Mgomo wa madaktari na kiburi cha watawala wetu, nani anaumia?

Katika pita pita zangu kwenye baadhi ya hospitali madaktari wengi wamemshukuru Mh Pinda kwa kuwa rahisishia kazi kwani wanasema siku mpya inaanza saa sita usiku basi madaktari wote wataacha kufanya kazi ifikapo saa sita usiku leo hii asubuhi hospitali zitakuwa nyeupe. Sitataja hospitali wala majina ya madaktari hao kwa usalama.
Mwana JF jichunge usije ukapata matatizo baada ya saa sita usiku inawezekana usipate huduma yoyote.

Nchi hii inakwenda wapi?
 
So "hautafanikiwa" kama ule wa kwanza eehhh!

Ule wa kwanza ulikuwa unaeleweka, ingawa sio madaktari wote waliogoma ila huu wa sasa umekaa kisiasa sana ndo maana bado narudia kusema "NAHISI" 85% hautafanikiwa.
Labda kama ungekua umeitishwa na
nyie walimu wa primary schools
Mwisho wa siku wagomaji ni madaktari wenyewe sio sisi tunaogoma kwa kutumia keyboard za computer..
 
Yote sawa lakini ni wizara gani waziri alibadilishwa tukapata matokeo tofauti?..Hawa wote wanatekeleza sera zile zile na yaleyale waliyoagizwa kuyafanya. Kila kiongozi toka mawaziri, wabunge, hadi mwenyekiti wa kata ni Mheshimiwa wataachaje kulewa madaraka!

For this case Mkandara acha waanze hawa kuwajibishwa kwa shinikizo, it'll be ana alarming note hata kwa "waheshimiwa" wengine kutambua they're being watched utendaji wao na kwamba likisanuka hata aliyewateua hawezi wabeba.inaweza ongeza uwajibikaji kiasi flani.wamezidi kujiona miungu watu mKuu!
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Kwa mantiki hiyo kwa nini wameachiwa madaktari peke yao kufanya jukumu hilo na wananchi wapo kimya?!
 
Amechanganya za kwake, za bochi wake za washauri wake na za mbayuwayu. sasa hapo kama zingekuwa za kwake tu sijui ingikuwaje!
 
waziri mkuu alitoa ahadi za serikali mbele ya camera na vyombo vya habari kama televisioni na redio sema kama una lingine achana na mambo madogo na leo kajitokeza tena iweje tunabeza juhudi zake?
 
Tunapoteza muda kwa kuongea na mfuga mbwa badala ya mwenye mbwa, sisi ndio wenye mbwa tunachelewa tu ni kuifutilia mbali hii serikali ya kishikaji ya JK na nduguze, dawa ni moja tu, wakati huu sio wa kushindana bali kushikan, pamoja na ufisadi wake tumuingize captain Lowasa mfanya maamuzi mjini maana hata FFU hawatathubutu kumpiga mabomu, tusonge nyuma yake tumpeleke ikulu katika kipindi hiki cha mpito, pamoja na matatizo yake yawezekana akawa ni ukombozi wetu tuachane na huyu handsome boy with no brains, hana utu anatufanya wote sisi wapumbavu na sisi tumebakia tunakuomba, ohh kuwa na huruma, aitoe wapi wakati pepo kasimama tops hebu tufanyeni maamuzi leo hii there is no tomorrow, jamani

haya mambo ya Haji Mponda na mwenzake Lucy Nkya ni matokeo ya kuwa na mawaziri washilikina.100% vyeo vyao vimetokana na nguvu za giza kufanya kazi na hata pale walipobolonga wao hawakuona ni kosa bali ni sawa tuu. hapo mganga kawahakikishia kukaa madarakani wawe wameikosea heshima jamii au lolote baya. wao moyoni husema kama Ngereja na wizara yake wamebolonga na bado wapo madarakani, iweje na sisi tuachie ngazi?
 
Bora hata Magufuli angekuwa PM kuliko huyu mzee wa porojo!
Mkuu wangu hapo awali nimeandika namkumbuka waziri mkuu Lowassa kwasababu yeye na mkulu walikua marafiki na alikua anaelewa udhaifu wa rafiki yake,ili jambo lisingefikia hapa,Lowassa angemkinga rafiki yake na aibu hii inayokuja! Toka kujiuzulu kwake bwana mkubwa amebakia mbele bila mtu wa kumkinga na aibu kama hizi!!
 
