Mgomo wa madaktari na kiburi cha watawala wetu, nani anaumia?

Mgomo sasa umetangazwa rasmi kuanza leo. Ananilea , Bisimba na Namala shangilieni maana sasa muda wa kuvuna damu kule Muhimbili, Temeke na Mwananyamala na Kwingine umewadia ili mkaiwasilishe kwa donors wenu , FREEMASONS.
Tutakwenda Makaburini tutatupa udongo na kusema Mungu aliwapenda akawaleta duniani ,lakini BISIMBA, ANANILEA na NAMALA wamejifanya miungu watu na kuwaua. Mungu awalaze mahali pema peponi Amina.

Rubish
 
Katika hili la wanaharakati binafsi nimeshindwa kutambua hasa Taasisi kama LHRC wanasimamia lipi hasa katika objectives zao. Manake naona kama wanafanya vise versa badala ya kusimamia HAKI za binadamu wao wamegeuka kupigana na Serikali kwa kutetea upande ambao unaweza leta athari kwa binadamu na kupoteza ila HAKI ambayo wao wanapaswa kuisimamia. Mimi nilidhani mtu kama Hellen Kidjo wakati huu pamoja na Serikali kuonesha ugumu wake yeye pia angeanza kwa kutafuta namna ya kuzungumza na Serikali kama mwakilishi wa kituo ili awe kama Mediator manake najua ana nafasi kubwa ila haya matamko ya "tunamtaka" "tunamwagiza" mi nadhani ndiyo yanayozidisha sintafahamu.
 
ole wenu wanaharakati 2015 tuone mnagombea ubunge ama urais. Tutajuwa kama kweli mlikuwa mnawekeza kisiasa kwa kupitia mgongo wa matukio yanayoendelea humu nchini.
 
Wananchi na wanafunzi wakigoma mnadai Chadema, leo madaktari mnadai wanaharakati, wakija maaskari wagome mtadai ni "KALAMU YA MWIGAMBA". Tafuteni suluhisho la matatizo sio lawama kwa watu wasiohusika.
 
Mgomo sasa umetangazwa rasmi kuanza leo. Ananilea , Bisimba na Namala shangilieni maana sasa muda wa kuvuna damu kule Muhimbili, Temeke na Mwananyamala na Kwingine umewadia ili mkaiwasilishe kwa donors wenu , FREEMASONS.
Tutakwenda Makaburini tutatupa udongo na kusema Mungu aliwapenda akawaleta duniani ,lakini BISIMBA, ANANILEA na NAMALA wamejifanya miungu watu na kuwaua. Mungu awalaze mahali pema peponi Amina.
images
 
Mkuu wekomaa na propaganda zako sisi tukomae na haki tuone nani atashinda we endelea kupiga domo badala ya kusolve tatizo tuone mwisho wake mkuu.
 
ole wenu wanaharakati 2015 tuone mnagombea ubunge ama urais. Tutajuwa kama kweli mlikuwa mnawekeza kisiasa kwa kupitia mgongo wa matukio yanayoendelea humu nchini.[/
Hoja kaka hapa ni kutatua matatizo ya madaktari kwanza sasa mlitaka watu wafanye kazi bure mmesahau anayekuza mambo ni serikali yenyewe kushindwa kutatua tatizo linapojitokeza hapohapo huliacha likuwe sasa suala la mtu anayesema atagombea ubungea au urais sisi hiyo haituhusu tunaangalia mantiki yakile mtu anakisema kuhusu tatizo lililopo mkuu wanaharakati kwa sasa wanahoja ya msingi ambayo nyinyi wala nchi mnajifanya vipofu hamuioni mnakalia vipropaganda tu.
 
Ndugu zangu,

Ni heri hekima inayokuja kwa kuchelewa kuliko inayokosekana kabisa.

Maana, ni heri kutibiwa na daktari aliye kazini na moyo mkunjufu kuliko kutibiwa na daktari aliyelazimishwa kwa nguvu kurudi kazini huku akiwa na kinyongo. Wahenga walinena; unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kuyanywa maji. Hilo la mwisho ni la hiyari, kama ilivyo kwa tabasamu, kwamba unaweza kumlazimisha mwanadamu kupiga makofi, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kutabasamu, hilo la mwisho latoka moyoni.
Kuna habari za kusikitisha kwa Watanzania, kuwa madaktari wetu wamo tena kwenye mgomo.

Gazeti Mwananchi ( Mtandaoni) linaandika; ” Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Waziri mkuu Pinda alisema Serikali haioni sababu ya kuwawajibisha mawaziri hao kwa sasa na kueleza kushangazwa kwake na hatua ya madaktari hao kugeuza suala hilo kuwa dai namba moja hivi sasa.

