Mh. Pinda alazimika kutumia PIPOZIII...POWER kumaliza hotuba yake

[h=2]
pindaaa(8).jpg


Wenje ateka mkutano wa Pinda[/h]Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Hezekiah Wenje, jana aliuteka mkutano uliopangwa kuhutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambapo wananchi waliohudhuria walimshangilia zaidi yeye (Wenje) huku wakinyoosha vidole viwili ambayo ni alama ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Hali hiyo ilijiri jana saa 11:00 baada ya msafara wa Waziri Mkuu kuingia katika viwanja vya Sahara huku Wenje akiwa miongoni mwa waliofuatana na Pinda.

Baada ya Pinda kuteremka kwenye gari na kuanza kuelekea kwenye meza kuu huku akisalimiana na baadhi ya wananchi, sehemu kubwa ya umati uliokuwepo walikuwa wakionyesha ishara ya vidole viwili na mara walipomuona Wenje walilipuka kwa shangwe ambapo Mbunge huyo machachari naye aliwanyooshea ishara ya vidole viwili.

Kama vile haitoshi baada ya Waziri Mkuu na viongozi wa mkoa wa Mwanza aliokuwa amefuatana nao kuketi vitini, ndipo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, alisimama kwa ajili ya kufanya utambulisho na alianza kwa kumweleza Pinda kuwa hizo ndizo harakati za miji mikubwa.

Wakati Konisaga akisema hivyo, wananchi waliendelea kushangilia, hali iliyomfanya adai kuwa wanamshangilia yeye (Konisaga) kwa sababu ndiye mtawala wa eneo hilo, lakini wananchi walionekana kuguna kwa sauti kama ishara ya kutokubaliana naye.

"Hayo makofi mnanishangilia mimi, kwa sababu bila mimi hakuna mkutano," alisema Konisaga na kupokelewa na sauti za wananchi walionekana kupingana naye wakisema weweeee! Katika utambulisho, Konisaga alianza kwa kumtambulisha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, lakini wananchi walionekana kupinga hatua hiyo ndipo Konisaga akawaambia bila yeye (Kabwe) hakuna maendeleo Mwanza.

Hatimaye Konisaga alimtambulisha Wenje ambaye alisimama kuelekea jukwaani huku akishangiliwa kwa nguvu na wananchi ambao walikuwa wakimshangilia kwa kuimba "mbunge, mbunge, mbunge".

Alipofika jukwaani na kupewa kipaza sauti, Wenje alianza kwa kusema: "Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili ndilo Jiji la Mwanza. Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita sijawahi kuona nguo za kijana uwanjani hapa."

Kauli yake ilizididha mlipuko wa sauti za wananchi wakimshangilia na ndipo alianza kumweleza Waziri Mkuu kwamba Jiji la Mwanza lina malalamiko mengi ya wananchi kuhusu migogoro ya ardhi.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu, Jiji la Mwanza lina malalamiko mengi ya ardhi. Nimesema sana ndani ya Bunge, lakini mnanijibu kisanii. Nimemweleza na Waziri wa Ardhi kwamba wanaoteseka sio Chadema peke yao kwani hata wana-CCM nao wana malalamiko vilevile," alisema.

Wenje ambaye alikuwa amepewa nafasi ya kusalimia tu, aliongeza kuwa ni matumaini yake kwamba ujio wa Waziri Mkuu katika mkoa wa Mwanza utaleta ufumbuzi wa migogoro iliyokithiri katika sekta ya ardhi.




CHANZO: NIPASHE

 
kama kuna watu vilaza kwenye uongozi wa jk mm kwa upande wangu pinda anaongoza!...huyu babu ni hewa kabisa,yeye kujifanya mnyenyekevu kumbe upuuzi mtupu.mtakoma na pipoz mwaka huu........
 
mmeacha sema Kilimanjaro?mlikwenda pia na arusha,baadaye mbeya, baadaye sijui mtasema dar kwa vile napo wana ushawishi mnono.soon moro,bila kusahau iringa walipobidi muua mwangonja.

