Mh. MDEE TEKELEZA AHADI ZAKO WANANCHI HATUKUELEWI AISEE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. MDEE TEKELEZA AHADI ZAKO WANANCHI HATUKUELEWI AISEE

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by GeniusBrain, May 27, 2011.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tunasikitishwa sana na style ya uongozi ya Mh. Mdee ( Mbunge wa kawe). Wakati anaomba kura alikuwa mnyenyekevu ila baada ya kupata ubunge amekuwa sasa malkia kwa wananchi wake badala ya kuwatumikia kama alivyo ahidi. Nakumbuka moja ya ahadi zake wakati wa kampeni ni kutengeneza barabara ya msasani ambayo ina anzia hapa Tanesco na kuzunguka eneo la msasani kwa mamwinyi ndani ya miezi mine. Ila mpaka sasa hakuna lolote na barabara ile inazidi kuharibika. Sasa Mh. Mdee mbona umeahidi kitu ambacho hukiwezi ? sie tulikuchagua ututumikie sisi au ufanye u sista duu wako ?. Tafadhali acha huo utoto wako na tekeleza ahadi zako, hatukuelewi badala ya kushughulikia kero zetu wewe kila siku uko kwenye maandamano ya cdm
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Yupo bize na maandamano kwanza hehehe:biggrin1:
   
 3. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe walalamikia miezi minne, je msanii wenu wa bagamoyo aliyepanga ikulu miaka 5 na miezi 7 amefanya nini zaidi ya kuagiza polisi kupiga watu masasi za moto?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  AHADI za Mkwe.re - ALIITOA AKIWA WAPI...

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
   
 5. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Mnafiki kama wewe huwezi kuwa ulimchagua mdee.
   
 6. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yaani kujitetea kwa namna hii ni kwa kitoto saana. Mbona fulani kafanya hivi??? Ukweli Mdee hana uwezo wa kujenga barabara isipokuwa kuishauri na kuishawishi serikali juu ya umuhimu wa barabara ile.
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ile barabara ni mbovu sana, nadhani kwa wanaopita pale wataniunga mkono aisee. Basi huyu mama alitudanganya kabisa !
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  lia lia kama dingi yako magamba
   
 9. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Week iliyopita nilipata fursa ya kwenda katika hotel ya HILTON HOTELMasaki Dar es Salaam kwenye kikao cha ku-promote uwekezaji Tanzania na baadhi ya wawekezaji katika sekta ya nishati na madini.

  Barabara ya kutoka chole road kuingia HILTON HOTEL ni mbaya sana, nadhani ni barabara mbovu kuliko zote katika jiji la Dar es Salaam, ilikuwa ni aibu kubwa kwa wawekezaji tuliowaleta nchini ilikuangalia nafasi ya kuwekeza, Masaki ipo Kawe, Huyu dada asirudi tena 2015, CDM wameshindwa kazi, na Kawe naweza kusema ni wilaya ngumu sana kwa mbunge muelewa, siyo wilaya ya kuikimbilia, nilibahatika kupita maeneo ya msasani barabara ya shoppers malls kulikuwa na mto kama siyo bahari ya maji machafu ya mvua.

  Wananchi wa Jimbo la Kawe inabidi mfanye maandamano ya kushinikiza kuondoka kwa Mbunge wenu.
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  usipende kujipendekeza jiwakilishe nafsi yako mwenyewe ....!
   
 11. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dah huyu jamaa kama mara ya 3 anarudia thread hii hii, haya bana, Halima Mdee mpiga kura wako kakukumbusha lifanyie kazi .
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Subiri Flyovers !
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwambie atekeleze ahadi zake ! sio kuleta u sista duu wa kuweka miguu juu ya dash board huku hawara yake anamuendesha, hayatusaidii hayo !
   
 14. semango

  semango JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hakukuahidi wewe, aliwaahidi wapiga kura wake
   
 15. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Barabara ile inamatatizo saana. Huenda amekosea namna ya kuwasilisha hoja. Siku nyingine anatakiwa afahamu kuwa uhusiano wa mwananchi na mpiga kura ni wakati wa uchaguzi tu ukikumbushia ahadi baada ya hapo wewe unakuwa adui na mtovu wa nidhamu.
   
 16. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masa inamaana kama jamaa hajatekeleza ahadi zake basi na wengine wafanye hivyohivyo, kweli, sasa mabadiliko gani mnayopigia kelele kila siku?.
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Tumesubili miaka 50 bila maendeleo itakuwa miezi 6, tumia akili hiyo hiyo kuiuliza serikali ya Magamba juu ya ahadi zao zipo hapo juu zimewekwa na masa...
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu pita ile barabara haifai aisee ! watu kila siku wanalalamika na huyu mbunge wala halisemei lolote utasikia yuko huko yuko kule , sio siri hata watu wa cdm wa eneo lile wamekereka sana na utendaji wa huyu dada
   
 19. a

  andry surlbaran Senior Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  MIEZI 4 unaona mingi mbona huendi kumng'oa ****** mjengOni hivi huyu mzee anaropokaga eeh? Mbona pumba na kimsingi nyingi hazitekelzeki ahadi zake??? Ha ha ha nimecheka mmh mbaka ng'ombe duh kweli haya magamba plus

  mimi mkazi wa kawe na katika harakati za kampeni sikuwahi kumsikia halima akiahidi kama ccm yeye alikua anaongea facts sasa wewe miezi minne oni?
   
 20. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Rita Mlaki alifanya nini? Miaka 5 aliyokaa pale
   
Loading...