luambo makiadi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2017
- 10,709
- 8,928
Hahaha mkuu Hawa jamaa huwa Ni wabishi wanaweza bishana hata na mbuzi[emoji16][emoji16][emoji16] wazoee tu hao ... Itabidi mwaka huu mwishoni niwapele Moshi tupite Kibololoni tule kiti moto, kisha tuende Marangu tunywe mbege mpaka ushikwe mkojo kila dakika.
Nakumbuka nilikujaga na mdada mmoja tuliosoma naye yeye anatokea Singida yaani alipapenda kweli kweli yaani alikuwa ananiambia maji yapo, barabara ya lami, umeme mpaka mgombani yaani alipatukana kwao ila nikapaelewa Singida kuna Punda wengi kuliko baiskeli. Huku shule zipo nyingi kweli kweli ni wewe tu kuamua na kuchagua
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app