Katavi: Wananchi Wilayani Tanganyika wamlilia Mkandarasi kuchelewesha barabara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462

Wananchi wa Kijiji cha Luhafwe iliyoko Kata ya Tongwe Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wamemuomba mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayoanzia Kijiji cha Vikonge hadi Luhafwe kukamilika kwa wakati uliopangwa ili waanze kunufaika nayo.

Kolita Ndulugu, Mateja Madaha na Deogratius Nyamali ni wakazi wa kijiji hicho ambapo wamemuomba mkandarasi kuzingatia mkataba wa kazi yake maana anaonekana kusuasua katika mradi huo ambao inapaswa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Albert Laiza ni Mhandisi wa madaraja kutoka TECU amesema ujenzi wa barabara hiyo ambayo inatekelezwa kwa kiwango cha lami kuanzia kijiji cha Vikonge hadi Luhafwe utagharinu zaidi ya shilingi bilioni 35 hadi kukamilika kwake.

Mhandisi Martin Mwakabende ambaye ni meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Katavi (TANROADS) amesema kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa miundonbinu ya barabara zinazotekelezwa nacserikali ili ziweze kudumu kwa manufaa ya Taifa.

Aidha, Mwakabende amesema Mkoa wa Katavi utaendelea kuunganishwa na mikoa jirani kwa kiwango cha barabara za lami ambapo Serikali anaendelea kutangaza zabuni mbalimbali za ujenzi wa barabara za lami.
 
Back
Top Bottom