Mgomo wa madaktari - Updates


Hayo maneno ungeiambia serkali ningekuelewa! Kuingia lini sio hoja! Hoja hizi serkali za ccm zimeingia lini kutawala? Na kweli wanawajibika au wanawajibikia matumbo yao! Huzioni hata safari za mkuu wa kaya, zinavyo ibemenda nchi? Sikushangai hata kwenye kampeni ilani ya ccm ingekuwemo kwamba; Kipindi chote cha utawala wa miaka5 raisi atakuwepo ofisini kwa miaka2, iliyobaki atakuwa nje! Wewe ungempa kura ya ndio na ukaita ni uzalendo!
 
Jana nilikwambia kuwa safari hii mtakoma....mgomo uko pale pale

Hawa viongozi wa wana sisiem sidhani kama akili zao zimekaa sawa. Anatishia taalumu adimu siyo au kwakuwa wao wanajua Appolo na hospital nyingine za nje zipo? Sasa kwa mikakati hii tuwaombe nchi husika kiongozi yoyote kutoka Tanzania akienda kutubiwa apigwe sindano ya mtindio wa ubongo. Hili likifanyika watakaokuwa wamebaki watatenda haki kwa wananchi.

Pamoja na yote haya watu wanaona kwa macho lakini watu wa Arumeru bado wanakimbia na bendera za kijani hivi akili au matope?:lol:
 


Kweli kabisa,

Suala la kaingia lini hata aingie kesho kutwa jawabu linakuwa ni moja tu, "Ni WAZIRI WA WIZARA YA AFYA"

KWani alipoingia si alikabidhiwa ofisi?? ina maana unakabidhiwa na matatizo yote pamoja na mafanikio ya ofisi ile hivyo ni jukumu lako kuendeleza yale mafanikio na kutatua matatizo uliyorithi toka kwa aliyekutangulia.

huu ndio uongozi Bora unaotakiwa.

Najua wote mnaoshabikia Serikali hamna tofauti na PINDA aliyetuambia eti Mponda ana mwaka mmoja tu katika uongozi wa Wizara hivyo asilaumiwe!!!!!!!!! PTYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!!!!!!!!!! KAULI INATIA KINYAAAAA KABISA.

Kwa Kiongozi kama yeye hakupaswa kabisa kutoa kauli ile kwani inadhihirisha jinsi alivyo mbumbumbu katika kujua taratibu za UONGOZI WA KIOFISI.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 

Sipendi migomo na hasa huu wa madakatari wetu.....however........Hebu tuambie mbinu gani itumike zaidi ya mgomo............maana mbinu za kawaida i.e. mazungumzo zinashindikana na utekelezaji wake............

Nakubaliana na wewe kwenye suala la kuunganisha mgomo na kutaka kujiuzulu kwa Mawaziri.........hili sikubaliani nalo.........wagome kwa sababu zingine....sawa sio hii ya kutaka Mawaziri wajiuzulu........

kuunganisha suala la kugoma na kujiuzulu kwa Mawziri ni UKILAZA USIO NA KIFANI..............
 
"mzee wa upako na mgomo wa madaktari" hawa ni wauaji wakubwa muhimbili wagonjwa hawafi ila wanauawa! Please kwa yeyote aliye na c.v ya mchungaji anthony lusekelo atuwekee hapa jamvini tuweze kuasesi capacity thinking yake!:a s 465:

Mkuu hata mimi amenitatiza kwenye maelezo yake. Lawama zote ni kwa madaktari na posho lakini la vitendea kazi ambalo limo kwenye matakwa ya madaktari halisemi hata!
 
wewe ndiye kilazawa kwanza kwa sababu hujui umuhimu wa mawaziri kuondolewa unavyoinfluence muafaka wa madaktari
 
Utawataja hadi walioko kaburini miaka mia moja ilopita. Usiniambie unataka madoc walale njaa ili hao kina Pinda waendelee kupeleka watoto wao kusoma nje kwa wizi wa pesa za govern

hivi pinda kumbe na yeye mwizi!
Si anajiita mtoto wa mkulima!
Kweli msafara wa mamba.........
 


Ndugu sikufahamu vizuri;

Lakini napenda kukuuliza swali moja jepesi sana.

Hivi unakumbuka Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Waziri enzi za Uraisi wa Hayati Nyerere; Ikatokea makosa yaliyofanywa na watendaji wake, lakini Mzee Mwinyi kwa busara na bila kuambiwa na mtu yeyote aliamua KUJIUZULU UWAZIRI??


Endapo kama ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa bado kupevuka naomba waulize wanaokumbuka.

