Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Huyu Tendwa umri unamtupa mkono, ajabu badala ya kuwa na hekima na busara anakuwa na akili kama ya mtu taahira. Kama kweli wazee wa kimeru walimwambia maneno hayo kweli kwa nini asikae nao na ku resolve tatizo hili?

Kuzungumza na waandishi wa habari jambo hili ili iweje, Lema asiende kufanya kampeni wakti ukifika? Mh. Lema hawezi kukubali, na huko CCM kazi wanayo ndo watajua kuwa kwa kumweka mkwewe EL wamepotea njia. Ngoja tusubiri tuone, kule si Igunga watu wa Meru wanakula na kushiba wanakunywa maziwa badala ya chai hivyo njaa iliyotengenezwa na CCM kule hakuna, hawaongeki au tuseme hawauzi kura yao.
Sio umri ni kisukari kilichochanganyika na kale kamdudu ndio kinamzeesha
 
Tumuombe Mungu Yehova, amani itawale mahali pale panapokwenda kufanyika uchaguzi, Arumeru
Na hila zote za Ibilisi na zishindwe katika jina la Yesu, hasa roho ya mauaji na ishindwe kabisa.
 
Nawasalimu



Leo asubuhi nimesikia habari za uzushi na majungu kutoka katika gazeti la Chama Cha Mapinduzi Uhuru pamoja na gazeti la serikali la Habari leo . Hivyo basi kilichosemwa na magezeti ya Uhuru na Habari leo ya leo tarehe 23/2/2012 ni uzushi na propaganda , Magazeti haya ya CCM yatatumika sana kipindi hiki kama yalivyotumika kule Igunga yalipojaribu kutaka kuwatenganisha watu hata kwa dini zao lakini baadae ukweli ulijulikana na ikawa aibu kwao .
Kwa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wa Taifa letu kutoka kwa mkoloni bado Watanzania wa Arumeru sio huru na Watanzania wote kwa ujumla bado wanaishi maisha magumu kama wakimbizi nje ya Nchi yao.
Ninafahamu wajibu wangu katika kupigania demokrasia safi ya Nchi yangu na wakati huu jimbo la Arumeru Mashariki litakuwa mfano wa mapambano hayo na nitakuwa mstari wa mbele bila hofu wala kumuogopa mtu yeyote na wa cheo chochote katika kupigania ukweli na haki.
Wajibu wangu na wa chama changu kwa sasa ni kutoa matumaini kwa watu wote wa Taifa letu , na tunazo sababu za msingi za kwenda kushinda jimbo la Arumeru na ni wito wangu kwa kila kijana wa Arumeru anayeishi mjini kuona fursa hii ni kwa ajili ya ukombozi wa Nchi yetu na sio Arumeru peke yake na hivyo kwenda kutoa elimu vijijini tulikoacha wazee wetu.
Jana nilikuwa Meru , wazee na vijana wamekataa kuburuzwa na siasa za CCM ambazo kwa miaka hamsini ya uhuru wa Nchi hii zimeshindwa kutatua matatizo yao bali kufikiri rushwa ya pesa kipindi hiki cha Kampeni ndio mahitaji yao ya Msingi.
Nimesikia Tendwa msajili wa vyama vya siasa naye ameanza kusaidia CCM kufanya propaganda chafu labda ni vyema akatambua wajibu wake na sio kuanza kufanya kazi za siasa za CCM ni vyema akajua kuwa yeyote anayeitetea uovu leo itakuwa hasara kwake au kwa familia yake kesho .
Mwisho . Ninajua macho ya Watanzania yako Arumeru mashariki , Ninawatia moyo wale mlioko mbali lakini mnapenda mabadiliko , sisi tulioko huku tutapambana kwa niaba yenu kufa na kupona kuhakikisha haki, usawa, na demokrasia vinapata thamani halisi bila uhuni wowote kufanikiwa , Msiogope pengine huwezi kabisa kufika Arumeru kusaidia ukombozi basi wewe huko uliko tuombee kwa Mwenyezi Mungu , hakika hatutakubali uhuni ,udhalimu , na Nguvu ya rushwa iwachagulie ndugu zetu wa Arumeru Mbunge , kama Mbunge mmoja wa CCM Mwigulu Nchemba alivyotamba jana pale katika Hotel ya Mount Meru kuwa pesa bado hazijaanza kumwagwa kwani ndio kwanza ziko njiani zinakuja. Hata hivyo Msiogope Udhalimu utashidwa Arumeru ““ Ni Afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu .
Godbless J Lema (Mb)
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye amesema Mbunge wa Arusha Godbless Lema yuko huru kufanya kampeni katika jimbo la Arumeru Mashariki kwa mujibu wa Katiba ya nchi na hakuna mwenye mamlaka yoyote ya kumzuia.Akizungumza na gazeti la Habari Leo kamanda huyo amesema polisi wamejiandaa kuhakikisha amani inakuwapo wilayani hapo.

Alipoulizwa kuhusu suala la kutishiana kukatana mapanga kwenye kampeni endapo mbunge Lema atashiriki, alisema mapanga yanatumika kufyekea majani na migomba na si binadamu.

Alisema kila mtu ana haki ya kuingia na kutoka wilayani humo, hivyo polisi watahakikisha haki hiyo inalindwa kwa kuzingatia sheria.
 
