Wanakagera wayachukulie Maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro, kama tution ya kujifunza wapi wanakosea, na nini!! wafanye ili angalau waweze kufikia nusu ya kile ambacho Mkoa wa kilimanjaro wamefanikiwa.Maana kwenye historia ya nchi hii, jamii za watu wa mikoa hii miwili wametoa mchango mkubwa wa ujenzi wa nchi yetu. Ivyo ni aibu kwa jamii ya mkoa wa Kagera kuongoza kwa kuwa na watoto wenye utapiamlo ambao kimsingi unatokana na kukosa lishe bora, tatizo ambalo linasababisha watoto kuwa na udumavu wa akili na kimwili. Pia ni aibu kwa Mkoa wa Kagera kukosa miundombinu chochezi ya ajira, barabara za uhakika wilayani mpaka vijijini!! Vituo vya afya kila kata, masoko yaliyo katika ubora ambayo yangeweza kuchochea uchumi na watu kuvutiwa kuja kufanya biashara, mpaka leo halmshauli ya manispaa ya Bukoba haina soko kuu wala stand inayoweza kukidhi maitaji ya dunia ya leo, ni aibu sana!!!! Kwa jamii ya watu wanao jinasibu na usomi. Pia umefika wakati jamii za watu wa Kagera zikaacha uvivu, uvivu umetamalaki sana mkoa wa Kagera, wajifunze kwa ndugu zao wa Kilimanjaro wanavyo chapa kazi bila kubagua haina ya kazi, si ajabu kumkuta kijana wa Kilimanjaro ana biashara ya kuuza supu tu kwenye bar, ila ana akiba ya zaidi ya milioni tano bank, tofauti ya kijana wa mkoa wa Kagera ambaye hawezi kufanya kazi yeyote ya kutumia nguvu kisa ana mjomba wake ni jaji wa mahakama kuu!!! Ni wakati sasa jamii za mkoa wa Kagera kubadili mentality zao ili walau wafikie nusu ya maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro.
Sent using
Jamii Forums mobile app