Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Mtoa mada katuumwa huyo na mafisadi ili waendelee kunufaika na pesa zetu. NSSF wanawakopesha wanasiasa wasochangia kitu then wanatupangia muda wa kuzeeka. nani kawaambia mzee ni kuanzia 55years.mtu kama huna pesa unakuwa mzee hata kama una 30 years. kuna mambo mengi ya kubishaniwa. Myika mbele kwa mbele tuko nyuma yako. Kwanini kipengele cha umri walikiingiza kwa mlango wa nyumba april na sio February walipopeleka mswada bungeni? wote ni uizi mtupu
 
SIYO upeo finyu, ni uzoefu wake, pia nadhani anatusaidia kuelewa mamba ambayo ni zaidi na yale tunayoelewa, mimi pia nimeona watu wakipeleka NSSF wakiwa na mikataba ya mwaka 1, miwili, nk. actually ninachokusudia kusema ni kwamba, tusione mchango wa mtu kwa mtazamo wa ufinyu, lets see if that what you call ufinyu can contribute to what we know.Na pale tunapoona mwingine hajaelewa vizuri au hajaelewa kama sisi tulivyoelewa, tujenge hoja itakayofanya tuelewe sawa. mimi binafsi napenda the way watu wanavyokuwa na mitazamo tofauti, I really enjoy, and I like your constructive contributions.

Mheshimiwa,

Nilipotumia neno ufinyu wa kulielewa jambo hili ni sikum-point yeye. Ufinyu kwa maana ya kwamba watanzani wengi wana ufinyu wa kulielewa hili.

Tuje kwenye unachosema. Unapokuwa na contract ya miaka chini ya mitano, ni rahisi kujinganisha na ubunge hata kama hujui utaalamu wa pension.

Wapo wanaotumia lugha ya kejeli kumponda mleta mada wakati wao hakuna hata mmoja anayepeleka NSSF mshahara wa Housegirl wake!

Hivyo, kazi ya contract ambayo inajulikna wazi kuwa contract ina mwisho huhitaji kupeleka NSSF ambako hawana policy ya kujitoa.

Tatizo watanzania wengi hata kujiunga kwenye hizi schemes wanafanyiwa na mwajiri na huyo mwajiri anapeleka anakotaka yeye. Watanzania hawaulizi kwanza status ya scheme inayomfaa kabla ya kujiunga na hivyo kama ni mhidni anajua kuwa kuna NSSF tu na hivyo anapeleka huko ndipi staff anajikuta kachaguliwa scheme na mwajiri na haya yot ekutokea.
 
Siwezi kumlaumu Mnyika kwa sababu nae ni Mwanasiasa,kitu cha msingi Sober ni kutoa elimu kwa wafanyakazi ambao haya mambo yanawahusu.Kabla ya hili sakata sidhani kama kuna mfanyakazi alikuwa anayajua haya
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada inaonekana ana interest na mifuko hiyo lakini hiyo sheria haijazingatia sisi wanachama kwanza tunataka hii sheria au hatuihitaji.
Pili thamani ya fedha sasa na baada ya miaka ishirini i takuwaje

Sheria hii inaonekana ni kwa ajili ya kuilinda mifuko ili serikali iendelee kukopa ila wafanyakazi wafe njaa
 
nachoona hapa ni matunda ya multiple ID,mwanzinsha mada na baadhi ya wanaomuunga mkono naamini ni mtu moja anapigia upatu huu wizi wa magamba,tunasema hivi hizo pesa ni akiba zetu na tutazichukua tunapozihitaji! Kama unabisha subiri bunge likatae kurekebisha hiyo sheria uone tutakachofanya...kwa hili tupo tayari kwa lolote hata mvue nguo hatutakubali.nimemaliza...

Ndugu,
Yaani toka nianze kusoma maoni sijapata ambalo limenikosha kama hili!!!
You have said it all...ni kwamba watake wasitake hizo hela ni zetu na hakuna mtu mwenye dhamana ya kutupangia
jinsi ya kutumia pesa zetu.

