Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

Mh. Mnyika kwa hili umepotoka!...

I didnt know kama Mnyika ndye anapeleka hii kitu kwa bunge, lol. Nimeshasem sana humu JF kwamba level ya ujinga ni kubwa kwenye pensheni, sasa wewe mtoa mada ulitakiwaufadhiliwe na Serikali ili uendeshe semina kila mahali ukiwa na ulinzi wa polisi, maana jamaa ni vilaza wanataka pesa yao eti wakaanzishe biashara, am happy na hiyo data, sasa 67% ni wale wamesoma na kusajili kampuni, kuna vilaza kama wale wa kwenye madini watanunua daladala na kuanzisha biashara hata hawazijui na 90% watafeli, kwahiyo tunakuwa tunapoteza sana capital in that way, pesa zina ishia huko. Mi nafikiri hata ile ya mikupuo mikubwa ya 50% nayo ishushwe sasa ili ensheniiwe kubwa, make it 25% ndiyo almost world average kwa sasa, chakushangaza hapa eti huyu Lawyer Mnyika ameikamata hii issue kusogeza mbele agenda ya kuwaua watu kutokana a ujinga wao! mambo ya ajabu sana, zaidi wengine hizo hela wanapiga, pombe, kitimoto na wadada poa hadi zinaisha!
 
I didnt know kama Mnyika ndye anapeleka hii kitu kwa bunge, lol. Nimeshasem sana humu JF kwamba level ya ujinga ni kubwa kwenye pensheni, sasa wewe mtoa mada ulitakiwaufadhiliwe na Serikali ili uendeshe semina kila mahali ukiwa na ulinzi wa polisi, maana jamaa ni vilaza wanataka pesa yao eti wakaanzishe biashara, am happy na hiyo data, sasa 67% ni wale wamesoma na kusajili kampuni, kuna vilaza kama wale wa kwenye madini watanunua daladala na kuanzisha biashara hata hawazijui na 90% watafeli, kwahiyo tunakuwa tunapoteza sana capital in that way, pesa zina ishia huko. Mi nafikiri hata ile ya mikupuo mikubwa ya 50% nayo ishushwe sasa ili ensheniiwe kubwa, make it 25% ndiyo almost world average kwa sasa, chakushangaza hapa eti huyu Lawyer Mnyika ameikamata hii issue kusogeza mbele agenda ya kuwaua watu kutokana a ujinga wao! mambo ya ajabu sana, zaidi wengine hizo hela wanapiga, pombe, kitimoto na wadada poa hadi zinaisha!

Friend watch your tongue! Watu wanauchungu na pesa zao wewe unadiriki kuwaita vilaza! Hivi hujui huko migodini kuna wakali kuliko wewe? Usilolijua ni usiku wa giza. Tuache hayo lakini watu kama wameumizwa na wanadai haki yao usiwaite vilaza. Ila naelewa mkuki kwa nguruwe..., naamini ungekuwa unafanya kazi mgodini usingethubutu kusema kwa kejeli hivyo. Lakini waswahili wanasema usitukane mamba kabla hujavuka mto, na pia hujafa hujaumbwa. Nakuombea huyo muajiri anayekupa mshahara mkubwa mpaka unasaliti "vilaza" akupige chini halafu uombe kazi Barrick wakuajiri halafu nikusikie ukiongea tena hivyo. tehe tehe teh
 