“Hivi kweli mnataka nifike mahali nimwaambie Rais (Jakaya Kikwete) tunakupa saa 72 uwafukuze kazi viongozi hao? Hapana... hapana... hapana kwa lipi hasa? Siwezi kumwambia atekeleze hayo. Ingekuwa hatujafanya chochote sawa, hata angekuwa mtu yeyote hawezi kukubalina na hayo unless (vinginevyo) wenzetu madaktari watuambie wana hoja nyingine.”

Pinda alisema Dk Mponda mwenyewe anayelalamikiwa ndiyo kwanza ana mwaka mmoja na nusu kazini na hata madai mengine hayajui kwa kuwa hakuwepo wakati huo akisema shinikizo la kutaka awajibishwe ni kumuonea.

Alipoulizwa endapo mawaziri hao wataamua kuwajibika wenyewe ili kunusuru maisha ya Watanzania Serikali itakuwa tayari kwa hilo, Pinda alihoji: “Kwa lipi hasa? Naona ni vyema tusubiri majadiliano, hayo yote yatajulikana baada ya kufikia mwisho.”

Waziri Mkuu aliwataka madaktari kutumia busara, hekima na uzalendo na kuendelea na kazi kama kawaida wakati Serikali inaendelea na majadiliano na viongozi wao. ( Mwananchi Mtandaoni, Machi 8, 2012)

Naam, kinachoonekana hapa ni ukweli, kuwa mgogoro wa madaktari na Serikali umeingia katika hatua nyingine mpya. Na hii ni hatua mbaya zaidi, maana, pande zote mbili zinaonekana kujichimbia mahandakini tayari kwa kujipanga kwa vita kubwa zaidi. Vita isiyo na tija.

Huu ni mgogoro na si kitu kingine. Na majeruhi wa kwanza kwenye mgogoro kama huu ni UKWELI. Katika vita yeyote iwayo, risasi ya kwanza huelekezwa kwenye ukweli. Ni hapa ndipo propaganda huchukua nafasi yake. Lakini, kama ni vita, hivi vitakuwa ni vita vya kiwendawazimu, maana, havitatoa mshindi. Na katika vita hivi, sote, kama taifa, tayari tumeshashindwa. Je, tunataka tushindwe mara ngapi?

Tumeona jana kupitia televisheni jinsi wagonjwa wanavyotahabika kwa kukosa tiba. Kwanini raia wasio na hatia wafe kwa vile watu wazima kwenye pande mbili kwenye mgogoro zinashindwa kufikia muafaka wa namna ya kwenda mbele? Inasikitisha sana.

Ushauri wa nini kifanyike;

Hatua hii inahitaji busara na hekima zaidi. Walikofikia madaktari kwenye mapambano yao na Serikali haifikiriki kuwa watarudisha’ majeshi’ nyuma. Na walipofikishwa Serikali na madaktari haifikiriki kuwa kuna Waziri au Naibu wake atakayejiuzulu ili kumaliza mgomo. Upande wowote utakaomkubalia mwenzake katika hatua hii utatafsiriwa kuwa umeshindwa.

Na position ya Serikali inachangiwa zaidi na hofu ya domino effect. Hilo linaeleweka ukiingia kwenye fikra za Serikali. Athari ya kidomino ina maana ya badiliko moja hata likiwa dogo linapelekea badiliko lingine, na lingine na lingine. Hatma yake ni mparaganyiko wa jumla.

Sasa basi, cha kufanya katika hatua kama hii ni kwa pande mbili kuepuka kuendesha mapambano yao hadharani. Maana, hakuna upande ulio tayari kwa sasa ’ kutua mbanji’ – kuweka silaha chini bila kufunika sura- face saving.

Mantiki hapa, ni kuwepo na njia ya tatu; kwamba pande zote mbili ’in a closed door dialogue’- mazungumzo yasiyoruhusu media kuwepo na hata kutangaza, kufikia makubaliano ya kudumu, ya kimaandishi ya namna ya kwenda mbele; hivyo basi, kwa pamoja, na kupitia taarifa ya pamoja- joint communique kutangaza muafaka na na hivyo ’ kutua mbanji’ huku sura zao zikiwa zimefunikwa.

Kwa mantiki hiyo, wanayohitaji madaktari yafanyike yanaweza yasifanyike kesho , lakini yakaja kufanyika kwa namna nyingine, kwa makubalino kama yasipofanyika, wahusika wa upande mmoja wa kwenye makubaliano wataitaarifu pande nyingine kiamandishi na bila kupitia media, kuwa walichokubaliana kifanyike hakijafanyika na kuwa wamekubaliana kisipofanyika nini kifanyike na ndicho kitakachofanyika.

