Mhadhiri Bashir Ally (UDSM) Atafutiwe Jimbo!

bashiru.jpg

Bwana Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Bwana Bashiru Ally ni miongoni mwa vijana waliofuzu makuzi ya kitaaluma na kijamii kutoka kwa watu wanaoheshimika na historia ya nchi hii; ile ambayo haikuhifadhiwa rasmi vitabuni. Enzi zetu tukiwa masomoni Bwana Bashir na Omar Ilyas ni miongoni mwa vijana waliopendwa na kujiweka karibu na Marehemu Prof. Haroub Othman (former VC-UDSM). Hali halisi inajidhirisha kuwa Bwana Bashir ndiye aliyefuzu kuyashika vema mafunzo na weledi wa Prof. Haroub Othman. Baada ya kuachana kitambo, miaka ya hivi karibuni nimekuwa nikimsikiliza, kumuona au kumsoma kupitia vyombo vya habari. Mara nyingine kwa bahati tumewahi kukutana kwenye mikutano.

Hivi majuzi Bwana Bashiru alishiriki mjadala wa DW juu ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya ugaidi. Msimamo na utetezi wa mtazamo wake juu ya jinsi vita hii inavyopiganwa nakubaliana nao kwa asilimia 100-"Mbinu zinazotumika kupambana na ugaidi ni za kigaidi na hivyo zinazidisha ugaidi"

Bwana Bashiru ni mtu aliyejipambanua kuwa na msimamo usiyoyumba katika masuala ya Kitaifa na yale yote anayoyaamini baada ya kuyatafiti kwa kina. Si mtu wa papara na kuropoka. Hisia zake juu ya jambo lolote hazijathibitika kufungamana na imani au itikadi. Kiufupi ni mtu-huru, mwenye fikra chanya kwa mustakhabari wa jambo lolote analoshiriki kulitenda au kulipendekeza. Tuna uhaba wa watu wenye sifa hizi katika utungaji wa sera na kuisimamia serikali. Kumuacha aendelee kuongea na makaratasi au kuwasilisha hoja zake kwa Power Point mikutanoni na kisha akitoka ukumbini hakuna wa kuzitekeleza ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wa nchi hii.

Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. Binafsi sijali atajiunga na CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, n.k ilimradi tu asijiunge na ccm, mahali ambako mawazo mapya na utendaji ni dhambi. Akitaka Jimbo nitamchagulia Bukoba Vijijini na nitakuwa tayari kuanza kumpigia kampeni. Naamini maeneo yenye wapiga kura wengi kama Ibwera na Katoro hatutakuwa nahaja kabisa ya kupita kupiga kampeni.

Eid Mubraak!

Cc: FaizaFoxy, Ritz, omar Ilyas, njiwa, Nivea
Hukutamani ajiunge na CCM Dah, kwa bahati mbaya sana kumbe jamaa alikua Kada Kindakindaki! Tanzania bhana
 
Bashiru zamani nilimwona kama msomi ambaye alikuwa anataka kuibadilisha hii nchi, ila nilimushuhudia kwenye kituo kimoja cha tv wakijadili kuhusiana na mabomu yaliyolipuliwa arusha, alikuwa anaongea kama mtu aliyetekwa na siasa za udini, badala ya kuongea hali halisi alijifunua na tukamujua namna alivyo, kwa ufipi mi namwona kama mtu hatari sana na hasa kwa kueneza propaganda za udini. Siku hizi hachambui mambo kama msomi mwenye kutaka kuleta mabadiliko ila anaongea km mtetezi wa dini fulani na pia kama mchocheza na mchonganishi
Wew jamaa ni janga la taifa
 
jf ni hazina Uzi wa mwaka 2013 utadhani umeandikwa leo. hapa Bashru amechambuliwa kama karanga
 
