Elections 2010 Mh. MDEE TEKELEZA AHADI ZAKO WANANCHI HATUKUELEWI AISEE

Huyu Mdee hana hela ya kujenga barabara.. Inabidi aibinye serikali na hii ya CCM lazima achemke..angalau aonyeshe kuwabana waskie aibu basi... Nilisahau kuwa namimi huyu ni mbunge wangu eti...! lol itabidi nifwatilie ahadi zake, inawezekana Kinyambiss nikaingia kwenye kinyan'ganyiro 2015..hehehe. ( I am just extra happy today JF, dont mind me).
 
huna akili wewe. unaambiwa mdee wewe unamuongelea kikwete; Pambaf..ungekaa kimya na copy and paste yako hiyo

78. Watoto wataenda kufanya elimu ya Mazoezi ya masomo ya sayansi Mwezini --- Cholesamvula

80. Polisi watakuwa wakitumia Helicopter ili kupunguza foleni -----Kikwete alitoa ahadi hii kule Msoga, Chalinze
 
AHADI za Mkwe.re - ALIITOA AKIWA WAPI...


  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Asante sana Babuuuuuu!
 
Tunasikitishwa sana na style ya uongozi ya Mh. Mdee ( Mbunge wa kawe). Wakati anaomba kura alikuwa mnyenyekevu ila baada ya kupata ubunge amekuwa sasa malkia kwa wananchi wake badala ya kuwatumikia kama alivyo ahidi. Nakumbuka moja ya ahadi zake wakati wa kampeni ni kutengeneza barabara ya msasani ambayo ina anzia hapa Tanesco na kuzunguka eneo la msasani kwa mamwinyi ndani ya miezi mine. Ila mpaka sasa hakuna lolote na barabara ile inazidi kuharibika. Sasa Mh. Mdee mbona umeahidi kitu ambacho hukiwezi ? sie tulikuchagua ututumikie sisi au ufanye u sista duu wako ?. Tafadhali acha huo utoto wako na tekeleza ahadi zako, hatukuelewi badala ya kushughulikia kero zetu wewe kila siku uko kwenye maandamano ya cdm

Afanye kwa bajeti gani?? Uchaguzi uliisha lini,
 
Mliambiwa mkichagua mbunge mtapata barabara?! lol, mmeliwa. Next time try fact pills.
 
78. Watoto wataenda kufanya elimu ya Mazoezi ya masomo ya sayansi Mwezini --- Cholesamvula

80. Polisi watakuwa wakitumia Helicopter ili kupunguza foleni -----Kikwete alitoa ahadi hii kule Msoga, Chalinze

sasa mzee kwa nini usifungue thread ya kujitegemea, au ndio unakataa kwamba mdee hakutoa hizo ahadi na kashindwa kutekeleza? au ndio kuamini kwamba hakuna kinachoshindikana kwa wabunge wa chadema na kikishindikana basi kuna mkono wa mtu ??
 
Mdee choka mbaya ukija suala la utekelezaji wa ahadi;
1. Anasumbuliwa na kesi ilifunguliwa na Mbatia, hana unakika wa kutopoteza jimbo
2. Muda mwingi anatumia kuzunguka majimbo mengine ya uchaguzi; mara Arusha Mjini mara leo yuko Nyamongo!
3. Anatumia muda mwingi kufikiri namna ya kuandaa na kutelekeleza mradi wa CDM wa maandamano
4. Hahudhurii vikao vya baraza la madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambako mipango huanzia
5. Hatoi ushirikiano kwa Mkurugenzi wa Manispaa na DC wa Kinondoni.

Sie wananchi wa Mzimuni ni mashahidi wa jinsi asivyokuwa na utu kwani KIPINDI CHA MAJOZI ULIOTOKANA NA MACHAFUKO YA KUGOMBEA ARDHI hakutia mguu eneo la Madale.
 
Mkuu Zing heshima mbele,

Kwa bahati nzuri huwa mimi si mtu wa kuacha mambo juu juu, japo nilikuwa Dar es Salaam kwa siku chache niliweza kufuatilia issue hii na niliambiwa funds za kutengeneza barabara za msasani, ile ya pembeni ya Tanesco, nyuma ya ofisi za Zantel hadi maandazi road pamoja na mitaa ya osterbay na masaki etc zilikuwepo na tatizo lilkuwa utekelezaji tuu, niliuliza sababu nikajibiwa kuwa wanaanza kwanza na mitaa ya Mwananyamala etc.

Kwa kifupi ndiyo hayo nayoweza sema.

