Mhariri Mtendaji wa Gazeti la MwanaHALISI, Saed Kubenea avamiwa na kumwagiwa tindikali akiwa ofisini kwake

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kuna habari kwamba watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemvamia mhariri na mmiliki wa Mwanahalisi, Saed Kubena na kumkata kwa mapanga. Habari zaidi baadaye.

===========

Saed 1.JPG
Saed 3.JPG

Mwanahabari Saed Kubenea akiwa hospitali baada ya kumwagiwa tindikali

Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwana Halisi na Mseto, Said Kubenea, amevamiwa ofisini kwake na watu wenye silaha na kumwagiwa tindikali usoni na kusababisha apoteze uwezo wa kuona.

Katika tukio hilo, vile vile mshauri na Mhariri wa Habari wa magazeti hayo, Ndimara Tegambwage, alijeruhiwa na kushonwa nyuzi 15 kichwani baada ya watu hao kumkatakata kwa mapanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jamal Rwambow, ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza kwenda kumjulia hali Kubenea hospitalini juzi usiku, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Hadi jana mchana, Kubenea (37) ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu kizito karibu na jicho la kulia, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku taratibu za kumpeleka nchini India kwa matibabu zaidi zikiendelea kufanywa kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Tukio hilo limetokea baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto gari lake na kisha kumpigia simu na kumtumia ujumbe wa maandishi wa simu (sms) wakitishia kumuua.

Akisimulia mkasa wa kushambuliwa na kumwagiwa tindikali hospitalini hapo jana, Kubenea ambaye anaongea kwa tabu kutokana kuelemewa na maumivu, alisema wakiwa ofisini kwenye saa 3:00 za usiku wa kuamkia jana pamoja na Ndimara ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia masuala ya Kijamii la IDEA na vijana wake watatu, watu watatu walifika na gari na kugonga mlango.

Kubenea alisema baada ya mlango kugongwa, alikwenda na kuufungua ili kuwatambua wageni waliokuwa wakibisha hodi.

Alisema baada ya kufungua mlango, watu wale walimwambia kuwa ‘Tunakutaka wewe’ na baada ya kuwambia hivyo, wakamwamuru kukaa chini na kuanza kutoa mapanga, visu na nondo.

“Nilipotaka kufunga mlango, wakawahi kuingia ndani. Ndimara ambaye alikuwa anasafiri leo (jana) kwenda Darfur, Sudan, akawauliza kuna nini? Kuuliza hivyo, wakamvamia Ndimara na kuanza kumshambulia kwa mapanga,” alisema Kubenea.

Alisema hali hiyo ilizua mapambano makali ofisini kati yao na watu hao yaliyodumu kwa dakika kadhaa kabla ya watu hao kuzidiwa nguvu na kukimbia.

Kubenea alisema tukio la kumwagiwa tindikali lilikuja baada ya mmoja wa watu hao kuangusha chini panga alilokuwa akilitumia na yeye (Kubenea) kuliokota na kutaka kulitumia katika mapambano hayo.

“Baada ya mapambano kuchukua kama dakika mbili hivi, panga la mmoja wao likaanguka chini. Nikaliokota, nilipotaka kulitumia, ndio wakanimwagia tindikali,” alisema Kubenea.

Hata hivyo, alisema hakukata tamaa, badala yake, alijitahidi na kuingia kwenye moja ya vyumba vya ofisi hiyo kutafuta silaha kwa ajili ya kukabiliana na watu hao na kufanikiwa kupata chupa lakini aliporudi kwa ajili ya kuendelea na mapambano, alikuta watu hao wametoka nje ambako waliendelea kupambana na Ndimara.

Alisema baada ya kudhibitiwa na Ndimara huko nje, watu hao walijaribu kummwagia tindikali usoni, lakini haikumuathiri kwa vile alivaa miwani.

“Ndimara alinisaidia sana. Kwani kama ningekuwa peke yangu, wangeniua au kuniteka,” alisema Kubenea.

Kubenea alisema baada ya hali kutulia, walikodi teksi na kukimbizwa katika hospitali binafsi ya Dk Mvungi iliyoko Kinondoni ambako walipatiwa huduma ya kwanza kabla ya usiku huo kuhamishiwa Muhimbili.

Alisema madaktari wanaomtibu wameshauri akatibiwe haraka nchini India kutokana na kutojua aina ya tindikali iliyotumika kumdhuru.

“Madaktari wanasema ingekuwa ni tindikali ya kawaida, ingekuwa rahisi kwao kunitibu, lakini hii inaweza kuendelea kutafuna kwa muda mrefu na kuathiri macho kabisa. Hivyo, wameshauri kama upo uwezekano ni vizuri nikaenda India haraka, ikiwezekana kesho (leo),” alisema Kubenea ambaye anaona kwa tabu.