Kama wasipobadilisha hizo sheria basi wategemee HUJUMA za hali ya juu sana ktk majengo yao huko Dar,Arusha na Mwanza. Mbinu za Al-Shabab au Boko Haramu tutazitumia tu,no way! Yaani wenyewe wakopeshane hela zetu afu leo
waje na sheria za ki-PUUZI namna hii??? Kweli???!

Subirini tu,wanachokitaka watakipata!
 
Sober
si lazima kuiga kila jambo linalofanywa katika nchi nyingine.
Mafao ya kujitoa ni muhimu kwa watu ambao wanafanya kazi kwa mikataba. Nafikiri ni sahihi kwa mtu aliyemaliza mkataba wake na haendelei tena kufanya kazi ya kuajiriwa sehemu nyingine akapewa mafao yake; si sawa eti asubiri hadi atakapofika miaka 55. why miaka 55? Ili wakubwa watumie fedha zake kujinufaisha?

Ndg yangu usiwaite wajinga watu wanaodai haki yao. Tumeshuhudia wafanyakazi wa sekta binafsi wanavyoipinga sheria hii. Sheria wanayopinga ni kandamizi kwao kwa sababu inawalazimisha wafike miaka 55 ili wapewe mafao yao. Ni muhimu sheria yoyote ile iwe ni ile yenye manufaa na inayotokana na wananchi. sheria inayolazimishwa na wanasiasa wakati wahusika hawaitaki ina mashaka

Namalizia kwa kusema John Mnyika hajakurupuka; anajaribu kuwasilisha mawazo na maslahi ya wafanyakazi wa sekta binafsi ambao wengi wao hufanya kazi za ajira kwa mikataba. Ni muhimu wabunge wa CCM na serikali wakamuunga mkono badala ya kushabikia CCM yao
 
Last edited by a moderator:
Elewa mantiki ya CAG
kuliongelea hili na siyo kukurupuka tu. Alichokiongelea ni mifuko
inaweza kufilisika kama serikali haitalipa deni inayodaiwa na hii
mifuko. Kumbuka guarantee ya mikopo ya serikali ni 100% kulipwa, so kwa
hili wanachama hawatakiwi kuwa na wasiwasi wowote

wewe kama sio IRENE KISAKA Cjui maana majibu yako na yake sawa sawa full copy n paste toka kwa wazungu bila kuangalia hali halisi.
 
Mimi nimefurahi na haya yote uliyozungumza lakini ujazungumzia iwapo huyu mtu akafanya kazi miaka yote alafu wakati wa kudai mafao ikatokea pengine hizo kampuni za mafao zikawa zimekufa au zimefilisika kwa kuwakopesha serikali fedha ambazo watashindwa kuzirejesha. Ukumbuke kwenye maswala ya Planning tumekuwa wakati mwingine ni wapangaji wazuri lakini kwenye usimamizi tumeshindwa na wakati mwingine tumejikuta wananchi wengi wakikosa haki zao na kurudi kwenye maisha ya dhiki.

Fikiria mtu atakapofikisha umri huo na akakuta mfuko uko bankrupt au hauna fedha za kumpa mafao yake itakuwaje. huoni bora mtu achukue chake mapema, kwani mpaka leo wazee wa jumuiya ya Africa Mashariki nadhani unaona wanavyopata shida si kwamba fedha zao hazikuwepo ila zilitumiwa na wajanja na wao kubaki hawana kitu.
 
Uzoefu wa hii mifuko mingi ni kuwa mwanachama anapochukua mafao ya kujitoa, mwanachama huyuhuyu atarudi kujiunga tena ndani ya miezi 18. Kwa hiyo suala la kusema unafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili na una miaka 30 hivyo utatakiwa usubiri miaka 28 ili upate mafao yako, si sahihi kwa asilimia 100%.

