Nawafaham in and out
Wanaanza kukubagua mgeni kule kwao wanaita "nyamahanga" wakimaliza wanabaguana wenyewe kwa wenyewe
Yan ni upuuz mtupu
Halmashauri Zao ukienda ni kilugha tu hadi kumebandkwa mabango "zungumza "kiswahili"
ndiona mkoa wao unazidi kuwa masikn mchawi wa maendeleo yao ni wao
View attachment 1030686
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu naona unazidi kuwaandama wahaya kwa chuki zako. Kurudi nyuma kimaendeleo kwa mkoa wa Kagera kuna factors nyingi na sio kuongea kihaya ofisini au kubagua wanyamahanga eti ndio sababu kuu. Kwani kuongea kihaya ofisini kama wanahudumia wahaya huoni kama wana facilitate communication? Ni sawa na kuongea Kiswahili unless anayehudumiwa hajui Kihaya.
Factors zilizorudisha nyuma Mkoa wa Kagera ni natural factors ambazo kwakweli haziepukiki.
1. 1978 Vita ya Kagera. Wahaya wengi wamekufa na mali zao nyingi kwa kujitolea zimetumika katika vita ya Kagera. Kwa kipindi cha miaka 3 hivi shughuli za maendeleo zilisimama huku Mikoa mingine ikiendelea na kilimo ufugaji n.k.
2. Kuporomoka bei ya Kahawa ktk soko la dunia 1978-1980s. Lilikuwa ni zao kuu la kibiashara Mkoani Kagera. Uchumi wa Mkoa ulikuwa unaenda vizuri sana kutokana na kahawa kuwa na soko zuri. Wahaya hadi leo hawaamini na vyama vya ushirika ambavyo vimesomesha wakina Sir George Kahama n.k havina nguvu tena kama zamani.
3. UKIMWI 1984. Hili janga la UKIMWI limechukua nguvu kazi kubwa ya wahaya. Ugonjwa huu kama ulikuwa hujazaliwa kwa taarifa yako hadi leo makovu yake hayawezi kufutika katika kaya mbalimbali Mkoani hapo.
4. 1994 Mauaji ya Kimbali Rwanda. Ni vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda ambayo ilileta athari Mkoani Kagera. Wanyarwanda wengi walikimbilia Mkoa wa Kagera na baadhi yao walikuja na silaha za kivita na kuanza kuendesha vitendo vya utekaji. Vitendo hivyo viliathiri shughuli za maendeleo kwa kiasi kikubwa sana na kwa muda mrefu kwani shughuli za usafirishaji bidhaa na watu ziliathiriwa. Wahaya wametandikwa viboko wakiwa uchi ktk msitu wa Biharamulo, Kasindaga n.k Wengine wamebakwa. Haikuishia hapo tu, mwaka 1994 ktk S/M Tumaini bomu lililipuka na kuua wanafunzi ambao hatujui labda leo ndio wangekuwa wanasayansi nguli ktk Mkoa huo.
5. 1996 Ajali ya MV Bukoba. Hakika mamia ya watu walipoteza maisha. 'Haitasahaulika' karibu kila kaya Mkoani Kagera iliguswa. Ukiachilia mbali nguvu kazi na mali kupotea, pia ile kasi ya kufanya biashara kati ya Kagera na Mwanza ilipungua sana. MV Victoria ndio hivyo imeharibika muda mrefu sasa, meli zilisaidia sana kuimarisha usafirishaji wa bidhaa pamoja na reli ya kati ambayo leo inasuasua. Wana Kagera na wana kanda ya Ziwa wanamshukuru sana Rais MAGUFULI kwa nia yake thabiti kabisa ya kutengeneza meli kubwa na ya kisasa ktk Ziwa Victoria. Pia wako pamoja naye ktk juhudi za kuimarisha usafiri wa reli kwa kuanza ujenzi wa reli ya kisasa kutoka DSM hadi Mwanza. Ni ukombozi wa kiuchumi kwa wanakanda ya Ziwa.
6. Mvua za Elnino 1998, hapa sitazungumza sana. Nadhani mnajua kwa namna gani shughuli za kilimo na usafirishaji zilivyoathiriwa. Ilikuwa ni mvua ambayo iliharibu kwa kiasi kikubwa miundombinu ya Mkoa wa Kagera.
7. Ugonjwa mnyauko 2000s. Hakika ni ugonjwa ambao umeathiri sana zao la ndizi. Ndizi ndicho kilikuwa chakula kikuu kwa wahaya na pia likikuwa ni zao la biashara. Wahaya hawakuwa na njaa kama ilivyo sasa. Ugonjwa huu ulitokea nchini Uganda na kwakweli hautasahaulika kwani leo wahaya wamegeukia kula ugali kitu ambacho hakikuwepo.
8. Tetemeko la ardhi, hili la juzi kila mtu analifahamu na athari zake.
Kwa ujumla athari za nilioyaeleza hapo juu haziwezi kuisha leo au kesho. Ndio maana Serikali kwa kutambua hilo inajitahidi kuja na mikakati ya kusaidia ikiwa ni pamoja na kununua meli nyingine ktk Ziwa Victoria kujaribu kurudisha hali ya zamani kwa kuimarisha usafiri wa majini, kufufua reli na zao la kahawa kwani tumeona juhudi za makusudi ktk maeneo hayo.