Mhadhiri Bashir Ally (UDSM) Atafutiwe Jimbo!

Mhadhiri Bashir Ally (UDSM) Atafutiwe Jimbo!

Nchi hii watu wanasoma ili wawe wanasiasa? Mtu anakuwa doctor au prof anaacha kuhudumia wananchi kwa kufanya research ili kuweka mazingira mazuri ya utafit anakimbulia kazi ambazo hata Lusinde darasa la 7 anafanya na ofcpz hawana tofauti ktk output zao.

Why why why my country? Prof Anna Tiba, Mwandosya, Hemed Msolla et al. Yani uprof wenu mnaiexercise bungeni ambako hata non-elite anaweza perform?

Sasa kijana kama huyu anataka kuzamia huko nae, mweeee kazi iko. Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za nje kidogo, ukichunguza mabunge mengi wazee ndio wako huko wkt ss vijana ndio option yenye ulaji tunaiona. Ka
MzLendo si uanzishe kitu ili kusaidia watu wengi kwa kutumia ujuzi wako wa darasani?

Inakatisha tamaa wasomi kukimbilia dodoma kwa kweli na vyuoi wanabaki ma-TA na Ass Lecturers

akienda kwenye siasa tu kwishinei. Watamzima
 
Hapa ndipo tunapokosea akiwa mwanasiasa atakuwa muhanga wa madhira mengi na matindikali ya kijana mpu.mbavu mwigulu, bora abaki huko jikoni...ukielimisha msomi mmoja ni ukombozi wa wanyonge 1000*
 
Nchi hii watu wanasoma ili wawe wanasiasa? Mtu anakuwa doctor au prof anaacha kuhudumia wananchi kwa kufanya research ili kuweka mazingira mazuri ya utafit anakimbulia kazi ambazo hata Lusinde darasa la 7 anafanya na ofcpz hawana tofauti ktk output zao.

Why why why my country? Prof Anna Tiba, Mwandosya, Hemed Msolla et al. Yani uprof wenu mnaiexercise bungeni ambako hata non-elite anaweza perform?

Sasa kijana kama huyu anataka kuzamia huko nae, mweeee kazi iko. Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za nje kidogo, ukichunguza mabunge mengi wazee ndio wako huko wkt ss vijana ndio option yenye ulaji tunaiona. Ka
MzLendo si uanzishe kitu ili kusaidia watu wengi kwa kutumia ujuzi wako wa darasani?

Inakatisha tamaa wasomi kukimbilia dodoma kwa kweli na vyuoi wanabaki ma-TA na Ass Lecturers

Kaka.! Umenena vyema.Binafsi naona kiza kinene mbele,sioni matumaini hata kidogo.Kila mhitim wa chuo kikuu leo anataka kuwa mwanasiasa,ni aibu sana japo baadh ya vijana wanaona ni fasion.
 
Namjua tangu mwaka 1997, alikuwa anakaa Hall IV na mpemba mmoja anaitwa Salum. Huyu jamaa ni mzinzi sana, hafai hata kidogo!

Hiyo ni personal issue ongelea mada iliyopo, tutajuaje kama na wewe ni msafi? Usiwe mkubwa jiwe mkuu.
 
Kaanza vizuri tu kalelewa na hayatiProf H.Othman then akaenda kwa Prof Shivji lakini pia hawezi kuwa nje ya scope za kina Marhum Prof Chachage na Dr Mwami kwa waliopita hilo jengo refu hapo mnaelewa kiwa ni zao la wengi ila hao waliomtangulia hawajawahi kuwa na silka za madaraka na impact zao mpaka leo mwangwi upo na waliyafanya haya kutokea hapo hapo UDSM

Mkuu Omutwale huyu abaki afuate nyayo za watangulizi wake maaaana hata akikiesha na kuelekeza huko mjengoni mwisho ni wanaoafiki..!!!!!!!(though kugombea ni haki yake)
 
kwann mkiona majina ya kiislam roho zenu zinawajaa chuki, husda, fitna na upumbavu? Mnadhani mnayofundishwa huko makanisani na akina slaa hatuyajui? Hii nchi siyo ya kanisa wala ya wakristo peke yao wala sio ya waislam peke yao. Ndio chuki mliyonayo kwa kikwete kisa dini yake. Mtakufa km mimbwa koko na chadema yenu ya kiliberali

Mkuu, unaonyesha jinsi usivyo jiamini swala la udini linatoka wapi hapa, unajaziba ya nini au ukweli unakuuma? Jitahidi kujibu hoja bila jaziba yoyote watu kama ninyi ndo mnaoendekeza udini. Binadamu aliye na akili hatukani ovyo anayefanya hivyo huwa hana akili bali ana ubongo tu ambao hata mnyama anao.
 