Samahani kaka ina maana polisi wameua mtu mwingine Iringa?
 
Weka Audio na sisi tusikilize kama alikuja kwenye ziara ya serikali CCM hoyee ilitoka wapi? na Pipooooz power ilitoka wapi?

Bado sijakuelewa labda nisikilize mimi mwenyewe audio.
Mbona wewe hukuweka Audio ya milio ya bunduki za polisi kule Madale?
 
Hivi nyinyi mmeiamini hii habari?

:A S 465:Nimeona nilete nukuru kutoka gazeti jingine zaidi labda utaamini kama kuna ukweli wa habari hii:A S 465:

Pinda azomewa
  • VIJANA MWANZA WAIMBA ‘PEOPLE'S POWER, HATUITAKI CCM'

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza kwa muda kutokana na wananchi wengi kumzomea.
Kiongozi huyo alikumbana na kisanga hicho cha aina yake akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Welle Ndikilo. Pinda na viongozi hao, walikumbana na zomeazomea hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sahara jijini hapa, ikiwa ni hitimisho la ziara ya Waziri Mkuu huyo ya siku saba mkoani Mwanza.
Chanzo cha Pinda na viongozi hao kuzomewa mkutanoni hapo, ilitokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa kero nyingi zilizodaiwa kushindwa kupatiwa ufumbuzi na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Kitendo hicho cha wananchi kilimlazimisha Pinda kushindwa kuhutubia kwa muda, huku akionekana kujawa jazba.

Sababu nyingine ya wananchi kuzomea, ni hatua ya Pinda kuwaambia wananchi hao watoke mjini waende vijijini wakalime waachane na mambo ya upinzani wa kisiasa.

Pinda alitoa kauli hiyo baada ya kundi la vijana mkutanoni hapo kuonesha alama ya V, bendera ya CHADEMA na nyimbo za Peoples, Power.
Kwa mazingira hayo, askari wa polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), waliokuwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG, mabomu na marungu waliokuwepo mkutanoni hapo, walianza kuwatishia kuwapiga wananchi hao kwa lengo la kumlinda kiongozi huyo.


Baada ya kuzidi zomeazomea hiyo, Waziri Mkuu, Pinda alilazimika kumuita mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliyekuwa meza kuu, kisha kusema:
"Nyamazeni basi!. Wenje...hii ndiyo serikali ya siku chache zijazo." Pinda "Kwa namna hii naona hamuwezi, maana itakuwa ni vurugu asubuhi hadi jioni". Akazomewa kisha wakaimba hatutaki CCM, hatutaki CCM. .


Baada ya kuona hivyo, Pinda akacheka na kusema: "Hahahaaaaa, hata mkiimba peoples power, CCM ndiyo inayowaongoza". Akazomewa tena kisha Pinda akashindwa kuendelea kuzungumza jukwaani.

Akahutubia mkutanoni hapo, Pinda aliwataka wananchi hao waache ushabiki wa kisiasa, na kwamba halmashauri ya jiji la Mwanza inayoongozwa na CHADEMA, ndiyo itapaswa kulaumiwa kama itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.
"Hapa jiji la Mwanza linaongozwa na CHADEMA. Meya wa CHADEMA, mwenyekiti wa Mipango miji wa CHADEMA, Naibu Meya ni wa CHADEMA. Lakini kama wameshindwa kuweka mipango mikakati ya kuwasaidia tutasema hawafai," alisema kisha akazomewa kwa mara nyingine.

Baada ya zomeazomea hiyo kuonekana kumwelemea Waziri Mkuu huyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Ndikilo alilazimika kuingilia kati kwa kusema: "Wanaozomea tunawafahamu, na tunawafahamu waliowaleta hapa ili mje kufanya nini". Akazomewa.

