gango2
JF-Expert Member
- Aug 31, 2011
- 1,941
- 2,251
Ni takribani mwezi mmoja sasa umepita Tangu mlipokuja na magreda na magari mengi kuzindua ujenzi wa barabara ya MAKONGO "tarehe 1 November"
Sasa tunaanza kukosa matumaini tena maana mlipoondoka siku hiyo na magari hayo nayo yakaondoka, tunaendelea kula vumbi kama kawaida! hakuna hata dalili kuonyesha kuna kitu kinaendelea kwenye ujenzi huu!
Barabara hii ina hali mbaya sana kwani kifusi kilichomwagwa mwanzo kilikuwa na mawe sasa baada ya mvua kunyesha udongo unaondoka unaacha mawe hivyo ni shida sana magari kupita.
===
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Tanzania, Paul Makonda amesema barabara ya Makongo Juu itajengwa kwa kiwango la lami kwa muda wa mwaka mmoja.
Mkuu huyo wa Mkoa pia alizindua ujenzi wa barabara ya Madale yenye urefu wa kilomita sita, utakaofanyika kwa mwaka mmoja na nusu, akibainisha kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hizo kutaondoa kero kwa wananchi, kupunguza foleni kwenda katikati ya Jiji.
Ujenzi wa barabara ya Makongo Juu yenye urefu wa kilomita 4.5 utagharimu Sh8.9 bilioni zinazojumuisha malipo fidia na uhamishaji na miundombinu ya maji na umeme.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo pamoja na watendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) ni miongoni mwa walioshuhudia uzinduzi huo. Kampuni ya Jasco ndio inajenga barabara hiyo.
"Poleni sana wakazi wa Makongo Juu na watumiaji wa barabara hii, sio kama fedha hazikuwepo ila mlikosa kiongozi mwenye ushawishi na anayejenga hoja, "amesema Makonda.
Awali, Chongolo amesema kwa kipindi kirefu wakazi wa eneo hilo walikuwa wakitaniwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mtu atakayeonekana na vumbi anatokea Makongo Juu jambo ambalo hivi karibuni litakuwa historia.
Chanzo: Mwananchi