Na kitapofanyika upande mmoja utakaolalamikiwa juu ya kwanini umefanya walichokifanya utakuwa na uthibitisho wa kuuleza umma kuwa umefanya ulichofanya kwa vile upande mwingine umekiuka makubaliano ya kimaandishi na umekubaliana nao kimaandishi juu ya hatua waliyoichukua.

Hivyo basi, tulipo sasa, pande mbili kwenye mgogoro huu hazina budi kurudi kenye meza ya mazungumzu huku wakitanguliza busara, hekima na maslahi mapana ya taifa. Wawe in a closed door na kuanza upya mazungumzo yatakayopelekea makubaliano ya kimaandishi.

Wahenga walinena; kwenye wengi hapaharibiki neno. Ni matarajio yetu, kuwa hatma ya mazungumzo kama hayo itakuwa ni kutolewa kwa taarifa ya pamoja kwa umma, na bila shaka itakuwa ni pande zote mbili kukubaliana kwenye mambo ya msingi na kuwa madaktari wanarudi kazini.

Maana, umma wa Watanzania kwa sasa hauna haja ya kuona nani mshindi na nani mshindwa, kwa vile tulipo sasa sote tumeshashindwa. Watanzania hawana haja pia ya kuona nani, leo au kesho , anatundikwa kitanzini na kunyongwa, bali, kuwaona madaktari wao wanarudi kazini na kufanya kazi wakiwa na mioyo mikunjufu.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Maggid Mjengwa,

Iringa
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Hapo ndipo penyewe watanzania wengi wanashangazwa na msimamo wa madaktari wa kumkataa waziri.waziri ni mmoja kati ya wafanyakazi wa wizara husika kama wafanyakazi wenzio hawakutaki na hasa wewe ukizingatia bkiongozi wao utafanyakazi nao vipi> wewe waziri wa afya unataka kuganda kama ruba achia ngazi.
Eti pinda anadai wamejipanga labda kweli wamejipanga kutuuwa lakini otherwise sioni labda tungoje nguvu ya umma iwashukie
 
Ndugu Maggid...logic ya kuja na makubaliano ya kimaandishi yenye commitments za serikali ni jambo ambalo serikali imekuwa inalikwepa kweli kweli na ndio maana kama umefatilia utakuwa umejua kuwa tume ya madaktari walikuwa wanaifailia ripoti ya serikali juu ya makubaliano ya kusitisha mgomo uliopita bila ya mafanikio.....kama hilo halitoshi ukifatilia madai ya madaktari utaona kuwa moja ya dai lao ambalo lilikubaliwa na pinda(si kimaandishi) wakati wa kikao kile cha CPL lilikuwa ni kuwatimua viongozi wa wizara..wakiwemo katibu mkuu na mganga mkuu ambao aliwasimamisha kazi na mawaziri husika ambao alisema atalipeleka kwa jk...Kinachoshangaza leo hii ni kumsikia huyu huyu pinda akisema mbele ya umma kuwa hawezi kumshauri jk awasimamishe kazi mawaziri na pia hili halikuwemo kati ya madai ya madaktari(eti ni dai jipya!!!!).......sasa kama mtu anaetegemewa kutoa majibu ya madai ya madaktari anakuwa kigeugeu kama mswahili tu layman wa mtaani we unategemea madaktari wafanyeje???????kama kiongozi aliepewa dhamana ya kutatua tatizo anawageuka leo madaktari..... hivi we unafikiri ni hatua gani itakuwa mbadala kwa madaktari?????????..ndugu yangu imefika sasa madaktari wameona kuwa kumbe hata yale madai yao mengine ya msingi ya muda mrefu inaweza kuwa ilikuwa magumashi tu ili watu wasitishe mgomo........sasa inabidi madaktari wasimame kidete ili kuondoa huu mzaha.....my support to the fellows......
 
In principle nakubaliana na madai ya madaktari juu ya maslahi yao.
Hata hivyo wamejiingiza katika mtego wa kisiasa, kwa kutaka kushinikiza kujiuzulu wanasiasa.
Thats dangerous.
Mwanasiasa anaishi kwa kupiga domo, na juhudi zozote za kumuondoa kwa domo ni lazima zitapata upinzani mkubwa sana.
Mbaya zaidi ni precedence ambayo madaktari wanataka kuiweka.
Nawashauri waachane na wanasiasa na waendelee kudai maslahi yao.
Wadau hapa JF,
I suppose nili predict muelekeo wa mgomo wa madaktari na nafikiri wameona muelekeo huo BAADA ya kukutana na JK mwenyewe.
Doctors , please stay advised.
 
Back
Top Bottom