Nchi hii watu wanasoma ili wawe wanasiasa? Mtu anakuwa doctor au prof anaacha kuhudumia wananchi kwa kufanya research ili kuweka mazingira mazuri ya utafit anakimbulia kazi ambazo hata Lusinde darasa la 7 anafanya na ofcpz hawana tofauti ktk output zao.

Why why why my country? Prof Anna Tiba, Mwandosya, Hemed Msolla et al. Yani uprof wenu mnaiexercise bungeni ambako hata non-elite anaweza perform?

Sasa kijana kama huyu anataka kuzamia huko nae, mweeee kazi iko. Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za nje kidogo, ukichunguza mabunge mengi wazee ndio wako huko wkt ss vijana ndio option yenye ulaji tunaiona. Ka
MzLendo si uanzishe kitu ili kusaidia watu wengi kwa kutumia ujuzi wako wa darasani?

Inakatisha tamaa wasomi kukimbilia dodoma kwa kweli na vyuoi wanabaki ma-TA na Ass Lecturers

Point tupu hizi mdau maana kazi ya wasomi ni kutoa ushauri na kutusaidia sie wananchi shuleless kwa kutusimamia lakini tatizo letu kila mtu mwenye mchango mzuri wa mawazo utasikia agombee tutampa kura kumbe kuna wengine wanafaa kukaa pembeni na kufanya observation na kutoa ushauri kwani kinachotakiwa ni uwazi kati ya viongozi na wananchi. Mfano mzuri mbona zamani nchi ilikuwa ina wasiasa wa kawaida na bado ilikuwa inakwenda na viongozi walikuwa wanafanya maamuzi magumu bila woga.

Tuache mtindo wa kuchagua kiongozi kwa kuangalia uwezo wa kumudu mijadala kwani mtu anaweza akawa fit nje ya uongozi kuliko anapokuwa ndani maana mwisho wa siku hata awe na hoja nzuri vipi hufika wakati inaamuliwa kwa kusema "walioafiki waseme NDIOOOO"
 
Wanasiasa watu wa ajabu sana,wao wakiona kitu kizuri tu wanataka kukitumia kwa manufaa yao.

Na hapa ndipo siku zote tunakosea kwa kufikiri eti mtaalamu/msomi fulani atakuwa bora zaidi
akiwa mwanasiasa.

Na wasomi/wataalamu nao wamebeba dhana ya kwamba eti mojawapo ya kukubalika/kupendwa
au kupanda cheo kitaalum ni lazima wao kuwa wanasiasa kwa kuchaguliwa au kuteuliwa.

Ni vema tukatenganisha elimu na siasa,kwani panapo siasa pana porojo na panapo elimu pana
maarifa.

Kama yeye mwenyewe anadhani kwamba siasa ni kitu chake kikubwa kimalengo ni vema akajipambanua
mapema kimsimamo,vinginevyo ni bora akawa mojawapo ya wanazuoni wa akiba tunaowategemea
sasa na siku za zijazo.
 
Hiyo ni personal issue ongelea mada iliyopo, tutajuaje kama na wewe ni msafi? Usiwe mkubwa jiwe mkuu.

I vehemently disagree with your assertion that " hiyo ni personal issue." If one wants to run for public office, it's important for voters to know his weakness and strength, and off course, that includes personal issues. Voters need to know these people inside out before electing them. We have to scrutinize those who are running for office in order to sort them out. We don't want leaders who can easily be manipulated or blackmailed. As far as I am concern, Bashir hafai hata kidogo.
 
Mkuu upo sahihi lakini kwa hoja ya stata mzuka akimjibu Rufiji nadhani hapa kuna haja ya kuangalia at that time 1997 alikuwa kwenye age ipi pia na historia ya wanachuo wetu wawapo chuoni ikoje kuhusiana na mahusiano, hoja nadhani je hiyo tabia anayo mpaka sasa akiwa mtu mzima mwenye majukumu kamili? kama anayo mpaka sasa kiukweli nakuunga mkono maana vijana wengi at the age of 20s huwa vipanga na wengine ni wa kisirisiri kutokana na factors mbalimbali za kibaiolojia ambapo wengine ndio huendelea nayo na kuwa tabia mpaka wanapokabidhiwa majukumu
 
Last edited by a moderator:
Si kila Mhadhiri wa UDSM ni PHD holder....

Bashiru Ally sio Daktari wa Falsafa....Sio Dk. Kama unavyodhani...

Mkuu ahasante kwa taarifa, huyu jamaa ni wa kitambo pale UD, mimi nikajua tayari atakuwa ameshakwaa PhD tayari.
 