Ila nimefurahi kupitia uzi huu nimeweza kujifunza mambo mengi sana, na kwa kweli inasikitisha kuona elimu ya umuhimu wa kuwa na akiba ya uzeeni inapokosekana kwenye mitaala yetu ya mashuleni.

Naomba niwaulize kitu kimoja tu. Je mmewahi kujiuliza ni kwanini watumishi wa hii mifuko, wao wenyewe wanawaomba waajiri wao wawawekee supplementary schemes kwa ajili ya kupata pension ya ziada? Sababu ni rahisi, wao wanaona jinsi pensheni zinavyowapa wazee nafuu kubwa ya kipato, na wengi wao wanaextra account mfuko wa UTT kwa ajili ya mafao ya uzeeni.


Mh. Mnyika, najua wewe umekomaa kisiasa, chukulia uzi huu kama changamoto za kuboresha utendaji wako na hasa linapokuja suala tata lenye kuhitaji upembuzi wa wataalam.

Niliona kama mtanzania mwenye ufahamu japo kidogo wa haya mambo, nijaribu kushare na wenzangu, ili pengine niwape kidogo cha ziada kufikiri badala ya kushabikia kwa nguvu kila kitu(hasa pesa ya leoleo). Ila kama michango mingi ilivyo, watu wameamua kujinyonga wenyewe kwa kamba zao... Sina la ziada bali ni kuongeza urefu wa hiyo kamba kwa wale watakaotaka kujinyonga.

Kwa wale walionielewa nawasihi sana, tukumbuke fainali uzeeni, hisani za watoto wetu kwa miaka tunayoelekea zitazidi kupungua sababu na wao gharama zitawaelemea... tutajuta na kusaga meno huku nguvu zikiwa zimeisha, nakubaki na msemo wa NINGEJUA!

Namalizia kwa kusema HUTAKI UNAACHA!.... FAINALI UZEENI.

Hutaki unaacha ..Fainali ni leoleo na uzeeni ni kusimulia wajukuu ulifungaje magoli kwishney!
289958318.JPG

Mkazi wa jijini Dar es Saalam, Mzee James Mafita ambaye alikua mfanyakazi wa Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii wa wakati huo, akitafuta wateja wa kununua boga kama alivyokutwa katika mtaa wa Mkwepu. (picha: Francis Dande/Habari Mseto blog)

Faida ya kutunziwa fedha halafu upate adha hii ya nini?

Source: http://www.wavuti.com/4/previous/2.html#ixzz22a5GdzzJ
 
Mnyika ni Mbunge kijana na makini sana. Lakini zaidi sana, ni muungwana. Ukisoma hoja yake ameomba radhi kwa wana_ubingo na wafanyakazi kwa yeye binafsi kutokuwakilisha mapendekezo ya marekebisho juu ya suala hili lililopitishwa 'kinyemela'. Naomba ninukuu kutoka kwenye blog yake...

'Ikumbukwe kwamba kifungu cha kufuta mafao ya kujitoa kilichozua mgogoro hakikuwepo wakati muswada uliposomwa kwa mara ya kwanza bungeni tarehe 1 Februari 2012 bali kiliwasilishwa kupitia jedwali la marekebisho ya Wizara lililowasilishwa tarehe 13 Aprili 2012 bila malengo na madhumuni yake kuelezwa kwa ukamilifu.

Kupitishwa kwa kifungu hicho kumethibitisha maneno niliyoyatoa bungeni kuwa tumefika hapa tulipo kutokana na ‘uzembe wa bunge na wabunge’ na kwa hili pamoja na mchango nilioutoa bungeni kwa maandishi siku hiyo juu ya haja ya kuwa mfumo mpana zaidi wa pensheni na hifadhi ya jamii (universal pension and social security) pamoja na kuwa sikuunga mkono kifungu husika kilichoingizwa kinyemela naomba radhi kwa wananchi wa Ubungo na wafanyakazi kwa kutokuwasilisha jedwali la marekebisho kupinga kifungu hicho kuingizwa.'