Hata hivyo, baada ya hali kutulia kidogo, Pinda aliendelea kuhutubia huku akiwataka wananchi wa jiji la Mwanza waondoke mjini waende vijijini wakalime, jambo lililoonekana pia kuwakasirisha wananchi wengi kisha kumzomea tena.
Ingawa Pinda alilazimika kutumia muda mfupi kutoa hotuba yake, aliwaomba wana Mwanza washirikiane kuleta maendeleo yao, na kwamba iwapo tatizo ni Mkurugenzi wa jiji suala hilo litaangaliwa.
Aliwaomba wadumishe amani iliyopo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Serikali kupambana na vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, ili kuweza kuzua samaki wadogo wasivuliwe kisha kuharibu mazalia ya rasilimali hiyo.
"Jambo jingine ninalotaka kuwaeleza hapa leo ni hili la uvuvi haramu. Samaki ndani ya Ziwa Victoria wameisha...na hii ni kwa sababu ya uvuvi usiozingatia sheria. Tushirikianeni kupambana na vitendo hivi", alisema Pinda kisha akazomewa tepa.
 
Kwa navyomjua mtu aliyefilisika kisera, atakachosema this time ni kwamba Mwanza ni Kaskazini

Las Mas Boboas: Kumbuka pia kwa wale magwiji wa propaganda watasema ni kaskazini kwa kuwa Mwaza ipo kaskazini mwa reli ya kati. Unaona eh!!!!!!! Watu wa ajabu sana hawa they never think outside the box.
 
Kwahiyo maendeleo ya nchi kwako ni maandamano ya toka uchaguzi hadi uchaguzi yanayosababisha mauaji kwa watanzania sio??
Watanzania wanahitaji sera zenye kuleta maendeleo kwao na sio kutangaza siasa za chuki na maandamano ya kila siku yasiokuwa na tija, badala yake kusababisha mauaji ya watanzania wasio na hatia. Au wewe unafaidika na vifo vya watanzania nini, kwamba akiuliwa mtanzania na polisi kwako ni nafasi ya kujizolea umaarufu kwa kuishutumu serikali!!!!
I don't understant u guys taking "pipoz powa"!

you'll never understand as long as you are a magamba.
 
Ni kweli Mwanza ni moja ya ngome kuu za Chadema,JK aliipenda sana Mwanza na Arusha lakini sasa hebu oneni
ni lini kafika Mwanza kwa mara ya mwisho,kinachonishangaza MAGAMBA wana roho kama ya FARAO,mna macho lakini hamuoni na tena mna masikio lakini hamsikii.Mnaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Kumbe kuna watu humu hawajui hata maana ya propaganda. Yani hata mtu akishuhudia kitu halisi kwa macho ama masikio yake, bado anasema ni propaganda, Daaaah...!
Kwani wewe ulihudhulia kwenye huo mkutano?Mbona unapotosha watu?Peoples power aliitoa bt c kwa 7bu ya kutosikilizwa bali ni kwa kejeli za wa2 waliokuwa wamenunuliwa viroba na (Mb) wa jimbo hilo.
 
Nilijua tu kuwa utatukana, na upeo wako mdogo wa kutafakari lazima ungekutuma niamini upuuzi wako unaoufikiria. Watanzania wenzangu mmeona hawa wanaojiita great thinkers , kumbe ni CDM thinkers, teh teh teh teh, twende tu hivi hivi hata CDM wakichukua nchi kutokana na upeo wenu mdogo wa kukubali kila jambo.

Umeulizwa kuwa Magamba wanapohutubia majimbo ya CDM Kaskazini na yale ya ccmB kule Pemba huwa kuna utulivu zaidi kuliko yale ya Mbeya,MWZ na Iringa. Jibu kwa nini hivyo?. Kama huna jibu andika "NO COMMENTS".
 
Back
Top Bottom