sober natanguliza kabisa wewe ndio umepotoka na kwa vile upo kazini bado hujui ya kesho. hayo mashirika hayana zaidi ya miaka 5 mbele kwani wamekopesha mabilioni ya fedha za Wanachama kwa kujenga vitu ambavyo havirejeshi michango yao (ujenzi wa UDOM, UKUMBI wa BUNGE, makaa ya mawe KIWIRA ununuzi wa Majengo ya Quality nk)
  • Hivi kwa nini hela ya mfanyakazi ming'ang'anie na kuipangia biashara zisizo na faida na mchangiaji akapata riba?
  • Ni mishahara ya kiwango gani mnayojilipa nyie Wafanyakazi na wakurugenzi wa mifuko hii, Mfanyakazi wa kima cha chini anakopeshwa mpaka milioni 15 je?atazirejesha lini fedha hizo za wachangiaji?
  • Mnawalazimisha wafanyakazi wa Sekta zote wachangie hata km Mashirika yao au taasisi zinaelekea kufa (Mimi ni mwajiriwa wa Chama cha ushirika ambacho hakielekei pazuri, na kusudio ni kuacha kazi mwezi Septemba 2012 kwani Mkataba wangu na chama changu ni miaka 2 tu na mwezi Septemba mwaka huu ni mwisho. Sasa unaniambia nisubiri miaka 21 mbele nitakapofikisha miaka 55 ndio mtanilipa je huo sio wizi?
  • Bado kuna Wafanyakazi wa benki za NBC na NMB toka miaka ya 1995 mpaka leo hawajapewa na wana Kesi mahakamani kupinga kipengele hicho cha miaka 55 (Shahidi ni kaka yangu aliyefanya NMB Mtendeni Dodoma)
Mwacheni Mnyika awatetee Wananchi kutokana na makucha ya mifuko hiyo mm ntamuunga mkono waache wachangiaji wapewe pesa zao msimtabirie Maisha, eti atakuwa maskini atakapofikisha miaka 60

Namshukuru Mh. Jaff kwa kufuatilia jambo hili na kushinda hawa walikuwa Wezi tu
 
You must give yourself a price, hata nikifanya kwenye mgodi wa makaa ya mawe pesa hii ni ya hifadhi yangu nikizeeka, hapo ndiyo nahitaji kuishi sasa, kuna shida nyingi uzeeni, kuumwa mara kwa mara, ukiwa mzee ndiyo utajuwa ninachosema hapa. Mtu pesa yako mwenyewe una haraka ya nini? umasikini wa wazee kule kijijini ni mkubwa ni kwasababu hawana pensheni, sasa jasho lako kwani kuna mtu amekula hili jasho? hakuna hata mmoja anatumia pesa ilwe ni contract, ukifikisha umri unapewa heal yako, au ukifa wategemezi wako wanapewa hela yako, ndiyo utakutamaisha yanendelea that way. Ufe huku umekula hizo pesa huku nyuma familia yako inaishije? fikirieni kidogo siyo kutumia masaburi hapa. PPF wanasomesha watoto wa watu waliuokufa, imagine kama wangekuwa wamejitoa? wala sikubembelezi huu usomi wenu uchwara sana, niambie mnataka kuendelea kuzaa watoto wa kuwategemea mkizeeka? utaanzisha biashara sawa lakini you are taking market risks etc, the value of your business itaongezeka kutokan na market inavyoenda, kuna uwezekano hata kama ni mdogo wa kupata hasara, a chance is just a chance, unaweza filisika, sasa hii ni akiba wanasema hata kwa kiswahili akiba haizozi, mmesoma wapi nyinyi. Mnaendesha ujinga humu acheni hizo. Mi namheshimu Mnyika sana angeachana na hii kitu kabisa, mafao ya kujitoa hakuna, ila ni hasara kubwa. Hutaki unataka ndiyo hivyo, na usinitishe hapa wewe siyo mungu na ni ukilaza kudai kujitoa badala ya kulipwa mafao.

Friend watch your tongue! Watu wanauchungu na pesa zao wewe unadiriki kuwaita vilaza! Hivi hujui huko migodini kuna wakali kuliko wewe? Usilolijua ni usiku wa giza. Tuache hayo lakini watu kama wameumizwa na wanadai haki yao usiwaite vilaza. Ila naelewa mkuki kwa nguruwe..., naamini ungekuwa unafanya kazi mgodini usingethubutu kusema kwa kejeli hivyo. Lakini waswahili wanasema usitukane mamba kabla hujavuka mto, na pia hujafa hujaumbwa. Nakuombea huyo muajiri anayekupa mshahara mkubwa mpaka unasaliti "vilaza" akupige chini halafu uombe kazi Barrick wakuajiri halafu nikusikie ukiongea tena hivyo. tehe tehe teh
 
