Bwana Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Bwana Bashiru Ally ni miongoni mwa vijana waliofuzu makuzi ya kitaaluma na kijamii kutoka kwa watu wanaoheshimika na historia ya nchi hii; ile ambayo haikuhifadhiwa rasmi vitabuni. Enzi zetu tukiwa masomoni Bwana Bashir na Omar Ilyas ni miongoni mwa vijana waliopendwa na kujiweka karibu na Marehemu Prof. Haroub Othman (former VC-UDSM). Hali halisi inajidhirisha kuwa Bwana Bashir ndiye aliyefuzu kuyashika vema mafunzo na weledi wa Prof. Haroub Othman. Baada ya kuachana kitambo, miaka ya hivi karibuni nimekuwa nikimsikiliza, kumuona au kumsoma kupitia vyombo vya habari. Mara nyingine kwa bahati tumewahi kukutana kwenye mikutano.
Hivi majuzi Bwana Bashiru alishiriki mjadala wa DW juu ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya ugaidi. Msimamo na utetezi wa mtazamo wake juu ya jinsi vita hii inavyopiganwa nakubaliana nao kwa asilimia 100-"Mbinu zinazotumika kupambana na ugaidi ni za kigaidi na hivyo zinazidisha ugaidi"
Bwana Bashiru ni mtu aliyejipambanua kuwa na msimamo usiyoyumba katika masuala ya Kitaifa na yale yote anayoyaamini baada ya kuyatafiti kwa kina. Si mtu wa papara na kuropoka. Hisia zake juu ya jambo lolote hazijathibitika kufungamana na imani au itikadi. Kiufupi ni mtu-huru, mwenye fikra chanya kwa mustakhabari wa jambo lolote analoshiriki kulitenda au kulipendekeza. Tuna uhaba wa watu wenye sifa hizi katika utungaji wa sera na kuisimamia serikali. Kumuacha aendelee kuongea na makaratasi au kuwasilisha hoja zake kwa Power Point mikutanoni na kisha akitoka ukumbini hakuna wa kuzitekeleza ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wa nchi hii.
Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. Binafsi sijali atajiunga na CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, n.k ilimradi tu asijiunge na ccm, mahali ambako mawazo mapya na utendaji ni dhambi. Akitaka Jimbo nitamchagulia Bukoba Vijijini na nitakuwa tayari kuanza kumpigia kampeni. Naamini maeneo yenye wapiga kura wengi kama Ibwera na Katoro hatutakuwa nahaja kabisa ya kupita kupiga kampeni.
Eid Mubraak!
Cc:
FaizaFoxy,
Ritz,
omar Ilyas,
njiwa,
Nivea