Mimi binafsi siwalaumu Nkya na Mponda,hapa naona Mungu anawatumia ili Tanzania ikombolewe,hasira yako na yangu kwa ndugu zetu itabadirisha mfumo mzima wa nchi yetu.
 
waziri mkuu alitoa ahadi za serikali mbele ya camera na vyombo vya habari kama televisioni na redio sema kama una lingine achana na mambo madogo na leo kajitokeza tena iweje tunabeza juhudi zake?

unaweza kuwa unafanya jitihada za kumtahiri paka, mwenyewe utajiona uko biiiiiiiiiize, huyu pinda bwana!!! aibu tupu, inafika wakati tunaona aibu kujitambulisha kwa utanzania wetu.
 
Narudia tena, ni selfish, ruthless and stupid to say the least! Kama hawataki kutoa matibabu wakatafute kazi zingine wafanye. Wanaweza kuwa wajasiriamali, madereva wa taxi, daladala, wakafungua maduka, ukulima nk

Kama Tanzania kuna matibabu kwa nini wakubwa wanaenda Apollo? Wanafuata nini na kwa nini? Ni vizuri wanasiasa kama Pinda kuacha ku-spin madai ya madaktari. Madaktari wamechoka kushughudia wagonjwa wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa dawa muhimu. Wamechoka kutibu wagonjwa wakiwa wamelala sakafuni. Kwa nini serikali inatumia hela za watanzania wanyonge kupeleka wakubwa wachache India?
 
mbona swala la posho ya bunge ilitatulika haraka,swala la madaktari wanaipuuzia tu
 
Madaktari wataojidai kugoma ndio watujuwa Watanzania kuwa hatutaki kuchezewa, tunaenda kuwashughulikia wao kwanza, halafu Serikali itutafutie madaktari kutoka India ituletee, wamejaa tele ni kiasi cha kukodisha ndege 5 zinajazwa madaktari wanakuja.

Within 24 hours huduma bora kuliko za hawa wajivuni.
 
Wale wahindi wa rotary club kama kweli huwa wanawasaidia watu kwa dhati wawasaidie na hawa wagonjwa watakao telekezwa na ma dr few hrs to come wawapeleke appollo nao wakatibiwe
 
Madaktari wataojidai kugoma ndio watujuwa Watanzania kuwa hatutaki kuchezewa, tunaenda kuwashughulikia wao kwanza, halafu Serikali itutafutie madaktari kutoka India ituletee, wamejaa tele ni kiasi cha kukodisha ndege 5 zinajazwa madaktari wanakuja.

Within 24 hours huduma bora kuliko za hawa wajivuni.

unaongea pumba hivi umefikiria gharama ya kuwalipa hao wa India??????????????? na usafiri???????????????

acha wagome, upuuzi wa serikali kudanganya watu kama mnavyopewa wewe na wenzako pipi mnaenda kupiga kura, walalalie nyie
 
Madaktari wataojidai kugoma ndio watujuwa Watanzania kuwa hatutaki kuchezewa, tunaenda kuwashughulikia wao kwanza, halafu Serikali itutafutie madaktari kutoka India ituletee, wamejaa tele ni kiasi cha kukodisha ndege 5 zinajazwa madaktari wanakuja.

Within 24 hours huduma bora kuliko za hawa wajivuni.

Hiyo ndoto na wala haitakuja kutokea!! Kila nchi inawahitaji madaktari tena inawezekana huko unakodhani kuna madaktari wengi sivyo ndivyo. Wanaonekana kwa sababu nchi zao zinawajali na zinawatafutia vitendea kazi ambvyo nchi yetu imeshindwa.
Isitoshe uwezo wa kuwalipa hao madaktari wa kukodiwa serikali haina kama imeshindwa kuwalipa wazawa itaweza kuwalipa wageni??
Pole kwa kuota huku unatembea!!
 
umejitahidi sana kuchota maneno ya kuchochea mfarakano lakini Pinda kaongea maneno ya busara umeyaacha ili kutimiza ndoto yako ya kugombanisha serikali na madaktari.

Kumbuka na sisi tumemsikiliza Pinda

Mama Porojo tafadhali ongezea nyama katika habari hii walau wengine tupate picha kamili...........
 
Back
Top Bottom