Sober
umetoa hoja kisomi zaidi hongera nimekubali tatizo tu utapata matusi kwa kuwa umegusa jini la watu
 
Last edited by a moderator:
Sober
I like your comment

ingawa kwa kiasi haujawa fair na umemuaccuse mtu isivyo halali kwa sababu

1. Mnyika ameomba radhi kuwa wabunge hakufanya kazi kama ilivyotarajiwa maana ilibidi apeleke jedwali la marekebisho na ameweka wazi kuwa haikuwemo

2. SSRA haijawahi kufanya research na kuweka wazi(share) kwa kiasi gani hiki kipengele kina athiri uhai wa mifuko na ustawi wa wanachama wanapofikia uzeeni.

3. sheria za tanzania haziangalii mahitaji ya watanzania, ndio maana sheria na mifumo ya serikali inaiga Uingereza pasi kuangalia waTZ kwanza.

4. Jambo muhimu kuliko yote juu ya sheria hii haikufuata process muhimu ndio maan wadau wanailalamikia ingawa hili nalo lilibidi liulizwe wakati wa kuchangia, wabunge hakufanya wajibu wao simple na ni kosa lao pamoja na Katibu wa Bunge.

Lakini pia Mnyika ameweka wazi hakuunga mkono kifungu wakati wa kupitishwa sheria, anyway najua utasema hatuwezi kuthibitisha hilo na ni kweli na hii sio kosa lake... america kila mbunge anajulikana aliunga mkono sheria ipi na alikataa sheria ipi sio huku ndio na Sio, ila nampa benefit of the doubt kutokana na mchango wake April 13 na kuwa ni mpinzani its obvious atapinga,

To declare interest, Mnyika ni Mbunge wangu, na mimi si Chadema wala CCM pia ni muathirika wa kipengele hiki. na nakipinga kwa sababu
1. hatuna supporting system kwa mtu anayeachishwa kazi(no unemployment benefits) ambayo wenzetu wanayo.
2. Mortgage rate ni zaidi ya 15%, it wont be incentive kupata hiyo loan
3. halafu imeassume kuwa wote wanaofanya kazi watakuwa na hiyo kazi hadi wakistaafu
4. kuna uwezekano mkubwa wa kubadilisha NSSF na kuipa kazi ya Benki, then more risk kwa kwa hela za wanachama.
5. na endapo watatumia fedha hizo kama colateral mtu akidifault hizo loan, lile lengo la kuwahifadhi wanachama halitotimizwa,

Sheria should be chaged all of it.

CHEAP popularity? I still believe kuwa MNYIKA is one of the most appreciated Politician in the Tanzania na anajua hili bado litabaunce, but it is worth to let the debate continue

for Policy change in any country the most important thing TO LET THE DEBATE CONTINUE kumbuka hilo kwa sababu debate ikifa THE ISSUE DIES AS WELL
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwanza unaongea kitu ambacho haukifahamu.
naomba nipe link ya NSSF ianyosema mwanachama atachangia 5%. Mimi ni mwajiriwa na ni member wa NSSF na nilijaza mkataba from the first day naajiriwa. Kwenye fomu yao wameandika kabisa kuwa ninakatwa 10% ya mshahara wangu na mwajiri ananichangia 10% hakuna 5% wala 15%.
Bado nakukumbusha tena kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya mshahara wa kila mwezi na pesa ambazo ulikuwa ukizihifadhi kwa miaka mingi.
Kumbuka ni pesa hizo hizo ambazo unaziona ni ndogo ndizo serikali inazichota na kuzifanyia projects za kifisadina hatimaye inashindwa kuzirudisha.

Nadhani atakuwa amekosea, mie mwenyewe ni NSSF nilikuwa nakatwa 10% itakuwa PPF ndio kama sikosei ni 5%. Ila hoja ya mdau ni nzuri kama utaendelea na ajira mpaka ufikishe hiyo miaka na kiukweli kwa calculation ukilipwa mafao yale ya mkupuo ni ela nyingi kweli lakini tatizo kwa waliopo kwenye sekta binafsi ni issue kazi ni za contract unaweza kupiga kazi ya miaka minne wasi-renew hivyo kama ukikaa kipindi kirefu bila ajira unakuwa frustrated hasa ukizingatia una hela zako nyingi umechangia kwenye mfuko na kiukweli kama hujafikisha michango 180 ambayo ni miaka 15 sidhani kama utapata pension maana ndivyo walivyokuwa wanatoa semina nakumbuka labda kwa hii miongozo mipya watatupa utaratibu mwingine wa pension.