Pamoja na kwamba wabunge wote wana wajibu wa kutetea yale yaliyo na maslahi kwa wananchi, yeye amechukua dhamana na kukili kosa.

Sasa nirudi kwa mtoa mada..Umeongea vizuri kwa asilimia fulani lakini unakosea kwa shutuma na maneno makali dhidi ya Mnyika. Alichokisema Mnyika ndio mapenzi ya wafanyakazi walio wengi.

Ikumbukwe kuwa lengo kuu la mwanasiasa yeyote yule ni kuongoza/kutawala kama lilivyo lengo la chama chochote cha siasa ni kushika hatamu. Hii ndio elimu ya siasa ninayoifahamu na wanazuoni wa siasa watakubaliana nami. Sasa mwanasiasa anapofanya jambo lenye maslahi kwa wananchi wake anaowaongoza ni kwamba anakuwa anatimiza malengo yake. Tuache unafiki, huo ndio ukweli.

Sasa nirudi kwenye suala la mafao na kwani wafanyakazi wanaona bora wajitoe wakati unaporuhusu. Ukweli ni kwamba mfumo wa mafao Tanzania si mafao bali ni wizi mtupu. Narudia ni wizi mtupu. Najua humu kwenye jamvi watu wanapenda data, haya soma hapa:
Old Age Pension

Natumia tu mfano uliotolewa na NSSF wenyewe. Mtu ambaye anawastani wa mshahara Tsh 360,000 aliyefanya kazi miaka 20 (240 months) akistaafu anapewa Lump Sum (mafao mkupuo) Tsh 3,240,000 halafu pensheni ya mwezi (Monthly Pension) Tsh 135,000.

Sasa kwa nini nasema wizi mtupu, mtu huyu kwa miaka 20 anakuwa ameweka akiba ya Tsh 17,800,000 (yaani 72,000 kila mwezi mara miezi 240). Sasa mtu aliyeweka akiba kiasi hicho unampa Tsh 3,240,000 na kila mwezi Tsh 135,000. Watu wanaojua hesabu twende pamoja..Hii inamaana itamchukua mtu miezi 104 kumaliza akiba yake sawa na miaka takribani 9 baada ya kustaafu. Sasa ni wangapi wanaishi kiaka 69?? Ijulikane hapa kwamba bado hapo unakula ela yako hamna riba!!! Huu ni mfano wa NSSF ambao kwangu mimi ndio mfuko kandamizi kuliko yote.

Formula ya PPF ni tofauti kidogo ila bado nayo ni kandamizi. Wenye muda wafuatilie: :: PPF Pensions Fund ::-

Niseme tu, kwa mtu anayepata wastani wa mshahara Tsh 2,000,000 leo akistaafu, mafao ya mkupuo (Lump Sum) ni Tsh 62M kwa LAPF/PSPF; Tsh 14.4M kwa NSSF, na Tsh 22.5M kwa PPF wakati Pension ya mwezi (monthly pension) ni Tsh 333,333 LAPF/PSPF; 600,000 NSSF, na 450,000. Hii ni kama utakuwa umefanya kazi kwa miaka 15 ya vigezo (miezi 180) ambayo ni lazima. Kwa kipindi hizo, michango ya yako na mwajiri (20% kwa mwezi Tsh 400,000 kwa miezi 180) ni Tsh 72M. Hapa utaona mfuko wa kujiunga ni PSPF na LAPF.

Swali la mwisho, kama leo napata mshahara wa Tsh 2,000,000 na pension ya juu ya mwezi ninayoweza kupata ni Tsh 600,000, je ni kweli maisha yangu yatabaki vile vile? Tusijidanganye, kwa mfumo kwa kitanzania HAPANA. Kwa yeyote anayemfahau mstaafu ambaye anaishi maisha mazuri kwa pensheni amtaje. Wengi wanaoishi vizuri ni wale waliojiandaa na kuanzisha miradi kabla ya kustaafu.