Sina imani sana na huyu Andengenye!ndo huyuhuyu aliyekuwa anamnyanyasa Lema!ndo huyuhuyu aliyekuwa anamtishia pia!sijui kama maneno yake yanaukweli ndani ya nafsi yake!Ngoja tusikilizie
 
Hivi John Tendwa ni mbunge wa chama gani vile?chama cha usajili wa vyama?
Mimi mbona sikumwelewa?
 
Hii habari ilishawekwa hapa jamvini jana! Ila basi naona unaweka msisitizo siyo mbaya.
 
Mie sioni sababu ya kumkataza Lema, kwenda Arumeru ni vizuri aende akaizamishe Chadema.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemshukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kikisema kuwa ameanza propaganda za kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Tendwa alikaririwa na vyombo vya habari akimtahadharisha Mbunge wa CHADEMA katika Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, kutokanyaga kwenye kampeni za uchaguzi huo kwa tishio la kuuawa na viongozi wa kimila (Washiri).
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alisema kauli ya Tendwa ni ishara ya kutumia madaraka vibaya kujaribu kuibeba CCM kwenye uchaguzi huo mdogo baada ya wananchi wa Arumeru kuonyesha wanakipenda CHADEMA na kutaka mabadiliko.
“Tendwa akae pembeni aache uchaguzi kwa vyama vya CHADEMA na CCM. Alikwenda kufanya tathmini na amelizungumzia jambo moja ambalo amelifanya propaganda, mbona hazungumzii rushwa iliyofanywa na CCM kwenye kura za maoni?” alihoji Mnyika.
Alisema wadau mbalimbali wamelalamikia vitendo vya rushwa vilivyojitokeza CCM na kwamba yeye kama msajili kuna sheria tatu ambazo zinampa mamlaka ya kuzungumzia hayo.
Alisema kuna sheria ya vyama vya siasa ambayo moja kwa moja inampa wajibu wa kuzungumzia rushwa kadhalika ile ya gharama za uchaguzi ambayo inampa mamlaka ya kufuatilia vitendo hivyo.
“Kama ana nia njema, vitendo vya rushwa ambavyo pia vinazungumzwa na wana-CCM wenyewe angevitolea kauli, kuacha hayo ni kutumia madaraka vibaya. Kuyaacha mambo ya msingi na kulizungumzia moja tu ni propaganda za kuibeba CCM,” alisema
Katika hilo, Mnyika alimtaka Tendwa afanye mambo mawili; kwanza atoe ripoti ya kina ya tathmini aliyokwenda kufanya Arumeru na ijulikane wazi na pili, kwa sababu ameitaja CHADEMA awakabidhi nakala ya ripoti kamili aliyoifanya, vinginevyo watachukua hatua.
Mnyika aliwatahadharisha wananchi wa Arumeru Mashariki, kukumbuka kuwa wakati wa kampeni, viongozi wa serikali wamekuwa na kawaida ya kutumika propaganda kusaka ushindi.
“Wanataka wananchi wa Arumeru, wajifunze kilichotokea Tarime mwaka 2008, waliamua kuwa na mshikamano, wakapuuzia propaganda wakaamua kuchagua CHADEMA,” alisema Mnyika.
Kwa mujibu wa Mnyika, Machi 3-4 watafanya uteuzi na si kuangalia propaganda kama za Tendwa. Hivyo kuwataka wazee wa Arumeru Mashariki kuwaunga mkono ili kazi waliyoianza mwaka 2010 ilete manufaa.

Source:Tanzania Daima
 
Tendwa na kampeni za CCM,
Uhuru,habari leo na propaganda,
Ila tutafika tu.
 
Lema doesn't need any permission to campaign for anyone....
 
Udini na Ukabila ni kama kula nyama ya mtu.Mkuu mnataka kuleta ya Igunga tena?

Kamanda Andengeye hiyo haitoshi. Mkamate Tendwa ili atoe maelezo (under oath) juu ya wazee wa Arumeru wanaotishia kumdhuru Lema, na baadaye wazee hao wa kimeru nao wahojiwe. Leo hii Lema akidhurika Tendwa atatakiwa kutoa maelezo maana tayari ameonana na watu (wazee) waliopanga kumdhuru Lema.
 
hii habari ilishawekwa hapa jamvini jana! Ila basi naona unaweka msisitizo siyo mbaya.

tendwa njaa inamsumbua, hata hajui wajib wake ila haya yatakwisha! Vyeo vya kupewa miaka michache ni taaluma yako na uwezo wako wa kuperform kwenye interview utakuweka pale!sio fulani kamkuadia fulani basi anamtunuku cheo, nonono haya soon yanaisha!tumeelimika watanzania!viva chadema!
 
Kamanda Andengeye hiyo haitoshi. Mkamate Tendwa ili atoe maelezo (under oath) juu ya wazee wa Arumeru wanaotishia kumdhuru Lema, na baadaye wazee hao wa kimeru nao wahojiwe. Leo hii Lema akidhurika Tendwa atatakiwa kutoa maelezo maana tayari ameonana na watu (wazee) waliopanga kumdhuru Lema.

Ni kweli mkuu.Inatakiwa kamanda Andengenye amfungulie faili akatoe ushahidi
 
Back
Top Bottom