Kuna watu wanafanya sekta binafsi kwenye ajira ya mikataba kwa malengo binafsi na anajua kabisa kutokana na experience yake atalipwa mshahara mzuri na endapo atapigwa chini NSSF yake itakuwa ndio security endapo kama akikaa muda mrefu bila kupata ajira, si mnajua watanzania walio wengi wameandaliwa kuajiriwa unakuta mtu analipwa vizuri lakini hana shughuli nyingine ya kumwingizia kipato wengine wanaweza kuwa na idea ya kutaka kufanya biashara lakini mwajiri wake anambana mpaka muda anakosa wa kufanya shughuli nyingine.

Sheria ina lengo zuri ila haikuangalia KIPENGELE CHA KWA WALE WANAOBANGAIZA SEKTA BINAFSI EITHER HAWAJABAHATIKA KUPATA AJIRA ZA KUDUMU AU VYOVYOTE VILE je ikitokea mkataba umeisha kila akituma application zinadunda kwa miaka kadhaa afanyaje na ndio maana zamani ilikuwa endapo huyu mtu akakaa miezi 6 bila ajira sheria ikamruhusu kujitoa lakini kama atabahatika kupata ajira anaendeleza michango yake.

Watu wanalalamikia hii sheria si kwamba hawaoni umuhimu wake bali imeanza kutekelezwa wakati kuna ambao mikataba yao imeisha hivi karibuni na walikuwa wamejiweka tayari kuchukua mafao yao (si unajua tena kama unategemea kupata kitu baada ya iezi kadhaa hata akiba yako unakuwa umeitumia kwa shughuli zingine ili ukipata kitita unaendeleza).

Kwa mtu mwenye ajira permanent hili halijamgusa ila wale wa mikataba ya miaka 2 unarudi mtaani miezi 6 no employment ndio wanaumia.
 
Mimi naungana na Mh Mnyika kwa nguvu zote. Mifuko hii imekuwa ni ya kiunyonyaji bila kutoa mafao yanayolingana na hela ya mtu aliyowekeza miaka yote.

Hivi shilingi inavyoanguka, baada ya miaka 30 unachopewa ni sawa na hakuna kabisa. Unapongojea; kama hukupata hela yako wakati una nguvu utakuja kuifanyia nini wakati huo umezeeka?

Mifuko ya jamii inakuwa na uchungu na maisha ya wafanyakazi ambao ni asilimia chini ya 5; je hao wengine wote wanajua wanaishije uzeeni? Mifuko hii ingeweza kuwasaidia walengwa kama ingekuwa inafuata haki na mchangiaji kuwa sehemu ya mfuko kama kuwa na share nk.

Kama mifuko hii ina tija, iweje kila leo kufikiria kuongeza miaka ya kustaafu? au kufanya kazi kwa mikataba?? Jamani mifuko hii ni ya kinyonyaji kupita kiasi. Kama sivyo watu wangefurahia kustaafu..
 
Point ya Sober ni nzuri ila tatizo hakuna exception kwa hili maana tupo wahanga wengi kwenye hili jambo hasa sie wenye mikataba ya kudunduliza kila ikifika mwisho wa mwaka unasikilizia kama uta-renew mkataba or not.