Nimalizie kwa kusema, watanzania pia inabidi tuwatendee haki wanasiasa wa vyama vya upinzani. Mara nyingi tunawakumbuka wakati wa shida kama sasa tunasikia humu jukwaani watu wanauliza wabunge wa CHADEMA walikiwa wapi? Wakati wa mavuno tunawatosa! Hii sio sawa; sasa ndio hivyo tunakula jeuri yetu. Kama upinzani tunaona unatetea maslahi yetu basi tuwape nafasi na CCM wawe wapinzani ili wajifunze.

Suala la kulazimisha watu wasile chao mpaka miaka 55-60 halikubaliki!
 
Mtazamotu
Tupo pamoja mkuu.
Kitaeleweka tu,otherwise ni HUJUMA tu na hapatakalika!
Afadhali tukose wote kuliko tunyanyasike eti kisa hatujafikisha 55yrs...UPUUZI mtupu!
 
Last edited by a moderator:
Sober
Yote sawa, sijui kwa mifuko mingine, Kuna mifano ya wazi mtu alifanya kazi miaka 30/35 akapata 6 million!!! Unaposema pesa ziwasaidie uzeeni sion mantiki. labda serikalini. Naweza nikakuelewa kwa mwajiliwa wa kudumu serikalini lakini migodini ambapo mtu anafanya kazi kwa mkataba, sidhani kama inamsaidia lolote kumcheleweshea mafao yake.Wengi hatuandikishi biashara zetu, ni hizi ndogo ndogo za kupata chumvi na mafuta ya taa-Issue ya BRELLA kwa mtu kama huyu data ya BRELLA hamsaidii.After all hakuna pesa ya pension ambayo unaweza kuipata kubwa ya kuanzisha biashara ya kwenda BRELLA! Sijui, anyway!!
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

Mashirika yanatofautiana, mengine ni 15% mwajiri kwa 5% mwajiriwa (mfano PSPF), na Mengine 10 kwa 10 (kv. NSSF).

NB
Nimepata kufika ofisi ya NSSF pale Ubungo mara kadhaa, nilikutana na watu wengi ambao walifika pale kuchukuwa mafao yao, si kwa kuwa ni wazee bali ajira zao zimekoma na hawatarajii kuajiriwa tena. Kama sheria itaendelea kusimama hivyo, basi atakayeacha kazi leo akiwa na miaka 25 atasubiri kwa miaka 30 kuchukua pesa yake.

Mtoa Mada
, kwa maana hiyo hicho unachodai kwamba huongezeka miaka ya baadaye hakitakuwepo. Aidha, nadhani hata suala la kushuka kwa thamani ya fedha linaweza likawa na athari hasi kwa huyu atakayesubirishwa kwa miongo mitatu.

Waweza kusema kuwa katika SADAC hakuna fao la kujitoa au hata duniani ingawaje mi binafsi sina hakika na hilo maana kuna nchi nyingi tu wakiwemo wahasimu wetu wa Malawi fao hili liopo na pia wanasiasa wote ukanda wetu huu hadi kwenye pembe ya afrika penye vita nyingi nao pia mafao yao yote ni ya kujitoa.

