakuta Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers, kampuni inayomiliki gazeti hilo na jingine la Mseto, Saed Kubenea na Mshauri wa habari wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage, wakiwa katika kazi ya kuandaa gazeti.

Katika mashambulizi yaliyofuatia uvamizi huo, watu hao waliojihami kwa mapanga na rungu, waliwamwagia tindikali waandishi hao na kusababisha Kubenea kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni.

Tegambwage alijeruhiwa kwa panga wakati akipambana na wavamizi wawili.

Akizungumza na wanahabari waliofika kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika wodi ya Sewahaji namba 19, Kubenea alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 2:30 usiku.

Akizungumza kwa taabu, alisema watu watatu wakiwa na panga, sime, rungu na chupa iliyokuwa na tindikali waliwavamia ofisini hapo na kuwajeruhi.

Katika kile kinachoonyesha masikitiko makubwa, Kubenea alieleza kuwa hivi sasa amepoteza uwezo wa kuona na hana uhakika iwapo ataweza kuona tena baada ya matibabu.

Kubenea alisema analihusisha tukio hilo na vitisho ambavyo amekuwa akivipata mara kwa mara kupitia simu yake ya kiganjani kutoka kwa watu wasiowafahamika.

Mmoja wa ndugu wa Kubenea, alisoma moja ya ujumbe huo wa vitisho uliokuwa ukimweleza Kubenea asingeumaliza mwaka jana akiwa hai.

"Nina uhakika kabisa kwamba tukio hili linatokana na simu na ujumbe mfupi niliokuwa naupokea kutoka kwa watu wasiojulikana. Mara kadhaa nimekuwa nikitoa taarifa Polisi Oysterbay, lakini hadi nakumbwa na tukio hili watu hao hawajawahi kutiwa mikononi mwa polisi.

"Mungu akinisaidia nikaweza kuona na endapo polisi watafanikiwa kuwakamata watu hao nina uwezo wa kuwatambua, ila kwa sasa siwezi kuwatambua kwa kuwa ndiyo hivyo tena sioni," alisema Kubenea.

Alisema hivi sasa familia na jamaa zake wanafanya kila liwezekanalo kumpeleka nchini India kwa matibabu zaidi.

Alisema juzi saa 6:45 usiku, baada ya kufikishwa hospitalini hapo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow na Kamanda wa Upelelezi wa wilaya hiyo, Damas Kasabi, walikwenda kumjulia hali, na aliwaeleza kwamba tukio hilo analihusisha na vitisho hivyo na waliahidi kulishughulikia.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Duni Haji, ambaye alikuwepo hospitalini hapo, alisema tukio hilo ni kitisho kwa wanahabari, ili wasiendelee kufichua maovu.

"Wanahabari mpo vitani, wapiganaji wawili wamejeruhiwa… Kubenea ni mmoja wa vijana waliokuwa mstari wa mbele kuandika habari za ufisadi… hii ndiyo tabia ya dola, haitaki kukosolewa," alisema.

Wengine waliofika kumjulia hali Kubenea ni Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (CHADEMA), waandishi kutoka vyombo vya habari, ndugu, jamaa na wapenzi wa magazeti ya Mwanahalisi.

Naye Tegambwage, ambaye alijeruhiwa kichwani kwa panga katika tukio hilo, akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tegeta-Machakani, Mtaa wa Matumbini, alisema alipata jeraha hilo baada ya kukatwa na panga.

Akieleza tukio hilo, Tegambwage alisema wakiwa ofisi hapo na Kubenea, walisikia watu wakigonga mlango wakitaka wafungulie ndipo alipomtaka Kubenea akawafungulie.

"Kubenea alipofungua mlango watu hao walimtaka atoke nje, ndipo Kubenea alipofunga mlango, lakini watu hao walitumia nguvu kuufungua na kufanikiwa kuingia ndani na mmoja kati yao akamwambia Kubenea kwamba alikuwa amemfuata yeye na alikuwa akimtafuta kitambo," alisema Tegambwage.

Alisema mtu huyo alikuwa amebeba chupa yenye kemikali ambayo anadhani ni tindikali, alimmwagia usoni Kubenea. Alisema walimmwagia na yeye lakini macho yake yalisalimika kwa sababu alikuwa amevaa miwani hivyo kemikali hiyo kumwagikia puani na mdomoni.

Alisema walivyoingia, Kubenea wakati anapambana na mtu huyo, mtu mwingine alimrushia panga ambalo alilikwepa na mwingine alimrushia panga jingine ambalo alilipangua na kufanikiwa kuwakamata mashati watu hao wawili hadi kuanguka nao chini.

"Baada ya kuwashinda nguvu ndipo yule aliyekuwa anakabiliana na Kubenea akanipiga panga la kichwa ambapo nyama ilikuwa ikining'inia… wale wenzake wakavua mashati niliyokuwa nimeyashikilia, wakakimbia," alisema Tegambwage.

Alisema watu hao waliacha pia silaha zao, ikiwemo chupa iliyokuwa na tindikali.

Alisema baada ya watu hao kuondoka hawakuwa wakihisi maumivu, licha ya kuamua kwenda kupata huduma ya kwanza katika hospitali binafsi ya Dk. Mvungi iliyopo Kinondoni, ambako alishonwa nyuzi 15 kwenye jeraha alilolipata na wakati huo Kubenea alikuwa akiona kwa taabu.