(Samahani kama nimeongea maneno makali)




MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Naona kuna haja ya kuamua as a nation viongozi wote kutibiwa ni umu umu nchini ili angalau gvt ianze kuwajari madr na kuwapa vtendea kazi na kuboresha mazingira ya kazi
 

Hivi waTanzania ni lini tutafunguka akili na kuacha kuendekeza ushabiki wa kizandiki katika suala kuwataka watu tunaowapa dhamana wawajibike!? Ni dhahiri kabisa kuwa hufuatilii hili sakata lilipoanzia wakati Intern doctors waliponyimwa stahiki yao kibabe na Wizara ya Afya na majibu ya kudhihaki taaluma ya uDaktari waliyopewa na CMO na Katibu mkuu..hali iliyopelekea MAT kuingilia kati, kisha Intern hao kulipwa na kutimuliwa Muhimbili. Hapo ndipo MAT ilipoitisha mkutano ambao pamoja na sakata la Intern ulijadili dhihaka za mara kwa mara wanazopata madaktari wakifuatilia maboresho ya maslahi yao pamoja maboresho ya huduma za afya wanazotoa kwa jamii.

Majibu ya dhihaka yaliyofutia hapo wakati MAT inafanya juhudi za kutatua tatizo toka kwa CMO, Katibu mkuu, Waziri na Naibu wake wizara ya afya nadhani kila mtu anayafahamu (kama Freema huyajui google utayapata, yaliandikwa everywhere) mpaka kupelekea mgomo! Waziri Mponda na naibu Nkya walidanganya umma wa waTanzania kupitia vyombo vya habari, walidanganya Bunge, walimdanganya na kumshauri vibaya waziri mkuu mpaka kupelekea kukurupuka mara ya kwanza kabla ya kujirudi.

Waziri wa afya na naibu wake, pamoja na wale wawili waliotimuliwa wamekuwa ni kikwazo kikubwa cha kuboresha maslahi ya madaktari na utoaji huduma za afya (hata kama wao hawakusababisha hali duni ya huduma za afya, kuzuia maboresho ni udhaifu)....hii imepelekea maDaktari kutowaamini na kuomba/kudai wajiuzulu au wawajibishwe. kitu ambacho waziri mkuu alikiri na kusema anamuachia rais aamue...rais haamui muda unakwenda, na papo hapo wanataka tuendelee na mchakato wa maboresho...kivipi, wakati hawa waliokuwa kikwazo ndio wasimamizi wakuu kwa upande wa serikali na hatuwaamini?! ili mchakato wa maboresho uendelee huku maDaktari wakiwa na imani na serikali, hawa wawili waliokuwa kikwazo waachie ngazi....

Nadhani sasa Freema umeelewa...anza kuchangia kuanzia hapo...acha kubwabwaja, wewe pamoja na wenzako mnaobwabwaja!
 
Madaktari Hatuna haja tena na Waziri mkuu! Kikwete aje kuongea na madaktari
 
Mkuu Bitabo kuna wengine humu hilo sio tatizo !

Mkuu MANI hao nadhani ndo wale ambao hata akipata chunusi usoni anaitwa ambulance ya Knight Support kuwahishwa Agha Khan. Wakuu huku vijijini hali ni mbaya yaani haielezeki.

kwenye vitanda wodini hata yale mashuka ya MSD yamechakaa mpaka yanafanana na magodoro.
wakina mama wanaotaka kujifungua wanalazwa chini, vitanda vimeisha wodini. mara wanaambiwa waende na vifaa vyao hospital.
Mtu anaumwa malaria hata dawa mseto dr hawezi kumpa maana hamna. Anamwambia aende pharmacy mtaani
Unaenda maabara wanakwambia umeme hamna hatuwezi kufanya vipimo. umeme ukichukua siku mbili bado kuna mgonjwa kweli hapo???

Eti serikali ina mpango wa kukabiliana na mgomo. Kwa kuleta dawa na vifaa au kumaliza ardhi kwa kuchimba makaburi??
 
Madaktari Hatuna haja tena na Waziri mkuu! Kikwete aje kuongea na madaktari

Mdugu yangu;

Hayo aliyoyasema Pinda ndiyo kauli rasmi ya JK.

Pinda ametumwa tu kufikisha ujumbe ingawa alikuwa anajifanya kuongea hadi mishipa ya shingo inasimama, lakini ilikuwa siyo kauli yake.

Kauli ya Pinda ilikuwa katika mgomo wa kwanza ambapo kwa kinywa chake alisema kuwa "Serikali imechukua hatua ya kwanza kuwasimamisha Dakitari Mkuu na Katibu Mkuu, hatua ya pili itakuwa ni kuwasimamisha Mawaziri wa Wizaara"


Kitu ambacho juZi amekipinga, yaani amepinga maneno yake mwenyewe. Na hii ni kwamba alipomwambia JK aliikataa hoja yakuwasimamisha na ndio maana nasema kuwa aliyosema juzi Pinda ni kauli ya JK.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 

msome huyu
 

Maneno mazito hayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…