Hata mimi nimeshangaaa yaani utadhani alikuwa na kitu kimemkaba kuhusu wahaya sasa anakitema. Anachuki kubwa na wahaya iliyo pitiliza. Maana nnachojua watanzania sote tunabaguana hata ukienda huko uchagani wachaga wanabaguana Mara huyu mkibosho Mara huyu mnanii, nipo hapa Lushoto watu ofisi za halmashauri wanaongea kisambaa mwanzo mwisho. Afu nao wanabaguana Mara huyu mumbugu Mara huyu msambaa. Sasa huyu kaifanya Bukoba kama ni sehemu isio faa kuishi watu. Afu swala la kuitwa mnyamahanga kila sehemu wanajinsi wanavyo waita wageni ambao sio wazawa Wa eneo husika mfano Mimi huku wasambaa wananiita "mnyika" wala sioni ajabu.Mkuu huyo anaye coment hivyo nadhani humuelewi vizuri. Hebu jaribu kuingia kwenye prof yake alafu uangalie posts zake na coments zake zote tangu aingie JF utajua kampeni yake hapa JF ni nini hasa! Asikupasue kichwa huyo, anatekeleza anachokijua dhidi ya wahaya. Na kila uzi unaohusu wahaya, Kagera, Bukoba huwezi kumkosa na kama hajauanzisha yeye basi amebadilisha upepo mwenyewe uzi mzima anatamba yeye.
So we mpuuze tu. Maana haiingii akilini kichwa cha uzi kinazungumzia waziri mkuu na kutumbua viongozi yeye anajitahidi kuhusisha mada na uhaya. Ukiangalia posts na coments zake hapa JF utaelewa vizuri anachokifanya
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app