Achilia mbali hoja hizi za kujitoa, naomba pia ikumbukwe kuwa katika kukokotoa kodi ya mapato na TRA na pesa hizi za mifuko ya hifadhi ya jamii zinakokotolewa na siku utakapoenda kuzichukua tena utalipia kodi ya mapato na hivyo kulipa mara mbili. Pili kwa wanaosifia kutokuwa na fao la kujitoa ni lazima waombe TUCTA ipiganie haki nyingine, kila mfanyakazi kupata ajira ya kudumu hadi afikishe miaka 55 hata akifanya kosa asifukuzwe, vinginevyo katika nchi kama zetu ambamo 'private sector' inakuwa kwa kasi na miradi inakuja ni ya muda mfupi (Usisahau miradi kama ICAP, IRC, Red Cross, World Vision n.k ni mashirika yenye wafanyakazi wengi lakini hayabanwi na sheria kwamba waendelea kutoa huduma (kwa maneno mengine kuisaidia serikali katika majukumu yake). Wanaweza muda wowote wakahamia hata Kenya au bara lingine kabisa. Wakiondoka na huku kuungua kwa majengo yetu nawe una miaka 19 uliajiriwa kwa mwaka mmoja kuhakiki wakimbizi huko Nyarugusu nao wakahamia Syria wewe mafao yako utajapewa na akina nani? Kumbuka pia sheria za ajira hapa kwetu zinasema mara moja ukiajiriwa uingizwe kwenye mifuko hiyo na mkataba ni kati yako na mashirika ya hifadhi ya jamii wala si mwajiri wako.

Jingine la kukumbuka ni mafao duni wafanyakazi wanayopewa baada ya kustaafu. Mfuko huo wa LAPF unaousemea ndo ulitaka kuleta balaa kwa wahadhiri wa vyuo vikuu maana walikaa miaka hiyo kuanzia wana miaka 24 hadi wakafikisha miaka 60 halafu kuja kuangalia mafao yao ni milioni 18 na pension kwa mwezi 50,000 na unapewa baada ya miezi sita kwa hiyo kwa mwaka ni laki 6 tu...ndo unataka watanzania tuzeeke tukiwa na mafao ya hivyo? Kwa taarifa yako hata serikalini tayari imefuta sheria hiyo kwa upande wa walioko migodini na hivi punde itafuta na kwa wengine...vinginevyo hatuishi kufuata sijui Kenya au SADAC tunaishi kufuata uhalisia wa maisha ya mtanzania.
 
Sober Ninavyofahamu mimi mtu akistaafu analipwa pension kwa mitindo miwili.
Njia ya kwanza ni ile ambayo naweza kustaafu nikiwa na miaka 40 nikaamua kuchukua hela zangu zote na hata nitakapofika umri wa miaka 55 sitapewa tena kitu. Hapa nakuwa nimejitoa moja kwa moja baada ya kupewa hela zangu zote.
Njia nyingine ni ile ambayo unapewa hela zako kidogo na zile zinazobaki basi utakuwa unazichukua kidogo kidogo utakapofika umri wa miaka 55.
Sasa kinachoonekana hapa ni kwamba hakuna kupewa hela yeyote mpaka nifikishe miaka 55. Hii sio sahihi kabisa
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada huna jipya! Ni matusi kutuambia 95% au 90% tumeshindwa kuitumia hiyo 5% /10% itatusaidia nini? Unashindwa kuelewa kitu kimoja, hiyo inayobaki 90% ni taxble pay, baada ya ku-calculate kodi unatoa hiyo kodi na unapata Net Pay, hiyo ni mosi.

Pili, elewa kuwa, formula ya ku-calculate mafao ni kandamizi sana, na kwa taarifa yako, jisumbue kidogo tu na ufanye mahesabu mfano. umefanya kazi Miaka 30 na Total Contributions zako ni Shs. 150 Millioni. Tafuta hapo Lumpsum amount payable ni kiasi gani na monthly pensionable amount ni kitu gani. Halafu jiulize mwenyewe kwamba, pesa hiyo time value of money ina kuwa taken into account or not. (Fikiria kuwa pesa hiyo ulichangia tangu mwaka 1982 mpaka 2012) Je thamani ya pesa yako leo hii 2012 ni sawa na ile ya mwaka 1982? Ukichukulia a constant contribution kuwa kila mwezi ulikuwa unachangia Tsh. 416,666.67 (mika 30 ni sawa na miezi 360). Hapa bado tunapigwa changa la macho tu, kwani walitakiwa kuja na formula mpaya mapema na kuwaeleza wafanyakazi kuwa hiyo formula itakuwa nzuri, na siyo kupitisha sheria halafu wanadai watakuja na formula nzuri ya mafao, hakuna kitu hicho hapa TZ.

