Mhadhiri Bashir Ally (UDSM) Atafutiwe Jimbo!

Ni mwl mzuri sana ktk ufundishaji kama ilivyo kwa dr bana ila kwenye mijadala hayuko objective sana.
Hayupo objective kwa vile sio mwalimu mzuri,ila ni mazao ya harakati za makundi ya akina Haroub othman na wengine pale udsm ktk kampeni zilizofichwa ktk ujamaa.
 
bashiru.jpg

Bwana Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Bwana Bashiru Ally ni miongoni mwa vijana waliofuzu makuzi ya kitaaluma na kijamii kutoka kwa watu wanaoheshimika na historia ya nchi hii; ile ambayo haikuhifadhiwa rasmi vitabuni. Enzi zetu tukiwa masomoni Bwana Bashir na Omar Ilyas ni miongoni mwa vijana waliopendwa na kujiweka karibu na Marehemu Prof. Haroub Othman (former VC-UDSM). Hali halisi inajidhirisha kuwa Bwana Bashir ndiye aliyefuzu kuyashika vema mafunzo na weledi wa Prof. Haroub Othman. Baada ya kuachana kitambo, miaka ya hivi karibuni nimekuwa nikimsikiliza, kumuona au kumsoma kupitia vyombo vya habari. Mara nyingine kwa bahati tumewahi kukutana kwenye mikutano.

Hivi majuzi Bwana Bashiru alishiriki mjadala wa DW juu ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya ugaidi. Msimamo na utetezi wa mtazamo wake juu ya jinsi vita hii inavyopiganwa nakubaliana nao kwa asilimia 100-"Mbinu zinazotumika kupambana na ugaidi ni za kigaidi na hivyo zinazidisha ugaidi"

Bwana Bashiru ni mtu aliyejipambanua kuwa na msimamo usiyoyumba katika masuala ya Kitaifa na yale yote anayoyaamini baada ya kuyatafiti kwa kina. Si mtu wa papara na kuropoka. Hisia zake juu ya jambo lolote hazijathibitika kufungamana na imani au itikadi. Kiufupi ni mtu-huru, mwenye fikra chanya kwa mustakhabari wa jambo lolote analoshiriki kulitenda au kulipendekeza. Tuna uhaba wa watu wenye sifa hizi katika utungaji wa sera na kuisimamia serikali. Kumuacha aendelee kuongea na makaratasi au kuwasilisha hoja zake kwa Power Point mikutanoni na kisha akitoka ukumbini hakuna wa kuzitekeleza ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wa nchi hii.

Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. Binafsi sijali atajiunga na CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, n.k ilimradi tu asijiunge na ccm, mahali ambako mawazo mapya na utendaji ni dhambi. Akitaka Jimbo nitamchagulia Bukoba Vijijini na nitakuwa tayari kuanza kumpigia kampeni. Naamini maeneo yenye wapiga kura wengi kama Ibwera na Katoro hatutakuwa nahaja kabisa ya kupita kupiga kampeni.

Eid Mubraak!

Cc: FaizaFoxy, Ritz, omar Ilyas, njiwa, Nivea

Mkuu

Dr Bashiru Ally yupo CCM miaka mingi. Hivi ninavyoandika ndiye Karibu Mkuu wa CCM Taifa akipokea mikoba ya Komredi Al Habsy Kinana
 
jamaa ni msomi mzuri ila napata sana wasiwasi na origin ya uraia wake naona kama kakaa kitusitusi hv asije akawa mnyarandwa huyu embu muangalieni vizuri sura yake halafu linganisha na sura za wale jirani zetu kule kama anashahabiana nao 100%
 
Nmamisi sana Prof Haroub Othman aisee huyu mzee Mungu amlaze mahala pema peponi alikuwa anatunyoosha sana kwenye DS 101 nakumbuka maisha yangu ya First year pale UDSM semester II huyu mzee baba alinitungia swali moja hatare sana yani ni kama nilishindwa kumwela maana nlienda off point alafu jamaa nlikuwa nimekaa nae ananichungulia tuu hapo nkawa naenda kuitafuta Supp bado jamaa wananicheki tuu mbaya Zaidi invigilator baada ya kuona ninatokwa na jasho akahisi natafuta mazingira ya kukitoa kibomu dah akaja akakaa pembeni yangu hapo ndio nkawa nasesereka sasa naikaribia disco mzee maana nlikuw tayari semester ya kwanza nina Supp 3.
 