Hukutamani ajiunge na CCM Dah, kwa bahati mbaya sana kumbe jamaa alikua Kada Kindakindaki! Tanzania bhana
Mkuu huyu jamaa kama ungalimskia akiwa ktk mijadala ya Nkrumah...huwezi mpa hats funguo za ofisi za chama hicho. Huwa anakiponda sana sana. Mara ya mwisho nafkiri mwaka jana au mwaka juzi idara ya philosophy and religion iliandaa mjadala Nkrumah aisee...huyu jamaa kuna kuna wakati anakosa objectivity kbsaaa hasa acha tuu
 
Namjua tangu mwaka 1997, alikuwa anakaa Hall IV na mpemba mmoja anaitwa Salum. Huyu jamaa ni mzinzi sana, hafai hata kidogo!
Acha ku- attack mtu kwenye mambo yake binafsi. Sisi kunataka kujua kama umahiri wake wa ufundishaji na uchambuzi wa mambo ya kisiasa utamsaidia kuwa mtendaji mkuu wa CCM. Amekuwa anafanya uchambuzi na ufundishaji ambavyo kimsingi ni theories sasa yeye atakuwa na wakati wa kuweka yote haya kwenye matendo naye achambuliwe na wasomi wengine.
 
bashiru.jpg

Bwana Bashiru Ally, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Bwana Bashiru Ally ni miongoni mwa vijana waliofuzu makuzi ya kitaaluma na kijamii kutoka kwa watu wanaoheshimika na historia ya nchi hii; ile ambayo haikuhifadhiwa rasmi vitabuni. Enzi zetu tukiwa masomoni Bwana Bashir na Omar Ilyas ni miongoni mwa vijana waliopendwa na kujiweka karibu na Marehemu Prof. Haroub Othman (former VC-UDSM). Hali halisi inajidhirisha kuwa Bwana Bashir ndiye aliyefuzu kuyashika vema mafunzo na weledi wa Prof. Haroub Othman. Baada ya kuachana kitambo, miaka ya hivi karibuni nimekuwa nikimsikiliza, kumuona au kumsoma kupitia vyombo vya habari. Mara nyingine kwa bahati tumewahi kukutana kwenye mikutano.

Hivi majuzi Bwana Bashiru alishiriki mjadala wa DW juu ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya ugaidi. Msimamo na utetezi wa mtazamo wake juu ya jinsi vita hii inavyopiganwa nakubaliana nao kwa asilimia 100-"Mbinu zinazotumika kupambana na ugaidi ni za kigaidi na hivyo zinazidisha ugaidi"

Bwana Bashiru ni mtu aliyejipambanua kuwa na msimamo usiyoyumba katika masuala ya Kitaifa na yale yote anayoyaamini baada ya kuyatafiti kwa kina. Si mtu wa papara na kuropoka. Hisia zake juu ya jambo lolote hazijathibitika kufungamana na imani au itikadi. Kiufupi ni mtu-huru, mwenye fikra chanya kwa mustakhabari wa jambo lolote analoshiriki kulitenda au kulipendekeza. Tuna uhaba wa watu wenye sifa hizi katika utungaji wa sera na kuisimamia serikali. Kumuacha aendelee kuongea na makaratasi au kuwasilisha hoja zake kwa Power Point mikutanoni na kisha akitoka ukumbini hakuna wa kuzitekeleza ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wa nchi hii.

Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. Binafsi sijali atajiunga na CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, n.k ilimradi tu asijiunge na ccm, mahali ambako mawazo mapya na utendaji ni dhambi. Akitaka Jimbo nitamchagulia Bukoba Vijijini na nitakuwa tayari kuanza kumpigia kampeni. Naamini maeneo yenye wapiga kura wengi kama Ibwera na Katoro hatutakuwa nahaja kabisa ya kupita kupiga kampeni.

Eid Mubraak!