Point ya tatu, mimi nilifanya kazi kwa miaka 6, nikabaili mwjiri na kuchukua mafao yangu, na nikajiunga na pension fund nyingine.

Huyo mshiko nimetumia kumalizia nyumba yangu na maisha yanaendelea! Sasa nikuulize, ningeacha kazi na kujiajiri na hiyo pension niisuburi for the next 30 years, hiyo pesa ningeweza kumalizia kibanda changu? (Consider time value of money), nafkiri ningeishia kununua mifuko hamsini tu ya Cement, ha ha ha ha!

Kila mtu ana matakwa yake, tusikazimishane, kama wewe unategemea kuishi miaka 70 ni wewe, wengine wamekata tamaa na wanataka kula raha, fainali itajijua yenyewe mbele ya safari. Mfano mzuri kwa hili ni kuwa, wewe unaweza kuona maisha ni kujenga, mwingine hana fikra na filisofia hiyo, anachojua ni kuendesha magari mazuri na kupiga vyombo!

Tusilazimishane kusubiria hiyo pension, cha muhimu ni SSRA kuja na Formula nzuri iatakayo wafanya wafanyakazi wavutiwe kusibiri pensioN, na si kwa kulazimishana.

WEWE SUBIRI HIYO PENSION YA KITANGANYIKA UONE KAMA UTAWEZA KUCHEZA NAYO KWENYE FUKWE ZA ZANZIBAR WAKATI WA UZEE WAKO, UNACHEKESHA!
 
Mkomamanga
Mkuu Mkomamanga,
Hivi unarejea nilichoandika mimi au...? Nadhani unamjibu Sober, hivyo ungem-quote yeye.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani rafiki yangu hujawahi fanya kazi sekta binafsi ndio sababu unashikilia theory zisizoendana na ukweli wa maisha ya mtanzania wa kawaida.
  1. mishahara ni midogo sana
  2. hakuna uhakika kwamba utakuwa kwenye ajira kesho, ama mwajiri kakuchoka au kampuni imekufa
  3. miaka 55/60 kwa mlalahoi anakuwa amekongoroka sana, hivi unafikiri pension atakayolipwa na nssf ni sh. ngapi? wakati huo hana msingi wowote maana aliachishwa kazi akiwa na miaka 35 hajajenga, watoto hawajasoma, hana shamba hana mradi - ukitumia weledi (professionalism) katika kutoa maamuzi lakini pia uwe na huruma kwa watu kwa kuangalia ukhalisi wa mambo
Matatizo yameanza baada ya kutaka kuifanya mifuko hii yote iwe sawa, wale wazee waliokuwa wameamua sheria za nssf ziwe tofauti na ppf na pension ya serikali walizingatia haya niliyoyaeleza hapa, ndio maana fao la kujitoa limekuwepo nssf siku nyingi tu.

Umetoa hoja ya mifano ya mifuko hii inavyofanya kazi nchi nyingine, uko sahihi kabisa. Ila ukitaka kuiga mfumo wao iga kila kitu kuanzia sheria za kazi, hali yao ya kiuchumi, fursa za kujiajiri na kuajiriwa tena baada ya ajira ya mwanzo kuisha.

ushauri wangu serikali isitishe matumizi ya sheria hii mara moja, halafu ifanye upembuzi yakinifu na wa wazi ili watu wengine wasiumizwe bila sababu.
 
Sober
Mtoa maada huna akiri inamaana kama nchi nyingine zinagandamiza Raia wake na sisi unataka tukopi tu umeniudhi sana! Mamayo zako (Kumradhi wasomaji wenzangu imenibdi nitukane tu ili hasira ziniishe)...nahic hili jamaa litakua ni Libunge tena la CCM manina zako wewe mbinafisi mkubwa usiye na chembe ya huruma ungekua mlala hoi usingediliki kusema hayo shezi type...akiri kama ya Lusinde!
 
