Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Kwa umri wa Tendwa kukurupuka na kuongea mambo ya aibu kama yale ni kituko...!
Sijui kwanini anashindwa kuelewa kuwa anaharibu heshima yake uzeeni.
 
Maajabu ambayo utayapata Tz peekee; Lema aongee maneno ya kuudhi (haielezwi ni maneno gani na yamemuudhi nani!) Familia ya wafiwa isilalamike, hao wazee wasilalamike, ila Tendwa asiye mkazi wa Arumeru wala mkoa wa Arusha au Manyara aibuke ghafla kuwa msemaji wa wazee wa kimeru!!! Hivi hawa watawala waliovimbiwa na wenye roho za kichawi tutawawajibisha lini???
 
umetumwa na magamba nini?kaungane na huyo tendwa kuwaomba msamaha wana nchi na wana cdm kwanza.
 
Kwa maelezo ya Tanzania Daima 25 Feb 2012, kilichowaudhi 'wazee wa kimeru' sio maneno aliyosema Lema (maana Lema hakusema kitu) ila hawakupendezwa na kitendo cha vijana kumzunguka Lema mara alipofika kwenye msiba wa marehemu Sumari! Sasa sijui kwa nini wamkasirikie Lema na sio hao vijana.

Mimi nadhani hawa wazee wa kimeru ni kweli walimwambia Tendwa kwama Lema ameaudhi na hata kutoa tishio. Ila kama ilivyokuwa kwa Pinda na mgomo wa madaktari hawakutarajia reaction ya watu. Sasa wanaanza kumgeuka Tendwa. Kama kweli hakusema next time kwenye meeting yao chini ya Mringaringa waape (kimila) kuwa hawakusema chochote kwa Tendwa.
 
bila kumsema lema huwa hamliziki napenda ujue kuwa kwa upande wa ccm hakuna mtu kama lema
 
Mkuu nimefanikiwa kuongea na baadhi ya wana familia wa Sumari wanashangaa sana haya mambo yanavyo kuzwa wanasema watakapo kutana tarehe 29.02.2012 wataangalia namna ya kumshitaki Tendwa...

Yanavyokuzwa je? Inamaana ni uongo au?
 
Mkuu nimefanikiwa kuongea na baadhi ya wana familia wa Sumari wanashangaa sana haya mambo yanavyo kuzwa wanasema watakapo kutana tarehe 29.02.2012 wataangalia namna ya kumshitaki Tendwa...

Wazee wa Kimeru ni watu wastaarabu na waelewa sana, pia siyo watu wa kusemewa na wapumbavu wa magamba kama akina Tendwa. Wakiamua kufanya jambo hakuna mtu anaweza kuwazuia. CCM wanatapatapa sana, kumbukeni uhuni walioufanya Igunga kwa kuwatumia wazee wao eti ni kauli ya waislamu wa Tabora kuhusu kilemba cha demu wa Alhaj Sheikhe Profesa Othman wa Urambo.
 
Kwa umri wa Tendwa kukurupuka na kuongea mambo ya aibu kama yale ni kituko...!
Sijui kwanini anashindwa kuelewa kuwa anaharibu heshima yake uzeeni.


Katiba mpya lazima iseme wazi kuwa uongozi is a public trust (nimekosa kiswahili chake). Mtu akipewa uongozi sharti atunze heshima ya hicho cheo na akilinde kisiaibike, wala kuonekana vibaya mbele ya jamii
 
wanamuogopa hata kumuona wanajua akionekana tu moto umewaka na huyo tetwa si ndo makamu mwenyekiti wa ccm
 
Kwa mawazo yangu tusiangalie tu uchaguzi wa Meru, bali busara kwa ujumla wake. Namuomba Mh. Lema kama ni kweli aliongea maneno ya kuudhi msibani na hao wazee wa Meru wakasikia, akawaombe radhi wayamalize. Najua hata kama asipoomba msamaha hakuna litakalotokea, na hao wazee hawawezi kumzuia asifanye kampeni kujiandaa na uchaguzi wa Meru, kwani kila mtu ana uhuru wa kwenda popote Tanzania hii, ila napendekeza busara itumike zaidi. Ni vizuri kujishusha wakati mwingine, pale tunapokosea hata kama tunayo support ya kutosha kutoka kwa wananchi.
tukumbushe LEMA aliongea maneno gani yakuwaudhi wazee?
 
Hao ndo wasimamizi wa uchaguzi huru na wa haki? Ndo washauri wakuu wa marekebisho ya katiba? Ndo JK anawategemea anapozurura ughaibuni kusaini mikataba ya kugeuza Tz magereza ya kimataifa?
 
kweli hawa wazee wa ccm wanazeeka vibaya-hata aibu hawana-wapo kama wamechanganyikiwa-wanazungumza pasipo hata kujua nini wanazungumza
 
pm me your foolishness and you will feel the vibe
 
Huyu babu huyu katumwa na magamba kuharibu hali ya hewa na uzuri wenyewe wamemkana kwa hyo ni aibu kwake na wajukuu zake plus the whole family
 
Nashukuru kuwa hao wazee wamekanusha, hii ni wazi kuwa kuna punguani mmoja amekula makaisari ya Mwigulu Nchemba ili ampake tope Lema na Chadema kwa ujumla. Tunawaomba hata hao wazee watakapokaa kikao tarehe 29 mwezi huu wawe makini kwani jamaa hawakawii kuwahonga ili wamchafue Lema na CDM kama chama kwa kuwa tu ccm ina pesa kuwahonga. Tutakapobaini hata harufu ya rushwa hatutasubiri TAKUKURU wawakamate, sisi wenyewe tutatosha.
 
Back
Top Bottom