Mh. Pinda alazimika kutumia PIPOZIII...POWER kumaliza hotuba yake

Zile propaganda za kina Nape kwamba Chadema chama cha kaskazini bado zinaapply?
 
Achana nao ..kwani hawajui propaganda sahihi na zenye kufuata ukweli ni Halali?Kwani promotion ni nini?Mbaya hata promotion zina uongo na mengine mengi ili kukwaza wapinzani.Ila hili n iwa wazi CCM automatically wanatia watu kichefuchefu.Na kutokea katika umati wa watu ni chokizo la wengi.
 
JF kulitakiwa kuwe na jukwaa la HABARI TAMU TAMU. Uzi kama huu ni mtamu kwa kweli. Ni mtazamo tu, magamba msijenge chuki
 
Ritz leo anapiga shift moja tu? Nilitarajia nimkute humu akishuhudia propaganda yake ya ukabila ikishindwa...
 
kile kikaragosi kinachoitwa ritz, leo kinapiga shift moja tu? Nilitarajia nikikute humu kikishuhudia propaganda yake ya ukabila ikishindwa...

Ritz, Rejao, Mafilili, Zomba and three others does not like this !!!
 
Mkuu, jibu la hilo lipo wazi, hawaelewi wakikaa ofisini wafanye nini, kwasababu ofisini kuna kazi nyingi while wao hawazioni then wanajikuta hawana cha kufanya hence wanakua bored halafu wanasinzia.

Ili kutoa usingizi bora waende safari kama hizo, baadhi ya mizigo ya safari ndo hiyo mikasi, Nina maana ya mikasi hii ya kukatia sio mikasi ile ya vijana.

Kwa Nchemba bila "Mikasi" ziara haijakamilika bado, na yule mwingine Joseph Josephat. lazima wafanye "Uzinduzi" tena wanapenda sana"Majimbo" ya watu!
 
ulizia kilichomtoke kwenye mkutano kahama.
Aliomba watu wamwambie wanachotaka, akanyanyuka Mzee miaka kama yake akamsifia ,akashutumu viongozi kahama,akampongeza Nyerere kwa kuleta vyama vya siasa baadaye akasema :Nukuu 'sasa naomba watu wote tusimame tuseme CHADEMA, Vema'.
Pinda akajikuna kisogoni
 
Ngoma unapiga mwenyewe, kuimba uimbe mwenyewe na kucheza pia ucheze mwenyewe, khaa!? Chadema bana!!?
Hivi cdm mna lipi la kuwaeleza wa-tz 2015? Au ni hayo mayowe ya ukombozi wa nchi iliyo huru?
 
Weka Audio na sisi tusikilize kama alikuja kwenye ziara ya serikali CCM hoyee ilitoka wapi? na Pipooooz power ilitoka wapi?

Bado sijakuelewa labda nisikilize mimi mwenyewe audio.
 
Wewe ni muongo mkubwa mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye mkutano huo, Waziri Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kiserikali na siyo ya Kichama na hakuna hata dakika ambayo alitamka neno CCM hoyee wala peopleeeez.

Kajipange upya kuja na uongo mwingine. Kulikuwa na sababu gani ya Waziri mkuu kusema CCM hoyee au Peopleee wakati akiwa kwenye ziara za kiserikali? Watanzania tujihadhari sana propaganda ambazo hazina mvuto wowote.

Eti wenje alibebwa. Wenje sasa hivi amekalia kuti kavu hapa Mwanza, labda kama maneno unayoasema ni ya kutaka kumfariji.

Weka sauti na picha zinazoonesha maneno ya PM na Wenje.
 
Afadhali wewe, inawezekana kabisa PM akawa amekumbana na hali inayoonesha CDM kukubalika, lakini siyo kweli alitamka Peopleeez. Teh teh teh , watu weingine bwana. Ina maana sisi tulikuwepo wote tusisikie maneno hayo?
 
Back
Top Bottom