Last edited by a moderator:
Sober, maelezo yako mazuri sana na umegota kwenye sheria lakini kitu kimoja tu umesahau au kushindwa kukizungumzia.. Hizi Social Security za Bongo zote ni wizi mtupu, ni biashara ambayo inanyang'anya wafanyakazi na watumishi haki zao, ni wizi kama wa mkoloni na hivyo ndio maana Mnyika anaomba option ya watu kujitoa kwa sababu Hii sio tena Social Security ni Unyonyaji mkubwa sana - Na nitakwambia kwa nini.

Mtu anaweza Tsh Millioni 10 leo baada ya miala 35 ya Utumishi (started at 20) unategemea kumpa zile zile Mil 10 ambazo thamani yake wakati huo itakuwa sawa Tsh 100,000 wakati huo - Hii haki kweli? Wakati hizo PPF, NSSF, LAPF na kadhalika wamewekeza fedha za hawa walalahoi kwenye majengo ya kifahari na kupangisha, ambayo yanapanda thamani kila mwaka lakini thamani hiyo hamfikii mwanachama..Wakati fedha za mwajiriwa mwanachi inashuka thamani kila mwaka, wakati fedha yake inaenda kujenga miradi ya shirika na serikali ilokwisha kusanya kodi yake toka mshahara inaendelea kumnyonya mwananchi hadi kwenye pension yake kwa shrika au serikali. I mean ifike mahala tuwazawadie wafanyakazi wetu, Social Security should mean good thing kwa Mtanzania.

Na pengine nadhani hivi vyombo vyote vya Unyonyaji vilazimike kupokea michango ya watumishi au wafanyakazi wake kwa kuthaminisha na Dollar, mkichukua Tsh 1,000 kila siku zithaminishwe kama Usd cent 75 ili miaka 35 ijayo hiyo cent 75 itathamishwa kwa chenji ya wakati huo na kwa kila mwezi, kila mwaka kila mchango wake ubadilishwe kwanza kwa dollar kuipata haki. Kama leo nina Tsh mil 10 na thamani yake ni Usd 6 leo basi mtu huyo atapewa Tsh equiv na Usd 6 ifikapo miaka 35 iyajo hata kama chenji imefika Usd moja kwa Tsh 5,000 au umeshuka na kuwa Tsh 500.

Kama haiwezekani hivyo basi kila mwanachama wa hizi financial institution.. eeeh! naziita financial institution iwauzie share watumishi wake kwa kila wanapowekeza.. Mwanachama aitwe ofisini na kuonyesha sehemu chombo hiki kinawezeka iwe kujenga ghorofa na upangishaji halafu wamuombe mchangiaji kuwekeza fedha zake huko kwa kutegema thamani kupanda kiasi kadhaa wa kadhaa..
Yaani Option ya kununua shares, wekeza fedha zako pale unapopata faida na sio wizi huu unaofanyika.Haya mashirika yanakusanya fedha za watu na kuzipfanya mtaji wao halafu nothing comes back kwa wanachama isipokuwa sikuya ku retire.. Huu wizi mbaya sana na pengine mbayua kuliko hata Mkoloni..
 
Last edited by a moderator:
Sikupenda kuongea bt Sober kiukweli uko mamtoni unakula maisha,nahic u kati ya familia chache zinazomudu kupeleka watoto ulaya.Kwanza km ulikuwa hujui,hao wazee wa kizungu kulipwa penseni ni sera za nchi zao na pension wanayolipwa ni reasonable amount,kuna mzee mmoja alistaafu mwk 1996 alikuwa boc wa NBC next to Residence Zonal director,analipwa 50,000! Km uko tz niambie inamsaidia nn?Kwanza kumbuka hyo cash si za serikari ni za wafanyakazi waachwe wazipangie matumizi wenyewe"
 
Back
Top Bottom