samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
huo ni mwanzo tu najua viongozi wa chuo huwa wanajaribu kutumia kila mbinu ili UDOM ionekane haina migomo na mara nyingi waandishi wa habari wa dodoma wamwkua wakipewa kitu kidogo ili kuficha ukweli. ukweli ni kwamba usanii umezidi chuoni hapo hata hao wanafunzi wa education walioenda field walifanyiwa usanii tu walimu walioenda kuwafanyia assessment walipewa wiki moja kukamilisha zoezi hilo kitendo ambacho kilisababisha walimu kufanya table assessment bila kuhudhuria darasani kuona jinsi walimu wanavyofundisha. UDOM ina matatizo mengi sana ya kiutawala ambayo yasipochukuliwa hatua wahitimu wa pale hawatakua na dili katika soko la ajira. Uongozi ulifikiri unaweza kuwadhibiti wanafunzi hao siku zote likini wanatakiwa wafahamu kwamba chuo hicho kina wanafunzi wengi sana na hivyo wasifikiri wataweza kuwanyamazisha kitu cha msingi inabidi wawatatulie matatizo yao. nimesikia mpaka muda huu vita inaendelea kati ya FFU na wanafunzi ambao wanafanya mashambulizi yao kutokea kwenye vichaka na mapori yaliyokizunguka chuo hicho.