umeuliza vizuri ila umemalizia vibaya. uhuru una mapana yake ambayo ukiyachanganua na kufananisha na nchi husika utagundia kiwango cha uhuru uliopo. nchi kujitawala yenyewe haimanishi kwamba ipo huru kwasababu hali hiyo inaweza kuwa uhuru wa bendera ili hali huwezi kufanya maamuzi yako mwenyewe. kwa wananchi uhuru ni kufanya mambo yao ya kila siku kwa mujibu wa sheria ambazo hazina vizuizi kandamizi, kwa mfano haki ya kuandamana haiitaji kibali bali matakwa ya wananchi pale wanapoona inabidi kufanya hivyo
kaka tanzania daima wameiandika japo sio kwa undani.
na avatar yako ina picha ya mwana chadema alafu unaponda kimoyomoyo tehetehetehetehe poke mkuummeacha sema Kilimanjaro?mlikwenda pia na arusha,baadaye mbeya, baadaye sijui mtasema dar kwa vile napo wana ushawishi mnono.soon moro,bila kusahau iringa walipobidi muua mwangonja.
Ukiwa gamba inabidi uwe chizi hata kama huokoti makopo,nadhani safari hii hata mtwara na songea watasema ni kaskazini.....wanalo na laana yao mkuu.ongezea kuwaambia kwamba wazidi kuiwaza kaskazini na uwasisitizie kwamba mwanza nayo ni kaskazini maana wana macho lakini hawaoni.peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees.
Ukweli husemwa:
Waziri Mizengo Pinda hawezi kusema maneno ya chama wakati yuko kazi kiserikali kama Waziri Mkuu. Na huo haukuwa mkutano wa chama bali wa wananchi ambao siyo wa vyama vya CCM na CHADEMA pekee. Watanzania bana, kwa sasa kila kitu ni siasa.
Tuacheni majungu ya kisiasa.
Weka Audio na sisi tusikilize kama alikuja kwenye ziara ya serikali CCM hoyee ilitoka wapi? na Pipooooz power ilitoka wapi?
Bado sijakuelewa labda nisikilize mimi mwenyewe audio.
CCM ni Wastaarabu na ndiyo maana wanaheshimika hata ugenini na wana sera siyo matusi wawapo majukwaani tofauti na CDM na vurugu, kukosa sera na matusi majukwaani.
hapo pm anapoligharimu taifa kwa msururu wa misafara yake ndipo palikotia nyongo furaha yangu.
Hivi kama hii nchi ni ya amani kweli kama wanavyosema ccm, je ni kwanini basi viongozi wao/serikali wasiwe na misafara midogo na tena yenye askari/walinzi wachache tu? Utakuta msafara una askari zaidi ya 100, magari ya usalama zaaidi ya 8, bado magari ya halmashauri, mikoa, na serikali kuu nk jumla utakuta zaidi ya magari 25.
Heche alisema hivi, namnukuu "....utakuta waziri mzima ametoka dar na msafara wake wanakwenda rukwa kuzindua mradi. Sasa waziri na msafara wake wanatumia shs milioni 80, au 100.....halafu mradi wenyewe wanaoenda kuuzindua ni wa milioni 4, au ni jengo la darasa ambalo halizidi milioni 20! Mkifanya mchezo watawauza na ninyi wananchi ili walipie matanuzi yao. Mshukuruni mungu chadema ipo inayapigia kelele...vinginevyo hawa jamaa wangekuwa wameshawauza..."
huu ni ubadhirifu uliohalalishwa lakini lazima tuushughilikie, muda ni sasa.