Alisema anaamini watu waliotekeleza tukio hilo, wametumwa kumshughulikia kutokana na waliowatuma kuchukizwa na msimamo wake wa kuweka hadharani maovu ya baadhi ya vigogo serikalini kupitia magazeti yake.

Kubenea alisema dhana hiyo inapewa nguvu kutokana na kuwa tangu Juni 13, mwaka jana, amekuwa akitumiwa sms za vitisho ambapo miezi miwili badaye watu wasiojulikana walichoma moto gari lake na kutamba kupitia sms kuwa wametimiza jambo hilo na kwamba kilichobaki ni kuuondoa uhai wake.

Alisema baada gari lake kuchomwa moto, aliendelea kupokea sms zinazomweleza kuwa:

“Kiburi chako kitakuponza, jiandae kwa shughuli nzito itakayokupata”, “Kifo chako kitakuwa cha aina yake, mzoga wako hautaonekana”, “Dawa ya kushughulikia maiti kama wewe imepatikana, jiandae”, “Maandalizi ya mauti yako yameiva, watangazie mabwana zako wanaokutuma. Unanuka uvundo wa kufa”, “Vuta pumzi zako za mwisho, hatuko mbali, yamebaki masaa machache kabla hatujakupeleka panapostahili”.

Alisema awali, alidhani watu wanaomtumia sms hizo ni waandishi wenzake wanamtania. Lakini kadri matukio ya kutisha yalivyozidi kutokea, akaamini kuwa watu hao ni maadui zake.

Mamia ya watu wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Juma Duni Haji na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Halima Mdee, waliokwenda kumjulia hali Kubenea, jana asubuhi walifurika katika Wodi ya Sewahaji chumba namba 19 alikolazwa mwandishi huyo kabla ya kuhamishiwa katika chumba maalum hospitalini hapo.

Akizungumza hospitalini hapo jana, Duni alisema Kubenea amekuwa mhanga wa kusimamia ukweli na kuwashutumu waliomtishia kumuua kwa sms.

Kamanda Rwambow, alisema polisi wanaendelea na upelelezi na kwamba leo watatoa taarifa rasmi kuhusiana na tukio hilo.

PIA, SOMA:
VISA DHIDI YA WANAHABARI WENGINE WA TANZANIA:
 
Oooh, uwiii, i hope hawakuchukua roho yake! Mpe pole sana utakapoenda kumjulia hali.
 
DUH hizi habari zikoje? Maana Halisi hua anakuja na data za mashaka. VP halisi ile kesi yako na TRA kule ARUSHA imeisha maana nshasahau kabisa.
 
mungu amlaze mahala pema peponi

bwana alitoa na bwana ametwaa

Mmmmmh Mtu Pwani ndio Lugha gani tena hiyo!!.Huyu Bwana Mzima mbona unaandika Lugha Ngumu,ina maana una Taarifa Tofauti na hii aloandika Bwana Halisi?Waungwana hatupo hivyo Mkuu umetoka Mrima nini?
 
Mmmmmh Mtu Pwani ndio Lugha gani tena hiyo!!.Huyu Bwana Mzima mbona unaandika Lugha Ngumu,ina maana una Taarifa Tofauti na hii aloandika Bwana Halisi?Waungwana hatupo hivyo Mkuu umetoka Mrima nini?

Alaaa mkuu kumbe nimeelewa vibaya kipengele sio, samahanini kwa uelewa mnayaufu.

ila sitoki mrima mkuu mie nnatoka kule kwenye kisiwa cha viungo.

kama yuko hai nnampa pole mungu amjaalie uzima wa haraka ili atuhabarishe
 
DUH hizi habari zikoje? maana Halisi hua anakuja na data za mashaka...VP halisi ile kesi yako na TRA kule ARUSHA imeisha maana nshasahau kabisa,...

Anayekuja na data za mashaka(controversial) nadhani ni Hasara. Namwiminia sana Halisi(Genuine).

Pole bwana mhariri. Wish you quick recovery.
 
mungu amlaze mahala pema peponi

bwana alitoa na bwana ametwaa

Hii Kali kweli, Mtu wa Pwani!! unamtanguliza mwenzako kwenye hukumu ya mwenyezi Mungu kirahisi hivyo? Ama unataka kutuambia unafahamu ama ulishiriki kuchapa mapanga na unauhakika hata pona? Pole pole mkuu.
 
DUH hizi habari zikoje? maana Halisi hua anakuja na data za mashaka...VP halisi ile kesi yako na TRA kule ARUSHA imeisha maana nshasahau kabisa,...

Chuma,

Angalia facts zako maana Halisi ni katika watu wachache sana hapa JF ambao wakisema jambo jua kuna 99% kwamba kuna ukweli.