Tunahitaji mtu atakayefuatilia kero za wananchi, kazi ya ubunge ni full time job kwa mtu makini na mwenye kujali maslahi ya Taifa lake.
Kamanda Aksante sana kwa changamoto. Si kwamba natetea uzembe .

Mkuu kazi ya mbunge ni full time time job but kama fund zimetoka basi hilo ji jukumu la jiji na wakurugenzi wake katika plan yao. Nachoona wengi wengi hatujui mamlaka , wajibu na kikomo cha wabunge.

Na wenyewe wabunge wengine hawajui kikomo cha madaraa yao. Kama kazi ya hiyo bara bara anayosema mleta mada Anaweza kupata na jibu kwa hara haraka ni diwani wa eneo husika na si mbunge. Kiutekelezaji na kiufutaliaji kwa hii secific case ya bara bara mbunge hapo ni 2nd best. Hapa siongeli siasa naongela taratibu za kitendaji.

Unaona wewe umeweza kufutiia na kupata jibu inawezekana mleta mada hajui hata number ya diwani wake. Nachojua mimi madiwani ndo wana plan na kupitisha badget za matumizi ya miradi fulani ya mendeleo. Kwa hii case wa kumfatilia nrudia si bunge uienda kwa mbunge ni sawa but the best ni diwani

Ingependeza Jf ikaazisha database ya official contact ya viongzi wte wa kisiasa.
 
Mdee choka mbaya ukija suala la utekelezaji wa ahadi;
1. Anasumbuliwa na kesi ilifunguliwa na Mbatia, hana unakika wa kutopoteza jimbo
2. Muda mwingi anatumia kuzunguka majimbo mengine ya uchaguzi; mara Arusha Mjini mara leo yuko Nyamongo!
3. Anatumia muda mwingi kufikiri namna ya kuandaa na kutelekeleza mradi wa CDM wa maandamano
4. Hahudhurii vikao vya baraza la madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambako mipango huanzia
5. Hatoi ushirikiano kwa Mkurugenzi wa Manispaa na DC wa Kinondoni.

Sie wananchi wa Mzimuni ni mashahidi wa jinsi asivyokuwa na utu kwani KIPINDI CHA MAJOZI ULIOTOKANA NA MACHAFUKO YA KUGOMBEA ARDHI hakutia mguu eneo la Madale.

Akihojiwa mbunge wa chadema, watakuja juuuu kama moto wa kifuu na kudai wanaonewa, una chuki mara hivi na kukuita majina meeengi. lkn ukweli unajulikana, huyu amezidi usista duu na anayebisha na abishe
 
Week iliyopita nilipata fursa ya kwenda katika hotel ya HILTON HOTELMasaki Dar es Salaam kwenye kikao cha ku-promote uwekezaji Tanzania na baadhi ya wawekezaji katika sekta ya nishati na madini.

Barabara ya kutoka chole road kuingia HILTON HOTEL ni mbaya sana, nadhani ni barabara mbovu kuliko zote katika jiji la Dar es Salaam, ilikuwa ni aibu kubwa kwa wawekezaji tuliowaleta nchini ilikuangalia nafasi ya kuwekeza, Masaki ipo Kawe, Huyu dada asirudi tena 2015, CDM wameshindwa kazi, na Kawe naweza kusema ni wilaya ngumu sana kwa mbunge muelewa, siyo wilaya ya kuikimbilia, nilibahatika kupita maeneo ya msasani barabara ya shoppers malls kulikuwa na mto kama siyo bahari ya maji machafu ya mvua.

Wananchi wa Jimbo la Kawe inabidi mfanye maandamano ya kushinikiza kuondoka kwa Mbunge wenu.

huyu rita yeye alifanya nini? Kwa miaka yote aliyokaa kawe? Iweje miezi minne umlaumu dada mdee? Acha ujinga subiri miaka mitano iishe alafu uulize amefanya nini
 
huyu rita yeye alifanya nini? Kwa miaka yote aliyokaa kawe? Iweje miezi minne umlaumu dada mdee? Acha ujinga subiri miaka mitano iishe alafu uulize amefanya nini

yaani Mdee ndio kakutuma na kukwambia uwaambie wapiga kura waliomchagua wasubiri na kuendelea kuumia hadi baada ya miaka mitano ??
 
Huyu mbunge ni ovyo viwanja Vya wazi vinavyamiwa hakuna Msaada wowote anafahamishwa yuko Kimya wala afiki sehemu husika. Kippe warioba ndiye angetufaa jamani
 
Back
Top Bottom