Ni jembe hata mimi namkubali sana!
bashiru.jpg

Bwana Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Bwana Bashiru Ally ni miongoni mwa vijana waliofuzu makuzi ya kitaaluma na kijamii kutoka kwa watu wanaoheshimika na historia ya nchi hii; ile ambayo haikuhifadhiwa rasmi vitabuni. Enzi zetu tukiwa masomoni Bwana Bashir na Omar Ilyas ni miongoni mwa vijana waliopendwa na kujiweka karibu na Marehemu Prof. Haroub Othman (former VC-UDSM). Hali halisi inajidhirisha kuwa Bwana Bashir ndiye aliyefuzu kuyashika vema mafunzo na weledi wa Prof. Haroub Othman. Baada ya kuachana kitambo, miaka ya hivi karibuni nimekuwa nikimsikiliza, kumuona au kumsoma kupitia vyombo vya habari. Mara nyingine kwa bahati tumewahi kukutana kwenye mikutano.

Hivi majuzi Bwana Bashiru alishiriki mjadala wa DW juu ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya ugaidi. Msimamo na utetezi wa mtazamo wake juu ya jinsi vita hii inavyopiganwa nakubaliana nao kwa asilimia 100—“Mbinu zinazotumika kupambana na ugaidi ni za kigaidi na hivyo zinazidisha ugaidi”

Bwana Bashiru ni mtu aliyejipambanua kuwa na msimamo usiyoyumba katika masuala ya Kitaifa na yale yote anayoyaamini baada ya kuyatafiti kwa kina. Si mtu wa papara na kuropoka. Hisia zake juu ya jambo lolote hazijathibitika kufungamana na imani au itikadi. Kiufupi ni mtu-huru, mwenye fikra chanya kwa mustakhabari wa jambo lolote analoshiriki kulitenda au kulipendekeza. Tuna uhaba wa watu wenye sifa hizi katika utungaji wa sera na kuisimamia serikali. Kumuacha aendelee kuongea na makaratasi au kuwasilisha hoja zake kwa Power Point mikutanoni na kisha akitoka ukumbini hakuna wa kuzitekeleza ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wa nchi hii.

Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. Binafsi sijali atajiunga na CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, n.k ilimradi tu asijiunge na ccm, mahali ambako mawazo mapya na utendaji ni dhambi. Akitaka Jimbo nitamchagulia Bukoba Vijijini na nitakuwa tayari kuanza kumpigia kampeni. Naamini maeneo yenye wapiga kura wengi kama Ibwera na Katoro hatutakuwa nahaja kabisa ya kupita kupiga kampeni.

Eid Mubraak!

Cc: FaizaFoxy, Ritz, omar Ilyas, njiwa, Nivea
 
Kwanza so kijana bali ni mtu mzima maana hayuko under 40. Anaweza kuwa kiongozi mzuri na anaweza kujifunza akawa mwanasiasa mzuri tu. Kitu kimoja kinabaki cha kujiuliza katika idara hii ya akina REDET (Prof Mukandara), Benson Bana, Bashiru Ally n.k utaona mwenyewe. Pili alishawahi kugombea awe rais wa DARUSO enzi zake akiwa hapo Mlimani lkn akafanyia kampeni za kupata kura katika nyumba moja (sina hakika kama ni ya ibada) ila iko maarufu sana hapo Dar maeneo ya Mwembe Chai. Sidhani kama ni maeneo tofauti sana na suala la Prof Bernadetta la Mwembechai Saga... kwa hiyo fikiri vema na mwisho mambo ya siasa ni yake mwenyewe so ya kwetu sisi.
 
Kwa taarifa yenu kila kikao cha Bunge kinapoanza, Bashiru huwa 'anatoweka' UDSM
 
Kwa mtazamo wangu bado hajaiva vya kutosha kuweza kujitosa kwenye majukwaa ya kupakana matope. Ajenge misingi imara kwanza ya kuaminika ili ajipambanue yupo mlengo gani. Maana kama wengine walivyosema anaonekana wakati mwingine kama anaegemea kwenye wigo wa kidini zaidi.

Ajaribu kufuta dhana hizo na nyinginezo kwenye vichwa vya watu, vinginevyo ni mwanasiasa chipukizi mzuri tu.
 
Dr. Bashiru alishindwa uchaguzi wa DARUSO mwaka fulani alipogombea uraisi dhidi ya Bw. Maimu kutoka kitivo cha uhandisi ambaye alishinda uraisi. Historia ina kawaida ya kujirudia, kama akigombea ubunge si ajabu akaambulia patupu hata kama ana uwezo mkubwa wa kiuongozi.
 
Mi natoka Bukoba vijijini,kwa huko hawezi kabisa kupita kwani watu waliisha msahau,tangu ajiunge na chuo kikuu hajawahi hata siku moja kurudi kijijini kuwajulia hali aliowaacha,hiyo ni sifa yake moja kuu,amezama Dar es Salaam.Sina uhakika kama ukweni kwake hapo Kemondo nako aliisha wahi kwenda.
 
Back
Top Bottom