Ukiona watu wanalalamika sio kwamba hawapendi kuweka hela mpaka miaka 60 ila kutokana na nature ya kazi yao ndio inakuwa shida kukubaliana na hili, simshabikii Mnyika ila nazungumzia hili fao la kujitoa katika mazingira yetu, mie siangalii pia LIFE EXPECTANCY ninachoangalia hapa ni hiki mfano umepiga kazi let say 7 years na uka-manage kuchangia kiasi kadhaa cha fedha yako labda kama 15 million ukapigwa chini labda kampuni imefirisika na wewe una miaka 35 na unajua kabisa wewe ulikuwa una malengo yako flani ukijua kabisa kwenye kampuni hii nitafanya kazi miaka zaidi ya hiyo ghafla mnapunguzwa na hii ni dharula umetafuta kazi miaka miwili kazi hakuna na balance mfukoni huna,

katika situation kama hii kweli utasubiri miaka hiyo 55 ifike ndio uchukue mafao yako kweli? kwa maana nyingine kuna uwezekano wa kuishi maisha ya shida miaka 20 ukaja ku-enjoy umeshakuwa mzee na nyumba ukute huna na hata kama wanasema wanatoa mkopo wa nyumba sijui itakuaje maana michango unayo NSSF lakini ajira ambayo ndio inatakiwa irudishe mkopo huna moja kwa moja hukopesheki maana unaweza tumia mwanya huo ujilipe mafao yao.

Unajua Ulaya japo sijafika nadhani ukiajiriwa kama wewe ni professional nadhani wana utaratibu mzuri si kama huku kwetu kampuni linaweza kuwepo leo baadae linakufa maana yake hata wafanyakazi wataathirika mfano mzuri umetoa 67% ya makampuni yaliyojisajiri BRELLA (nyuma ya pazia kuna wafanyakazi wanaoathirika).

Kuhusu hiyo 95% ambayo unasema mtu anapata na 5% anakatwa inakuaje unashindwa kujipangia maisha, hapa lazima tukubaliane unalipwa ngapi mshahara maana kama mtu analipwa laki 8 ukikata 10% NSSF na PAYE utakuta huyu mtu anapata laki 5 kwa miezi 12 ana 6 million miaka 5 ana million 30 alafu akapigwa chini (na hapa katika mchanganuo bado hatujakata karo za shule, kodi ya nyumba, umeme na maji).

Kwa situation kama hii hiyo 95% ndio matumizi hayo na huyu mtu amekaa uraiani miaka 2 anahangaika na ajira, hapa kweli huyu mtu aendelee kuteseka na watoto wakati ukimpigia hesabu kwa miaka 5 anakuwa amechangia elfu 80 ukichanganya na mwajiri kwa mwezi amechangia laki 60 kwa miaka 5 ana salio la million 9 (hapa ni halali kweli huyu mtu asubiri mpaka afikishe miaka 55?)

Hizi sheria tuangalie na mazingira yaliyopo na ndio maana wabunge wao wakimaliza tu miaka 5 wanakula mafao yote wanasepa na wao wana hela. Kama unalipwa 7 million hapo hiyo 95% unaweza ukajitutumua hata kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi maisha yakasonga mbele.
 
Huu ni mwanzo wa the silent to get violent. Hili swala ni gumu kumeza haswa ukizingatia mwenendo wa kifisadi wa nchi yetu. Maswala ya kujiringanisha na hao wazungu mnaosema tunaona vibabu vinakula bata uzeeni ni rediculous!
Kwanini msituringanishe na hao wazungu kuanzia salaries, working conditions e.t.c. mnakuja kuturinganisha nao pale tu mnapoona nyie mna maslahi.

Aisee pata chimbika hapa ohooo.
 
kuna mambo mengi yakujiuliza bila kufuata ushabiki mnyika anaweza kuwa yuko sahihi lakini pia mtoa maada usilalamike njoo na solution wala si kumlaumu mnyika
 
kuna mambo mengi yakujiuliza bila kufuata ushabiki mnyika anaweza kuwa yuko sahihi lakini pia mtoa maada usilalamike njoo na solution wala si kumlaumu mnyika

Maada ni kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi.
Topic ni Mada(sio maada)
 
Kwa maoni yangu mnyika yuko sahihi, je inakuwaje mtu aache kazi halafu alipwe baaa ya miaka 55? Suala la life expectany huitaji kuwa na elimu ya digrii kujuwa.. Ukweli ni kwamba umri wa kuishi kwa mtanzania umepungua. Hizo zingine ni mbwembwe!
 
