mgomo:WAALIMU KENYA WAONGEZEWA MSHAHARA 300% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mgomo:WAALIMU KENYA WAONGEZEWA MSHAHARA 300%

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bilionea Asigwa, Sep 24, 2012.

 1. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imekubali kutoa nyongeza ya asili mia 300 kwa mishahara ya walimu ambao wamekuwa katika mgomo wa kitaifa kwa wiki tatu sasa.

  Kutokana na maafikiano hayo kati ya serikali na chama cha walimu nchini KNUT, sasa walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu. Hatua hiyo sasa itawapa afueni maelfu ya wanafunzi hususan wa shule za msingi na upili za umma ambao hawajafunzwa wakati huu walimu walipokuwa mgomoni.

  Vyama vya walimu nchini Kenya KNUT na Kuppet vilikuwa vikishinikiza serikali kuwalipa walimu nyongeza hiyo kwa awamu moja. Awali serikali ya Kenya ilikuwa imekataa kutekeleza matakwa hayo na kuwataka walimu kukubali kulipwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikitekelezwa Oktoba mwaka huu.

  Mwalimu wa chini aliyekuwa akipata shilingi 13,000 sasa atapata shilingi 39.000. Serikali ya Kenya imetenga zaidi ya dola 159 milioni kuwalipa zaidi ya walimu 250,000 ambao walikuwa wakigoma kulalamikia mishahara duni na mazingira mabaya ya kazi.

  Source:BBC SWAHILI

  MY TAKE:Hapa bongo mbona waalimu wanapigwa changa la macho sana ??
   
 2. KATUMBACHAKO

  KATUMBACHAKO JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh . .! Kumbe hata hapa kwetu wangekomaa wangeongezewa ile 100% ! 13,000 x 15 = 195,000hadi 39,000 x 15 = 585,000 za kitanzania! Hapa kwetu thubutuuuu . . . ! Wanapenda kula kweli viongozi wetu,hawawajali walimu
   
 3. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo ualimu Kenya ni deal sijui nihamie Kenya ili nikafundishe huko
   
 4. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Mbona umetumia exchange rate ambayo siyo?? Kiwango halisi ni Shs 1 Kenya = Shs 18.4 Tanzania na siyo Sh 15 kama ulivyoweka. Au una maana hiyo Shs 3.4 siyo kitu?? Fanya home work yako vizuri, rejea http://www.bot-tz.org/
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kama migomo yenyewe ndio kama ile ya madaktari, bora wasigome. Hii mambo ya kugoma na kuishia njiani na kuanza kuomba msamaha desperately kama mtoto, haifai wala nini!
   
 6. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kima cha chini mwalimu wa kenya ni 39000*18.4=717600. Hakyamungu narudi kenya uwalimu dili.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Na hiyo nyongeza aise kwenye nchi ambako hadi leo shs moja bado inanunua bidhaa sokoni ni kubwa sana aise.
   
 8. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nitamshauri mdogo wangu aende Kenya akafundishe.
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Hapa kwetu ni ngumu sana!!!!
   
 10. cpt

  cpt JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Kweli ualimu ni taaluma katika nchi za wenzetu,ila bongo mmmmmh......bado wiTO!!!!!!
   
 11. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,125
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  bongo hyo kitu haiwezekani joh,unajua kwa nn,wengi wa walimu wetu vyeti vyao vya shule ni vya kimagumashi na ndo maana hawajiamini hasa hawa walimu wa .com,we fanya utafiti utang'amua hili tu
   
 12. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Aibu sana kwa watanzania,ni nani alituloga?haiwezekani eti kuna watu wanaionea huruma sirikali wakati ni choka mbaya na familia zao.
   
Loading...