ZeMarcopolo binafsi siungi mkono mgomo wa
Mzee Mwanakijiji lakini si kwa sababu ulizotaja wewe. Kama mwandishi wa makala wa muda mrefu, Mwanakijiji amefanikiwa kuwadanganya Watanzania walio wengi kwamba yeye ana weledi mkubwa wa mambo mengi, lakini nilipompa changamoto ndogo tu ya kujibu hoja yangu kwa nini mgomo wake ni wa kifisadi, ameshindwa kunijibu kwa ufasaha. Inaonekana hata hiyo lugha ya Kiingereza inampiga chenga, kwani ni dhahiri kwamba anaendekeza ufisadi na uzandiki zaidi, kuliko uzalendo.
Badala ya kuwatia hasara wenye kumiliki mitandao ya simu, mgomo wake huo utawapa faida zaidi. Sitaki kurudia jambo ambalo nimeshalielezea mara kadhaa, lakini kwa bahati mbaya wapo Watanzania wengi ambao wameingizwa mkenge na kuamua kuunga mkono mgomo huo. Kumbe wamegeuzwa kondoo wa kafara altareni.
Nishasema, atakayezima simu kwa hizo siku tatu, ajue kwamba imekula kwake na yeye ni fisadi pia.
Sitaunga mkono ufisadi. Line zangu mbili za Airtel na Vodacom zitabaki hewani.
Mwanakijiji, utahukumiwa hapa hapa duniani kwa ufisadi wako. Siku zako zinahesabiwa. Amini usiamini, Mungu yupo na haitwi Athumani wala Petro!