Wadau.
Kwa mtizamo wangu, siasa katika kipindi hiki tulichopo ni Biashara / Mradi au vyovyote tunavyoweza kuiita kwa maana ya wanasiasa kunufaika na tasnia hii.
Angalia jinsi watu wanavyo-invest wakati wa kugombea nafasi za uongozi kama ubunge halafu jiulize ni wapi hizo pesa wanazotumia zitarudishwa. Ni pamoja na mishahara na marupurupu yasiyo na kodi etc.
Kwa maana hii sishangai kusikia kuwa hoja hii ya mafao ilipitishwa na kuungwa mkono na bunge. Hii inawezekana kabisa kwa maana wako bungeni kwa maslahi yao wakifikiria sitting allowances zao na sio kuwepo kwa makini kujadili hoja zinazowagusa wananchi.
Hivyo basi, kutegemea wawakilishi hawa kusimamia maslahi ya wananchi ni kujidanganya, inabidi kutafuta njia mbadala ambayo sijaijua bado kwa vile tuna uwezo mkubwa wa kuongea na kulalamika chinichini bila kutekeleza kwa vitendo - Nguvu ya Umma!
 
Mimi nashauri tuweke hoja ya kulivunja Bunge maana wabunge walipitisha Sheria ambayo haikubaliki wala haitekelezeki. Ni kandamizi katika mazingira yetu ya kitanzania ambapo hakuna employment security. Fikiria Mfanyakazi wa Baa analipwa shs 80000 kwa mwezi. Anachangia elfu 8 na mwajiri elfu 8 jumla ni 16 kwa mwezi. Akidumu sana kazini ni miaka 2 tu. Huyu atanufaika vipi na sheria hii?? Ni unyonyaji kwake?? Afadhali angeipata akajianzishia hata kibanda cha kuuza nyanya.
 
Mkuu mmeshaambiwa kuwa hamna sheria ya mfuko wowote inayoongelea hilo fao la withdrawal. SSRA walichofanya ni kama reglator ni kulipiga stop tu!

Mnyika kakosea kuingilia kitu asichokifahamu kwa ajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa. Asione wengine waliokaa kimya kuwa ni wajinga.

Kwa hiyo hilo fao lilikuwepo illegally?
if yes, so unakubaliana kua tuanze kulijadili upya, but waliokua wakitoa hilo fao "illegally" hapo kabla wawajibishwe?
 
Mnyika ange raise hii concern yake wakati hii sheria ikipitishwa. Nashangaa hakufanya hivyo. Sijui anataka ijadiliwe tena upya kwa mantiki ipi.

Naye pia tumweke kwenye hilo kundi la BENDERA FUATA UPEPO!!

Najua wewe ni walewale walioweka rehani akili zao na kuendeleza fikra mgando na kutegemea kukopi na kupesti bila kuelewa ni nini kiwapasacho kufanya. Inawezekana wewe uko SSRA au si mtumishi wa umma. Kama ungekuwa mtumishi wa umma hungesema hayo, hiyo ni hela halali ya mtumishi aliyeacha kazi, haiingii akilini niache kazi nikiwa na miaka 35 kwenye utumishi wa umma, nisubiri hela yangu kwa muda wa miaka 25. Tunafanya kazi kwa ajili ya kuweka maisha yetu katika hali nzuri, sasa kama kuna watu ambao hawawekezi wakitarajia hizo hella za pensheni, basi isiwe adhabu kwa watu wengine. Tumefika hapa tulipo kwa sababu ya watu kama wewe ambao akili zao zimevilia wanaenda nchi za wengine na kuchukua sheria za huko bila kulinganisha mazingira yanayotawala sehem hizo.
 
Magu
Umeelezea vizuri sana na analysis yako nimeipenda. But kuna vitu tunatofautiana kidogo.

Kwanza kumbuka kuwa nia ya compulsory pension scheme ni kwa ajili ya kukusaidia wakati wa uzee au kipindi ambacho huna uwezo wa kufanya kazi. Kufanya withdrawal ni kinyume na maana ya scheme yenyewe. Tungekuwa na voluntary/supplimentary schemes, ndio mtu ungeruhusiwa kutoa mafao yako muda wowote na pension yako ingetegemea na performance ya hiyo scheme.