Pole kwa aliyeumia na mungu amsaidie ili apate nafuu.
 
Pole aliye uliye umizwa mungu akujalie kupona haraka.

Ila wasi wasi wangu, ni ujambazi tu wakawaida? Ama inahusiana na cheo chako cha kuwa mhariri wa gazeti la mwana Halisi, ambalo ni kati ya magezeti yanayo ongoza kwa kuita a spade.
 
Namtakia Mhariri kupona mapema.

Nani kafanya ujambazi huu? Huu ni ujambazi au njama za kuyafunga mdomo magazeti?

Sikujua watu wa Mrima ndiyo hawajui Kiswahili, nilifikiri watu wa Mrima wanajua kiswahili mpaka kuwa na lahaja yao ya Kiswahili Mrima kama ilivyo kwa Kiswahili Unguja.
 
Sasa wale mafisadi baada ya kugundua kwamba wameshindwa kwenda Mahakamani na huenda kuna mambo yatazuka yameamua kampeni ya kuwaondoa wale wote walio chapisha majina yao. OK zile za Kenya sasa zinakuja Tanzania na mtaishia kusema majambazi siyo?
 
Taarifa rasmi ni kwamba watu watatu wasiojulikana wamevamia ofisi za Mwanahalisi zilizopo Kinondoni, Dar es Salaam na kupambana na Mshauri wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage na baadaye Saed Kubenea, ambaye baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani alimwagiwa acid usoni, iliyomwingia mdomoni na machoni.

Ndimara amekatwa mapanga kichwani, shingoni na mgongoni, lakini baada ya kushonwa nyuzi 15 kwa Dr Mvungi kinondoni na baadae yakupaatiwa matibabu zaidi Muhimbili, ameruhusiwa lakini Kubenea amelazwa kutokanan na madhara katika macho yake. Anaona kwa shida na tumuombee Mungu aweze kuona na kuendelea na majukumu yake magumu.
 
Taarifa rasmi ni kwamba watu watatu wasiojulikana wamevamia ofisi za Mwanahalisi zilizopo Kinondoni, Dar es Salaam na kupambana na Mshauri wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage na baadaye Saed Kubenea, ambaye baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani alimwagiwa acid usoni, iliyomwingia mdomoni na machoni.

Ndimara amekatwa mapanga kichwani, shingoni na mgongoni, lakini baada ya kushonwa nyuzi 15 kwa Dr Mvungi kinondoni na baadae yakupaatiwa matibabu zaidi Muhimbili, ameruhusiwa lakini Kubenea amelazwa kutokanan na madhara katika macho yake. Anaona kwa shida na tumuombee Mungu aweze kuona na kuendelea na majukumu yake magumu.
Halisi,
Thanks Mkuu- we all wish them quick recovery- yaonekana kuna ill motives associated na vitendo vya ufisadi kutoka ktk hilo gazeti ambalo ndo limeanza tu siku za karibuni!

Muhimu ni kutokata tamaa- na kutambua hii ni vita of social, economic and political justice of our future Tanzania!

Aluta continue!
 
Ni wakina mvi hao (an educated hunch), this might signal the beginning of the end of mafisadi hao. Mwanahalisi ndio wako mstari wa mbele kabisa kuanika uchafu wao. Pole sana waioathirika. Itabidi waondoe mamilioni ya watu kabla ya kudhani siri zao hazitafichuka wale.
 
Kuna habari kwamba watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemvamia mhariri na mmiliki wa Mwanahalisi, Saed Kubena na kumkata kwa mapanga. Habari zaidi baadaye

huyu naye alikuwa hasikii alishapelekewa taarifa zamani lakini wapiiii yuko ka Benazir Bhutto vilee
 
Mm sishangai. Maana wameongoza kuwashambulia wakubwa. Sasa mnafikiri hao majambazi wametumwa na kuna motive za kisiasa katika mashambulizi hayo. Wakati wanawashambulia hawakusema chochote? Jamani Tz ndiyo twaelekea nchi jirani?

Hiyo sio dawa. Unafikiri mbele ya kamati ya bunge ya Mwakyembe juu ya Richmond si mambo yatawekwa wazi? Sio hayo kaeni mkao wa matazamio siku chache zijazo kuna mambo yataibuliwa kutoka Manispaa mmojawapo za mkoa wa Mwanza au Dar ambayo wengi mtashangaa mtakapoona vigogo wanashinikizwa kuachia ngazi. Sisemi mengi
 
Masikini rafiki yangu Kubenea!!!!

Kulikoni jamani kafanya nini tena, bahati mbaya gazeti lake haliko online, mkipata sababu tujulisheni: who is behind the move...
 
Back
Top Bottom