Mhandisi Leo Magomba: Wanaotumia internet ya uhakika Afrika ni asilimia 38 ya watumiaji wote, hili ni pengo kubwa

Mhandisi Leo Magomba: Wanaotumia internet ya uhakika Afrika ni asilimia 38 ya watumiaji wote, hili ni pengo kubwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mhandisi wa Miundombinu ya Mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Leo Magomba amesema kwamba katika bara la Afrika wanaotumia internet ya uhakika ni asilimia 38 kati ya watumiaji wote, ambapo amedai kuwa zinahitajika juhudi za pamoja kuchochea ongezeko.

IMG_4941.jpeg
"Ni asilimia 38 pekee ya Afrika wanaotumia intaneti ya uhakika, huku kwa dunia nzima ni asilimia 68. Hili inaonyesha pengo kubwa,” alisema Mhandisi Magomba.

Aidha ameeleza kuwa katika Mkutano wa 14 wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF) utakaofanyika kuanzia Mei 29 hadi 31, 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Tanzania akiwa mwenyeji, wadau wanatarajia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo yanayoweza kuchochea ongezeko hilo.

IMG_4940.jpeg
Ambapo amebainisha mambo kadhaa yatayojadiliwa. Namna ya kuongeza upatikanaji wa intaneti kwa wote, kuondoa tofauti ya matumizi kati ya mijini na vijijini, pamoja na kuimarisha usalama wa mtandao pamoja kujadili suala la teknolojia ya Akili Mnemba (AI)

Ameyasema hayo Mei 22, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu mchakato wa maandalizi ya Mkutano huo.
 
Back
Top Bottom