Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Sheria za nchi zipo wazi kabisa kwamba kunuia kuua ni kosa la jinai basi mimi naitaka Serikali iwakamate wazee wa Arumeru kwa kupanga kummuua LEMA,pindi atakapo kanyaga ARUMERU. shahidi wa kwanza awe TENDWA
 
Mie sioni sababu ya kumkataza Lema, kwenda Arumeru ni vizuri aende akaizamishe Chadema.

wewe unaongeaga pumba muda wote sijui ulisoma kata halafu mbaya zaidi hukumaliza!! sijawahiona siku hata moja ukatoa hoja inayojadilika zaidi ya ***** kila kukicha, halafu na wewe unjiita great thinker!!
 
WAZEE wa kimila wa kabila la Meru (Washili) wamekanusha madai ya kutishia kumuua Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, endapo atakwenda Jimbo la Arumeru Mashariki kwa ajili ya kampeni za ubunge.

Katibu wa Washili wa Meru, Jacob Kaaya, aliliambia Tanzania Daima jana kuwa habari zilizotolewa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, John Tendwa, kwamba wao wametishia kumuua Lema si za kweli.

Alhamisi wiki hii, Tendwa alikaririwa na Tanzania Daima akidai kuwa wazee wa Kimila wa Washili walimwambia kuwa watamuua Godbless Lema ikiwa atakwenda jimboni Arumeru Mashariki.

Tendwa katika habari iliyochapishwa na gazeti hili, alidai kuwa wazee hao walimwambia kuwa wametoa onyo hilo kutokana na kuudhiwa na mbunge huyo.Akikanusha habari hizo jana, Kaaya alisema kuwa mpaka sasa hakuna kikao cha kimila cha kabila hilo kilichokaa kujadili suala hilo, na wao kama wazee wa mila hawajawahi kukutana na Tendwa na kutoa kauli ya pamoja juu ya madai ya kumuua Lema.

Alisema wao kama wazee wasingeweza kutoa madai mazito kama hayo na kwamba huenda Tendwa alikutana na Mshili mmoja na kumweleza maneno hayo, ambayo alidai kama yalikuwapo hayawezi kuchukuliwa kama kauli rasmi ya umoja wao.

Alisema kuwa shughuli za wazee wa mila ni kulinda amani, usalama na maliasili, hasa ardhi pamoja na kuhakikisha wajane na yatima kwenye maeneo yao wanapata haki zao, na kuwa wao kama wazee wa mila hawahusiki na shughuli za siasa.

Kaaya alisema kutokana na uzito wa tuhuma hizo walizosukumiwa na Tendwa, wanatazamia kukutana Februari 29, mwaka huu eneo la Poli chini ya Mringaringa, ambapo pamoja na mambo mengine watajadili suala hilo kwa kina.

Alisema kikao cha baraza la mila kitaafiki na kuangalia uwezekano wa kuwaita wagombea wote watakaoteuliwa na vyama vyao kuwania ubunge Arumeru Mashariki katika kikao chao kinachotarajiwa kufanyika Machi 7, mwaka huu eneo la Poli.
Aliongeza kuwa lengo ni kuwataka wagombea hao kuhakikisha kuwa wanaendesha siasa za kistaarabu zinazozingatia amani, usalama, umoja na utengamano miongoni mwa wakazi wa jimbo hilo ili wananchi waendelee kubaki wamoja hata baada ya kampeni na uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Hata hivyo, kiongozi huyo alikiri kuwa Lema aliwakwaza baadhi ya wazee wa kimila kutokana na kitendo chake cha kuzungukwa na kundi kubwa la vijana wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki marehemu Jeremiah Sumari, jambo linalodaiwa kuwa liliwaudhi wazee hao.

"Kumbuka kwenye mazishi watu wanakaa kwenye vikundi wanaongea mambo yao lakini yeye (Lema) alikuwa chimbuko la vurugu, kwani alikuwa amezungukwa na kundi kubwa la vijana na picha inaonyesha kuwa alikuja kufanya kampeni," alisema Mshili huyo.

Lakini alipotakiwa kueleza endapo kuna maneno ambayo mbunge huyo aliyatamka kudhihirisha kuwa alikuwa akifanya kampeni, katibu huyo alishindwa kutaja maneno wala kueleza kitendo chochote alichofanya kikiashiria kuleta vurugu, badala yake alisisitiza tu kuwa wazee wa mila hawakufurahishwa na kitendo cha mbunge huyo kuzungukwa na vijana.

Hata hivyo, habari kutoka kwa mmoja wa washili ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alidai kuwa suala la Lema linakuzwa na baadhi yao ambao wameamua kushiriki shughuli za siasa, hivyo wanaamua kutumia nafasi hiyo vibaya.

Mshili huyo alitolea mfano kuwa wakati wakiwa kwenye kikao chao cha Februari 22 , mwaka huu Mshili mmoja alijaribu kuibua suala la Lema kwenye kikao hicho ambapo walimkatalia kulijadili kwani kikao hicho hakikuwa cha siasa.

CHILL:TANZANIA DAIMA
 
Hivi inakuaje zee zima linapokua liongo na ligombanishi?na isitoshe hiyo si kazi yake!hii nchi bwana,wazee wetu tunatakiwa tuige busara toka kwenu,ila baadhi yenu mnakua na tabia za ajabu kwy jamihi kama Yohane Tenda
 
Tendwa na magamba wameshikwa pabaya.Mbaya zaidi HIJABU hazipo!
 
Tendwa ni ganda la muwa lililotafunwa na kitupwa jalalani. CDM fungulia mashatka huyo tendwa kwa kuleta siasa za uchochzi hapo Arumeru.
Na ikiwa vurugu zozote zitatokea hapo Arumeru katika kipindi chote cha kampeni basi Tendwa ndo muanzilishi wa vurugu hizo..
 
Kwenye vitu kama hivi ndio unapojua kuwa hii nchi tuna tatizo kubwa sana zaidi ya hata tunavyofikiria...
Bahati mbaya sana wazee wengi waliokabidhiwa idara nyeti za nchi hii wanaakili kama za Tendwa.
Tutaendelea kuwa nchi ya majanga tu
 
Huyu zee linashindwa kusimamia position ambayo kapewa na mg.amba mkuu wao na akija huku arumeru wameru watamtoa macho maana vijana wote huku ni chadema na ndio maana lema alipofika katika msiba ule vijana wote walishindwa kuvumilia wakamkusanyikia maana wanamwona kama mkombozi wao kafika
 
Tendwa ni ganda la muwa lililotafunwa na kitupwa jalalani. CDM fungulia mashatka huyo tendwa kwa kuleta siasa za uchochzi hapo Arumeru.
Na ikiwa vurugu zozote zitatokea hapo Arumeru katika kipindi chote cha kampeni basi Tendwa ndo muanzilishi wa vurugu hizo..

Inanishangaza sana refa kuonyesha dhahiri anashabikia timu fulani
 
Katudhirishia ana uwezo wa kupindua kura mpaka upande wa aliyemweka hapo washinde
 
Hata sipendagi hata kusikia story zake ni ndumilakuwili!!
 
Back
Top Bottom