Kuhusu formula, kila mfuko umeanzishwa na sheria yake na kila moja wakati wa kuanzisha walifanya analysis ya kutosha wakaona formula inayofaa ni ipi. Ukiangalia mifuko yetu, formula inayoumiza ni ya NSSF ambayo ni ya muda mrefu, ikufuatiwa na PPF ambayo ikikuja baada ya NSSF. PSPF na LAPF formula zao ni nzuri kwasabu mifuko ya hivi karibuni. Nafikiri hili suala SSRA wameshaliona na mifuko husika inarevise formula zao.

Sikubaliani na wewe kuwa actorial valuations zinaonyesha kuwa mifuko inakaribia kufa. Ukiangalia mifuko mingi inaidai serikali yetu kiasi kikubwa cha fedha. Ukijumlisha deni la serikali kwenye hesabu za haya mashirika unaona bao haya mashrika going concern yake ipo vizuri.

Kuhusu kuwekeza kwenye projects ambazo payback period yake ni ya muda mrefu, kumbuka kuwa pension fund zinawekeza kwa ajili ya kufulfil long term obligations. Wanachofanya ni matching ya cashflows zao na obligations zao. Nafikiri wanafanya vizuri kwenye portfolio zao na mixture of short term na long term assets ndio maana hatuwahi kusikia mfuko wowote umesuffer liquidity problems.

Hapo kwenye Red n bolded, naomba unifahamishe ili kunitoa wasiwasi je serikali inaweza kwenda kuomba misaada kwa wafadhili kwa ajili ya kulipia hili deni lake kwenye mifuko ya jamii? Nauliza hivyo nikijua kuwa serikali yetu ina records nzuri sana katika kuomba misaada na ufisadi.
 
I didnt know kama Mnyika ndye anapeleka hii kitu kwa bunge, lol. Nimeshasem sana humu JF kwamba level ya ujinga ni kubwa kwenye pensheni, sasa wewe mtoa mada ulitakiwaufadhiliwe na Serikali ili uendeshe semina kila mahali ukiwa na ulinzi wa polisi, maana jamaa ni vilaza wanataka pesa yao eti wakaanzishe biashara, am happy na hiyo data, sasa 67% ni wale wamesoma na kusajili kampuni, kuna vilaza kama wale wa kwenye madini watanunua daladala na kuanzisha biashara hata hawazijui na 90% watafeli, kwahiyo tunakuwa tunapoteza sana capital in that way, pesa zina ishia huko. Mi nafikiri hata ile ya mikupuo mikubwa ya 50% nayo ishushwe sasa ili ensheniiwe kubwa, make it 25% ndiyo almost world average kwa sasa, chakushangaza hapa eti huyu Lawyer Mnyika ameikamata hii issue kusogeza mbele agenda ya kuwaua watu kutokana a ujinga wao! mambo ya ajabu sana, zaidi wengine hizo hela wanapiga, pombe, kitimoto na wadada poa hadi zinaisha!


Kuna tetesi kuwa mifuko ya jamii itapunguza wafanyakazi kwa ajili ya kubana matumizi. Sitashangaa nikifahamu kuwa wewe au mwenzi wako ni miongoni mwa wahanga watarajiwa.
 
Kaka ulichokiandika hakiingii akilini kabisa kwa nchi maskini kamahii,unyanyasaji na unyonyaji uliokithiri,ukandamizaji,na mengineyo yanayoendana na hayo nilokwambia.Huwezi kulinganisha Tanzania na nchi nyengine za kusini mwa jangwa la sahara. Eti nisichukue changu paka nitimize miaka 55 ama 60. je nikizipata nikitimiza miaka hiyo nitazifanyia nn cha maana zaidi ya kusubiri kifo kutokana na magonjwa na matatizo mbalimbali nilokutana nayo wakati nipo kijana? Kwanini nisichukue mapema nikiwa na umri wa miaka32 ili nifanye yale ninayoona ni ya msingi nikiwa na umri husika? Tusidanganyane nchiyetu bado haijajipanga kwa maswala kama hayo.
 
Back
Top Bottom