Cc: FaizaFoxy, Ritz, omar Ilyas, njiwa, Nivea
Maombi yako yametimia. Kapewa Ukatibu mkuu wa CCM
 
Namjua tangu mwaka 1997, alikuwa anakaa Hall IV na mpemba mmoja anaitwa Salum. Huyu jamaa ni mzinzi sana, hafai hata kidogo!
Kwani alikuwa ameoa wakati huo? Mtu asiye na ndoa hawezi kuwa mzinzi. Wazinzi ni watu wanaoacha ndoa zao na kutoka nje. Lakini mtu asiyeoa ni freelance acha ale vitu anavyovipenda till atakapojicommit!
 
Acha ku- attack mtu kwenye mambo yake binafsi. Sisi kunataka kujua kama umahiri wake wa ufundishaji na uchambuzi wa mambo ya kisiasa utamsaidia kuwa mtendaji mkuu wa CCM. Amekuwa anafanya uchambuzi na ufundishaji ambavyo kimsingi ni theories sasa yeye atakuwa na wakati wa kuweka yote haya kwenye matendo naye achambuliwe na wasomi wengine.
Usinzi kwa kiongozi wa umma au chama siyo mambo binafsi. Ukishakuwa kiongozi wa umma au chama inabidi ujiheshimu. Hata input yako iwe nzuri kiasi gani kama wewe huwezi ku-control matamanio ya ngono hufai. Tukiendekeza hili tutajikuta tunapata viongozi wanaoendeshwa na mataminio ya miili yao katika kutoa maamuzi. Labda nisisitize tu nimetoa mawazo ya kijumla kuhusu uhusiano wa uongozi vs sexual relationship, lakini sijui kama madai ya mchangiaji ni kweli au uongo, hivyo simhukumu jamaa.
 
Kwani alikuwa ameoa wakati huo? Mtu asiye na ndoa hawezi kuwa mzinzi. Wazinzi ni watu wanaoacha ndoa zao na kutoka nje. Lakini mtu asiyeoa ni freelance acha ale vitu anavyovipenda till atakapojicommit!
Mtu ambaye hajaoa tunasema ni muasherati. Uasherati nao haufai na si mzuri! Kama kabla ya kuoa huwezi kutulia na msichana mmoja na unabadilisha badilisha basi hata kwenye ndoa mke mmoja hawezi kukutosheleza. (NB: Hapa nime-assume madai ya mchangiaji ni ya kweli na siyo kama namhukumu huyo jamaa)
 
Nchi hii watu wanasoma ili wawe wanasiasa? Mtu anakuwa doctor au prof anaacha kuhudumia wananchi kwa kufanya research ili kuweka mazingira mazuri ya utafit anakimbulia kazi ambazo hata Lusinde darasa la 7 anafanya na ofcpz hawana tofauti ktk output zao.

Why why why my country? Prof Anna Tiba, Mwandosya, Hemed Msolla et al. Yani uprof wenu mnaiexercise bungeni ambako hata non-elite anaweza perform?

Sasa kijana kama huyu anataka kuzamia huko nae, mweeee kazi iko. Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za nje kidogo, ukichunguza mabunge mengi wazee ndio wako huko wkt ss vijana ndio option yenye ulaji tunaiona. Ka
MzLendo si uanzishe kitu ili kusaidia watu wengi kwa kutumia ujuzi wako wa darasani?

Inakatisha tamaa wasomi kukimbilia dodoma kwa kweli na vyuoi wanabaki ma-TA na Ass Lecturers
hongera mkuu tatizo wasomi watz wengi kwasababu ya umaskin wameona siasa ndo sehemu ya kupiga mpunga ndo maan unakuta watu hata waliosoma science wanatumbukia huko kwa sababu tu ni makada au undugu sio uwezo mtu alionao.
my take: wasomi watanzania waangalie professional zao na wafanye kulingana na principles za career zao kwa mfano mtu aliyesoma science aangalie nikipi ambacho anaweza kugundua kitakachoishangaza dunia na kuleta mabadiliko.
The role of modern educator is not to cut down jungle but to irrigate desert -Arristotle
 
Back
Top Bottom