bashiru.jpg

Bwana Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Bwana Bashiru Ally ni miongoni mwa vijana waliofuzu makuzi ya kitaaluma na kijamii kutoka kwa watu wanaoheshimika na historia ya nchi hii; ile ambayo haikuhifadhiwa rasmi vitabuni. Enzi zetu tukiwa masomoni Bwana Bashir na Omar Ilyas ni miongoni mwa vijana waliopendwa na kujiweka karibu na Marehemu Prof. Haroub Othman (former VC-UDSM). Hali halisi inajidhirisha kuwa Bwana Bashir ndiye aliyefuzu kuyashika vema mafunzo na weledi wa Prof. Haroub Othman. Baada ya kuachana kitambo, miaka ya hivi karibuni nimekuwa nikimsikiliza, kumuona au kumsoma kupitia vyombo vya habari. Mara nyingine kwa bahati tumewahi kukutana kwenye mikutano.

Hivi majuzi Bwana Bashiru alishiriki mjadala wa DW juu ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya ugaidi. Msimamo na utetezi wa mtazamo wake juu ya jinsi vita hii inavyopiganwa nakubaliana nao kwa asilimia 100-"Mbinu zinazotumika kupambana na ugaidi ni za kigaidi na hivyo zinazidisha ugaidi"

Bwana Bashiru ni mtu aliyejipambanua kuwa na msimamo usiyoyumba katika masuala ya Kitaifa na yale yote anayoyaamini baada ya kuyatafiti kwa kina. Si mtu wa papara na kuropoka. Hisia zake juu ya jambo lolote hazijathibitika kufungamana na imani au itikadi. Kiufupi ni mtu-huru, mwenye fikra chanya kwa mustakhabari wa jambo lolote analoshiriki kulitenda au kulipendekeza. Tuna uhaba wa watu wenye sifa hizi katika utungaji wa sera na kuisimamia serikali. Kumuacha aendelee kuongea na makaratasi au kuwasilisha hoja zake kwa Power Point mikutanoni na kisha akitoka ukumbini hakuna wa kuzitekeleza ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wa nchi hii.

Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. Binafsi sijali atajiunga na CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, n.k ilimradi tu asijiunge na ccm, mahali ambako mawazo mapya na utendaji ni dhambi. Akitaka Jimbo nitamchagulia Bukoba Vijijini na nitakuwa tayari kuanza kumpigia kampeni. Naamini maeneo yenye wapiga kura wengi kama Ibwera na Katoro hatutakuwa nahaja kabisa ya kupita kupiga kampeni.

Eid Mubraak!

Cc: FaizaFoxy, Ritz, omar Ilyas, njiwa, Nivea
Atafutiwe JIMBO au MKE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa anaipeleka CCM kwenye udikteta kwa kuwaruhusu wapinzani wanaohamia CCM kugimbea viti vya ubunge bila kufuata mfumo uliowekwa na katiba ya CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmamisi sana Prof Haroub Othman aisee huyu mzee Mungu amlaze mahala pema peponi alikuwa anatunyoosha sana kwenye DS 101 nakumbuka maisha yangu ya First year pale UDSM semester II huyu mzee baba alinitungia swali moja hatare sana yani ni kama nilishindwa kumwela maana nlienda off point alafu jamaa nlikuwa nimekaa nae ananichungulia tuu hapo nkawa naenda kuitafuta Supp bado jamaa wananicheki tuu mbaya Zaidi invigilator baada ya kuona ninatokwa na jasho akahisi natafuta mazingira ya kukitoa kibomu dah akaja akakaa pembeni yangu hapo ndio nkawa nasesereka sasa naikaribia disco mzee maana nlikuw tayari semester ya kwanza nina Supp 3.
Mkuu hivi Prof. Haroub Othuman alikuwepo pale UDSM hadi wakati semester system inaanza?
 
kwann mkiona majina ya kiislam roho zenu zinawajaa chuki, husda, fitna na upumbavu? Mnadhani mnayofundishwa huko makanisani na akina slaa hatuyajui? Hii nchi siyo ya kanisa wala ya wakristo peke yao wala sio ya waislam peke yao. Ndio chuki mliyonayo kwa kikwete kisa dini yake. Mtakufa km mimbwa koko na chadema yenu ya kiliberali
Calm down
 
Back
Top Bottom