Baadaye walishauriwa na madaktari kwenda Hospitali ya Muhimbili, ambapo yeye alipelekwa MOI, ambapo alipigwa X-ray na kuruhusiwa.

Tegambwage, ambaye ni mchambuzi mahiri wa mada kupitia vyombo vya habari, alisema anaamini tukio hilo ni mchezo mchafu unaochezwa na baadhi ya watu woga ambao inawezekana wameguswa na uandishi wa magazeti hayo, hivyo kuamua kutumia dhiki za vijana kutenda unyama wa kiwango kile.

"Ninachoelewa vijana wale hawana sababu ya kutujeruhi au kutaka kutuua, isipokuwa wametumwa kutekeleza matakwa ya watu wengine.

"Tendo hili limetokana na uandishi wa habari, hakuna sababu ya kukataa kuwa shujaa… wanahabari wote waendelee na mtindo huo huo, waandike," alisema Tegambwage.

Hata hivyo, alisema waliotumwa kutenda tukio hilo ndio wanaotetewa na vyombo vya habari na waliowatuma wanataka kuangamiza uhuru wa kila mmoja na si wanahabari peke yake.

Hii ni mara ya tatu kwa Kubenea kukumbwa na matatizo, kwani katikati ya mwaka jana watu wasiofahamika walichoma gari lake aina ya Suzuki Escudo.

Katika tukio la pili, akiwa nyumbani kwake Kinondoni akitembea kandokando mwa barabara, aligongwa na gari lisilofahamika na kuanguka chini na baada ya gari hilo kumgonga lilikimbia.

Naye Meneja Utalawa wa magazeti hayo, Yusuf Aboud, aliwaambia waandishi wa habari hospitali hapo kwamba mapema mwezi uliopita kijana mmoja alifika katika ofisi zao na kumuulizia Kubenea ambaye alimtaka atoke nje ya ofisi, kwani alikuwa ameleta habari.

Hata hivyo, Kubenea aligoma kutoka nje na kumtaka mwandishi wake, Iddy Mkwama, aende kuzungumza na kijana huyo.

"Pamoja na Iddy kwenda kumsikiliza kijana yule alisisitiza kumwona Kubenea, kwani alitaka kumweleza kuwa alikuwa kwenye kijiwe kimoja aliwasikia baadhi ya vijana wakipanga njama za kutaka kumdhuru," alisema Aboud.

"Baada ya kijana kusema hivyo, Iddy alirudi kumwita tena Kubenea na walipotoka nje walimuona kijana huyo akikimbia na kuingia kwenye gari aina baloon lililokuwa limebeba watu wengine watatu na kuondoka kwa kasi," alisema Aboud.

Katika hatua nyingine, Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Christopher Nyenyembe, alilaani tukio hilo, na kubainisha kuwa lina lengo la kuzika uhuru wa habari. Aliwataka waandishi wa habari na wanaharakati kote nchini kuungana kulaani kitendo hicho.

Wakati huo huo, Jukwaa la Wahariri leo limeitisha mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) kwa ajili ya kutoa tamko kuhusiana na tukio hilo.

news from Tanzania Daima
 
for a long time, wewe upo kwenye wrong side of the tracks......goodluck!!.

Heri yako mkuu uliyepo "on the right side of the track". Lakini ili wewe uonekane upo "on the right track" inabidi wengine tuwe "on the wrong side", vinginevyo nyie mliye on the right side hamtaonekana.
 
Quote:-

"kina ES na wenginea mtakuwa mnakubaliana nasi kuwa tukio hili la Kubenea lina mkono wa mafisadi,na kwa kuwa mafisadi ni wana CCM basi ni CCM ndo wahusika wakubwa,simple logoc will tell you that.Unless you can bring someting else out of all this."

Mkuu sio mfisadi wote ni wana-CCM, na CCM has nothing to do na mafisadi, halafu ninaomba nikuambie wazi kuwa so far toka hii topic ianze GT ndiye peke yake ametoa hard evidence ya anachokisema, ninaweza kumpa some support kwa sababu wengine wote mmeshindwa kutoa angalau a hint kuhusiana na madai yenu kuwa serikali ya CCM au mafisadi ndio wanaohusika na huu uharamia,
Ninarudia tena so far ni GT peke yake ndiye anaye make a sense kwa kutoa angalau "Evidence" ku-back up theory yake, hebu na nyinyi toeni japo dataz kidogo, badala ya kuanza analysis over analysis, bila dataz, siamini 100% anayosema GT, lakini kama mjadala ukifungwa sasa theory yake inasimama tena kwa nguvu sana, kwamba Mwandishi alikuwa aki-play double stadard against the rules za uandishi, Mkuu Kithuku, lete facts tuacheni na analysis bila facts!

Please tunahitaji facts na sio itikadi na hisia, pia tunawaombea walioathirika kupona haraka warudi kutuamusha wananchi. Lakini ukisoma hapa chini GT makes a lot of sense na pia ana back-up theory yake na some "Evidence" ingawa siamini lakini angalau mnyonge mnyongeni lakini ninaichukulia hii chini as a fact unless mwingine aje naz tofauti, please enough of analysis tunahitaji facts!!


Kinachokufanya useme GT katoa "hard evidence" ni nini? So far yeye kaja na theory nyingine tu ya possible reasons za ndugu yetu kupigwa mapanga na kumwagiwa tindikali. Nasema hivyo kwasababu hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kuwa alikuwa anapokea pesa toka kwa hao mafisadi unless mzee unajua zaidi ya haya yanayosemwa hapa.
 
Back
Top Bottom